Shukurani kwa wenye kuchangia hali hii ya mtoto wetu Nairat | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shukurani kwa wenye kuchangia hali hii ya mtoto wetu Nairat

Discussion in 'JF Doctor' started by abdulahsaf, Sep 10, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Matibabu ya Nairat

  Written by Stonetown (Kiongozi) // 10/09/2012 // Habari // No comments

  [​IMG]
  ASALAMU ALAYKUM.
  WAKATI tunaendelea kukusanya michango ya watoto wetu Nairat na Bisambe ambao wanasumbuliwa na matatizo ya ngozi, Napenda kutoa taarifa kwamba ahadi ya kwenda hospitali Nairat kulazwa ilikuwa ni tarehe 4 na kufanyiwa upasuaji ni tarehe 5 mwezi ujao inshallah lakini bahati nzuri kumetokea shirika la Kimataifa la Sight savers chini ya mradi wake wa huduma za macho Zanzibar litamdhamini matibabu ya macho Nairat na hivyo kwa sasa badala ya kusubiri mwezi ujayo matibabu yake yatafanyiwa mwezi huu inshallah, ambapo leo hii Nairat na Bisambe wanakwenda Dar es Salaam kwa ajili ya uchunguzi wa macho na hivyo huenda wakalazwa katika hospitali ya Muhimbili badala ya CCBRT na hilo ni kutokana na makubaliano kati ya madaktari wa CCBRT na Muhimbili.

  Lakini kwanza kwa kuwa Sight saves wanahusika na macho peke yake tena kwa watoto hivyo basi Nairat ndio atakayenufaika na huduma hii ambayo baada ya kufanyiwa vipimo na kukamilika taratibu zote basi atalazwa hapo Muhimbili na kuendelea na hatua zinazofuata za matibabu. Tumuombee dua inshallah afanikiwe na kila kitu kiwe chepesi kwa uwezo wake Jalali Mola wa uulimwengu wote.

  Na baada ya hapo tukishajua suala la macho sasa tutaendelea katika suala la ngozi na katika hilo watalazimika kufanyiwa vipimo wote wawili na tukishajua kitachoendelea tunaendelea kuarifiana lakini kwa sasa tunamshughulikia Nairat ambaye yeye anahitajika matibabu ya haraka kuhusiana na macho yake ambayo yameathirika na kuonekana kuwa ana kensa.

  Mwenyeenzi Mungu ndio Mjuzi na ndiye mweye uwezo wa kulifanya gumu kuwa jepesi hivyo dua kwa watoto hawa ni muhimu sana kwetu inshallah.

  Hadi tulipofikia hapa katika kushughulikia masuala la watoto hawa tunakwenda vizuri Alhamdulillah na mambo yote takriban yanakwenda kwa utaratibu mzuri na kwa wepesi kabisa tunamuomba Mwenyeenzi Mungu atupe nguvu ya kuendelea kushugulikia suala hili hadi kufikia kikomo.

  Kwa ufupi kabisa katika suala la hali ya Bisambe ambaye yeye ni mdomo wake ndio wenye kuwa na vidonda na kukatikakatika bado tatizo lake anaendelea nalo licha ya kuchukuliwa vipimo na kutumia dawa kadhaa lakini hajapata unafuu sana ila angalau kidogo hali yake sio kama awali kwa kuwa angalau anaweza kula vizuri kwa sasa ingawa sio nyakati zote hutegemea na yale maumivu anayopata.

  Kwa upande wa Nairat vidonda ndani ya macho vimepona, vidonda kwenye pua ndani na nje pia vimekauka ila vidonda katika mdomo bado vinamsumbua ingawa kwa kiasi kikubwa vinaonekana kukauka na kujirudia tena lakini ile kutoka damu tokea nilipomchukua nyumbani kwangu wili ya pili sasa sijaona hata siku moja kutoka damu na ulimi wake sasa naona upo safi vidonda vimekauka na angalau anakula vizuri, na ule mwili wake tokea kuanza kumpaka dawa na kutomruhusu kutoka nje amebadilika na sasa baada ya kufuata masharti ya kutokaa juani ameanza kubadilika rangi ule weusi yaani madodoa meusi katika mwili wake yameanza kufifia na nadhani akiendelea zaidi inshallah yatakwisha ingawa itachelewa lakini naamini atabadilika kwa uwezo wake Allah.

  Kuhusiana na fedha tulizopokea hadi sasa tumeanza kuzitumia kwa vipimo mbali mbali tokea walipoanza vipimo vya hapa hapa nyumbani Al Rahma, Mnazi Mmoja na hatimae huko CCBRT na leo huko Muhimbili na pia tumenunua dawa na vifaa ambavyo Nairat ametakiwa kuwa navyo kwa ajili ya kujikinga na jua pamoja na dawa maalumu ambazo anatakiwa atumie muda wote na hivyo risiti zote zipo yaani nakusuadia kwamba hakuna fedha ambayo inatumika au itatumika bila ya maelezo na wala hakuna fedha iliyotoka bila ya utaratibu wa matibabu.

  Mama Nairat yaani Bi Khadija Mohammed amekubali kutochukua fedha kwa kuogopea kuja kuzitumia kwa shughuli nyengine nje ya lengo yaani ‘matibabu ya watoto' na hivyo ameniachia mimi kwa ridhaa yake niwe nashughulikia masuala yote hayo. Nami kwa kuwa ameniamini naahidi kwenu nyote mliotoea fedha zenu kwamba fedha hizo zitatumika kwa malengo yaliokusudiwa na inshallah maana lazima tuweke msisitizo wa kumtangulia ALLAH mbele katika suala la fedha kwamba nitajitahidi malengo tuliokusudiwa yafikiwe.

  Kwa niaba yangu binafsi na mama mzazi wa Nairat Bi Khadija Mohammed tunawashukuru wote wale ambao wamekuwa karibu sana nasi katika jambo hili kwa kutoa michango yao mbali mbali, kifedha, usafiri, huduma na hata mawazo na kutupa fikra za kufanya katika kufikia lengo la tiba tokea tulipoanza mbio za kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya watoto hawa.
  Kwa kila hatua tutaelezana inshaallah

  Salma Said
  [​IMG][​IMG][​IMG]
  [​IMG]
   
 2. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Mungu ampe heri ili apone kabisa...
   
Loading...