Uchaguzi 2020 Shukrani za dhati kwa wote walioshiriki kusambaza taarifa za Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu tangu mwanzo hadi mwisho

Shukrani kwako pia Mkuu umejitoa sana katika kutuhabarisha tangu mwanzo wa kampeni hadi mwisho. Thank you πŸ™πŸ½ so much Sir on your efforts. We salute you Sir! God bless you and your beautiful family
πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½
Wakuu, poleni sana na Majukumu yenu ya kila siku, Naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote mliochangia kusambaza taarifa zote za uchaguzi za Chadema ikiwa ni pamoja na kusambaza kampeni kali za kiwango cha juu za Tundu Lissu Mgombea Urais wa Chadema, ambaye anatajwa kama Mgombea bora kabisa wa Urais kuwahi kutokea barani Africa tangu kuumbwa kwa Mbingu na Ardhi.

Wahenga walisema tangu awali kwamba kidole kimoja hakivunji chawa, bila mshikamano wa wadau wote nyinyi kampeni za Tundu Lissu zisingefikia mafanikio ya 96% ambayo ilifika tangu juzi, Kwa niaba ya Chadema na kwa niaba ya Lissu Mwenyewe nachukua nafasi hii bila kuwataarifu kushukuru kila mdau aliyejitolea fedha, muda, nguvu na bando lake ili kusambaza taarifa za kampeni za Lissu, ni imani yangu kwamba Mungu Mwenyezi atawalipa kwa kazi hii iliyotukuka.

Natambua mchango wa kila mmoja na nauheshimu sana, lakini Kipekee naomba kuwashukuru wafuatao kwa niaba ya wengi, JAMIIFORUMS pamoja na Moderator kwa masahihisho na miongozo, Mungu awalinde watu hawa na mabaya yote katika kipindi walichosaliwa nacho hapa duniani, Shukrani zingine ziende kwa CHADEMA Makao Makuu.

Si rahisi kushukuru watu wote kwenye andiko hili, bali shukrani zetu zimfikie kila mmoja aliyesambaza kampeni za Lissu popote alipo , mmefanya kazi ya kutukuka mno! Nina hakika Mungu atawalipa bila shaka.

Mungu ibariki JF, Mungu ibariki CHADEMA, Mungu mbariki Rais Mpya Tundu Lissu.

Shukrani kwako pia Mkuu umejitoa sana katika kutuhabarisha tangu mwanzo wa kampeni hadi mwisho. Thank you πŸ™πŸ½ so much Sir on your efforts. We salute you Sir! God bless you and your beautiful family
πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½πŸ™ŒπŸ½
amina sana mkuu
 
Yaaa moderators ni lazima muwashukuru kwa kweli, kwa maana wamejitahidi sana kusema ukweli, Mungu awabariki sana kwa kumlinda Tundu kwa hali na mali, BTW yuko wapi tundu, atakuja Dar kumalizia Kampeni kama mlivyosema hapo mwanzo ?
Amekuja na mafuriko ya watu, umemuona enhee?
 
Shukrani pia zifike kwa Molemo , bagamoyo , Mshana Jr , Akilindogosana ,BAVICHA Taifa Sky Eclat , @bawachataifa kwa msaada maalum walionipa wakati wote wa kampeni hii
Umewasahau DARMPYATV. Walifanya kazi nzuri sana japokuwa inaelekea siku za mwishoni mwishoni ninafikiri walipata vitisho kutoka kwa watawala. Na wewe ulijitahidi japokuwa mara kadhaa ulianzisha uzi na ukawa unashindwa kutoa updates. Lakini ulijitahidi na inaelekea ulikuwa na nia njema. Hongera sana
 
πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Mungu ibariki Chadema
FB_IMG_1605430308082.jpg
 
Back
Top Bottom