Shukrani ya punda ni mateke , Chadema msikatishwe tamaa

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,163
2,000
Mungu ibariki Chadema , chama ambacho kimekuwa mstari wa mbele kuwarejeshea utu wao watanzania wenzetu wanaodhalilishwa kwa tuhuma za kutunga , Chadema imetumia mpaka Wanasheria wa chama kupangua kesi wanazotungiwa baadhi ya watanzania mahakamani kisiasa, Mungu aendelee kuwapa moyo huohuo na awajalie subira kuu.

Pamoja na kujitoa kwenu lakini baada ya kufanikiwa kurudisha Utu wao uliopondwa mithili ya karanga za kuungia kisamvu , baadhi ya wahanga wamekuwa na shukrani ya punda , hiyo isiwakatishe tamaa ya kuokoa wengine .

Endeleeni kuwapigania wengine wanaoonewa bila kuchoka , maana vitabu vya kumbukumbu vitawaandika , punda ana tabia ya kurusha mateke hata kama unamtoa mwiba kwenye mguu wake mwenyewe .
 
Cognitivist

JF-Expert Member
Aug 7, 2011
1,058
2,000
Tatizo hapa ni hujuma dhidi ya upinzani, vitisho na maslahi binafsi. Ukweli ni kuwa kuna wanaccm wengi wanatamani kuondoka ccm ila tatizo ni risasi na hujuma nyinginezo. Angalia Masha ofisi yake ya uwakili ilipigwa moto after a short while akarudi ccm, wema anakesi ya kukutwa na bangi leo amerudi ccm, mkumbo, kafulila na wengine hali ni hiyo hiyo. Ukiwa mkaidi yanakukuta ya lissu au unapotezwa coco beach kama Ben wa saa sita
 
Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,942
2,000
Mungu ibariki Chadema , chama ambacho kimekuwa mstari wa mbele kuwarejeshea utu wao watanzania wenzetu wanaodhalilishwa kwa tuhuma za kutunga , Chadema imetumia mpaka Wanasheria wa chama kupangua kesi wanazotungiwa baadhi ya watanzania mahakamani kisiasa, Mungu aendelee kuwapa moyo huohuo na awajalie subira kuu.

Pamoja na kujitoa kwenu lakini baada ya kufanikiwa kurudisha Utu wao uliopondwa mithili ya karanga za kuungia kisamvu , baadhi ya wahanga wamekuwa na shukrani ya punda , hiyo isiwakatishe tamaa ya kuokoa wengine .

Endeleeni kuwapigania wengine wanaoonewa bila kuchoka , maana vitabu vya kumbukumbu vitawaandika , punda ana tabia ya kurusha mateke hata kama unamtoa mwiba kwenye mguu wake mwenyewe .
Mimi sijaona kubwa juu ya kuondokewa na huyu kada ambaye ni nane au tisa tangu alivyojiunga na chama chenu kwa hiyo huyu bado alikuwa na chama changu kwa hiyo hasira zimeisha amerudi chadema mko huru Sana. Au mmemtuma huko kwa ajili ya kututafunia mafaili kwani Siasa zetu ni moja ya comedi
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,163
2,000
Mimi sijaona kubwa juu ya kuondokewa na huyu kada ambaye ni nane au tisa tangu alivyojiunga na chama chenu kwa hiyo huyu bado alikuwa na chama changu kwa hiyo hasira zimeisha amerudi chadema mko huru Sana. Au mmemtuma huko kwa ajili ya kututafunia mafaili kwani Siasa zetu ni moja ya comedi
Asante kwa kuandika mkuu
 
Mkwaruu

JF-Expert Member
Mar 13, 2017
2,942
2,000
Wakuu uhuru mlionao ni mkubwa na hili haliko mbali kulikubali ukitaka kulijua hilo fuatilia kauli za Makada ambao wametupwa nje uongozi wakati umri wao bado inakuhusu kuwepo ktk uongozi. Kwa hiyo ndani kuko vibaya na haya yanafanyika kuwaogopesha ya kuwa hata wakienda Upinzani upinzani hakuna jipya lakini jibu ni hili fupi Mambo ni mabaya ndani 2018 up to 2019 tutashughudia mengi ambayo yalikuwa hayategemewi.
 
Sisi makamanda halisi tutahakikisha nchi hii inakombolewa kwa udi na uvumba , wanaosaka shibe ya miezi michache waendelee na njaa zao .
 
jimmyfoxxgongo

JF-Expert Member
Jan 23, 2013
5,375
2,000
Kama mwanadamu uliyekamilika lazima uwe na msimamo,

Lazima uwe na kitu unachokiamini,

Kushindwa kuwa hivyo ni sawa na kuwa maiti

Hawa watu wote wanao hama hama hawana misimamo na hawajui wanachokisimamia,

Wanachoangalia ni urahisi wa maisha yao,

Watu kama hawa ni hatari sana

Ikitokea msando kaambiwa toa tigo au tuharibu biashara zako bila shaka anaweza kugawa mzigo

Lazima tuwe na tunachokisimamia iwe kwa furaha au maumivu

Na kama mtu hawezi kufanya vile basi yampasa akae mbali na ushwishi wa kisiasa.
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
36,420

Msando anaweza kuambiwa atoe nini? Nimecheka sana kwani mfano wako waweza kuwa kweli kabisa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom