Shukurani Kutoka kwa Mtambuzi kwa wana Jamii Forum.

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,393
Kama mlivyopata taarifa kutoka kwa mwana JF mwenzetu Cantalisa.
Nilipata ajali kwa kugongwa na gari tarehe 25 Octoba na kulazwa katika hospitali ya regency. Nilifanyiwa upasuaji wa mkono wa kulia na kuwekewa vyuma alhamisi tarehe 27 usiku na kuruhusiwa jumamosi tarehe 29Octoba.
Tarehe 2 Novemba nimewekewa POP ambapo nitakuwa nje ya kazi kwa muda wa mwezi mmoja. Kwakuwa natumia mkono wa kushoto itakua ngumu kuonekana mtandaoni lakini nitajitahidi japo mara moja moja.
Shukhrani ziwaendee Cantalisa kwa kuwahabarisha wana JF na kufuatilia kwa karibu matibabu yangu pale hospitali. Pia Mwita Maranya kwakuja kunitembelea na wengine wote waliotoa pole zao na kuniombea nipone haraka kupitia mtandaoni. Sina chakuwalipa ila Mungu mwenyezi atawalipa.
Ahsanteni Sana
Mtambuzi
 
Mkuu tunakuombea sana na Mungu atangulie uweze kupona
Tunaamini kwa rehema zake utapona na kuendelea na majukumu yako ya kawaida
Pole sana mkuu
 
mungu ni mwema nipo safarini mtambuzi ila nikirudi nitakuja kukuona nafurai kuskia unaendelea vema
 
Twakuombea kwa mola upone haraka_ili tujumuike wote mkuu.
 
Tunazidi Kukuombea Upone na urudie ktk hali yako ya uzima kama zamani.
 
Cantalisia will keep updating us on how u are progressing if we wont manage to come personally. Get well soon and forgive some of us for not visiting u sooner.
 
Pole Mtambuzi kwa ajali iliyokupata...Ugua pole
 
Pole sana mkuu Mtambuzi kwa yaliyokukuta, ni mipango ya Mungu. nakutakia nafuu ya haraka.,,,,,,,, niwasiliane na wife hapa tuje kukuona aisee..Get well soon
 
Hivi "The finest" anaendeleaje? Tunaomba mwenye habari atujuze, nisamehe mtambuzi kwa kuchakachua thread yako.
 
Back
Top Bottom