Shukrani zangu kwako Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shukrani zangu kwako Mh Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndusty, Oct 8, 2012.

 1. N

  Ndusty JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Mh Raisi nikupe pole na majukumu yako ya kila siku ya kusimamia taifa lako.kuhakikisha kwamba nchi yetu Tanzania inaendelea kuwepo kwenye ramani ya dunia.Tofauti na wananchi wengi au baadhi ya viongozi kuanza kukulaumu na kukutuhumu kwasababu ya mwelekeo wa nchi mimi binafsi kwa heshima zangu zote nakupa hongera na shukrani zangu kwa yote uliyotufanya na utakayoendelea kutufanya kwa watanzania wote mpaka utakapo maliza kipindi chako cha uongozi wa nchi.Nitakuwa mchoyo wa shukrani na heshima kwa Mwenyezi Mungu ambaye ndiye muweza ya yote kama nitashindwa kushukuru kwa chochote(kiwe kingi au kidogo) ninachofaidika nikiwa kama Mtanzania.

  Pasipo kujali wala kujiingiza kwenye mambo ya ushabiki wa kisiasa mimi pekee kwa niaba ya familia yangu nitapenda kukushukuru kwa kutusaidia watanzania kwenye mambo yafuatayo;

  Kwamba nchi yetu imeendelea kuwa na amani mpaka leo.sijawahi kukosa usingizi kwa kuhofia nyumba niliyomo kuvamiwa na rebels.sijawahi kulala porini kwa kuhofia kulipuliwa au kupigwa risasi na watanzania wenzangu.sijawahi kuficha kabila langu kwa kuhofia kuuwawa au kutengwa kwa sababu ya kabila langu.sijawahi kubaguliwa kwasababu ya dini yangu.

  Nikiwa kama mjasiriamali sijawahi kunyimwa visa ya kusafiri kwenda nchi yoyote nitakayo kwasababu ya utanzania wangu.Nikiwa nchi za nje utanzania wangu umekuwa ni sifa nzuri na mfano wa kuigwa kwa wananchi wengine wanaotoka nchi nyingine za Afrika.Japokuwa nchi yangu ni maskini lakini nimekuwa najivunia utanzania wangu hata mbele ya wananchi waliotoka mataifa yaliyoendelea.

  Najua kwamba yote haya yamefanikiwa kwasababu yako wewe Mh Raisi.kwamba kuna nchi nyingi duniani ambazo zina vita au zimepitia vita nchini mwao.nchi kama rwanda,burundi,ethiopia,somali,sudan,chechnyia,iraq,iran,libya na nyingine nyingi.Sababu ya hivi vita vyote kila mahali ni suala la madaraka.kila nchi inayoanzisha vita au mapigano ina sababu zake,lakini sababu zao zimekuwa zinafana kila sehemu yenye vita.Sababu yao imekuwa ni mabadiliko ya serekali.Zaidi imekuwa ni vita baina ya vikundi vya watu au vyama vya kisiasa kutaka kuongoza serekali kwa manufaa yao wenyewe kuanza kulumbana na serekali iliyoko madarakani.watu wamechukulia umaskini wa watanzania kama mtaji wa wao kupata wanachokitaka.Kutokana na ufukara wetu na uelewa wetu mdogo wananchi tumekuwa rahisi kudanganywa na kuhadaiwa na baadhi ya watu ambao wanamadhumuni ya kujinufaisha wenyewe.Kwamba wananchi wengi wamekuwa wakijiingiza au kupigania vita wasiyoijua kwasababu tu ya uelewa mdogo na umaskini wao.
  Mh Raisi imefikia hatua mpaka wananchi wanaanza kuhoji safari zako za nje ya nchi.wakihoji delegation unayokwenda nayo,wakihoji watu unaokutana nao pasipo hata kujua au kujaribu kutafakari madhumuni ya safari zako.pia pasipo kuelewa kwamba yote yanayotokea nchini yanatokea kwasababu tuna Raisi.

  Wananchi hawafikirii kwamba the reason that nchi haina vita ni kwasababu yako Mh Raisi.Umejitahidi kulinda nchi na mipaka yake, umejitahidi kutatua matatizo yote ambayo yamejitokeza( mengi ambayo sisi kama raia wa kawaida hatuyajui) baina ya nchi yetu na nchi nyingine kwa hekima na upeo wa hali ya juu ambao umetukinga kuingia kwenye vita.Nakumbuka the way ulivyo address suala la ziwa nyasa.Mh Raisi ulisema Raisi wa Malawi ni dada yako na hamngeshindwana kwenye kutafuta suluhisho.Kutoka moyoni kwangu niliadmire uwezo wako wa kutatua matatizo pale yanapotokea.Japokuwa kuna baadhi ya viongozi wako,viongozi wengine kutoka upinzani,na wanachi ambao walisema Tanzania iko tayari kuingia vitani na Malawi lakini Mh Raisi hukukurupuka kutoa mtazamo wako.na kama ulivyo m-address Raisi wa Malawi as your sister na lengo lilikuwa ni kujaribu kutafuta suluhisho kwa njia ya amani pasipo umwagaji damu,nimezidi kukupa heshima zaidi kwasababu ukiwa kama kiongozi mkuu wa nchi ulitoa maamuzi kwa kujali watanzania wote.Mh Raisi matunda ya maamuzi yako tumeyaona.Hajutaingia vitani japokuwa wengine walikuwa wanapropose hivyo ili wa-gain politicaly.Kwangu mimi hayo ndio maamuzi magumu!!!

  Watanzania wengi wamekuwa wepesi wakutafuta wakumlaumu kwa failures zao kwen
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  Yote haya ni because of Kikwete
  au it is despite of Kikwete ?
   
 3. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,493
  Trophy Points: 280
  Kumbe upo eeh.
   
 4. aminiusiamini

  aminiusiamini JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,416
  Likes Received: 1,298
  Trophy Points: 280
  Kuna watu hawana kazi.
   
 5. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,493
  Trophy Points: 280
  Hongera mwenzetu. uhuru wa kuandika.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,463
  Trophy Points: 280
  i miss u
   
 7. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  katumwa kupima upepo anakulipa bei gan?
   
 8. Father of All

  Father of All JF-Expert Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 3,093
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Ndusty you have dust in your head and if you are serious and sincere you must be sick. Huyu kama si Kikwete aliyeandika haya au Riz basi ni mgonjwa anayehitaji msaada wa haraka. Anatapatapa. Kwanini asitafute anuani ya Kikwete ambaye amemgeuza Mungu akamuimbie hizo nyimbo zake za sifa?

  Kama Tanzania itakuwa na watu kama hawa laki moja basi itazidi kuzama.

  Nakushukuru kuwa Tanzania haijawahi kukumbwa hata mafuriko kwa sababu Kikwete yupo kuilinda kama alivyoilinda familia ya Daud Mwangosi hivi karibuni.
   
 9. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,046
  Likes Received: 6,493
  Trophy Points: 280
  Same to me.
   
 10. m

  mzee wandimu JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 441
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  wewe kweli ni dust! jitambue basi!
   
Loading...