MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,757
- 48,407
Hawa majirani tunaowajua sio wa kuchekwa nao, lazima uwe makini, vyeti watafoji kariokoo na kuja navyo eti wamepimwa, au hata wapewe tu na mamlaka zao huko bila kupimwa, kwa sasa wameshajidanganya hawana corona, hivyo utakuta hata vipimo vyenyewe hawavifanyi ili wasimuaibishe rais kwa kauli zake kwamba corona imeisha kwao.
Natanguliza shukrani kwa uongozi wa Kenya kwa kukomaa kwenye hili, muhimu sana kuwa makini, leo hii Sweden ambao walikaidi na kuachia wameanza kujuta, kumbe kirusi kilikua kinawalia timinig, wameanza kupukutika kwa kasi.
Majirani zetu Tanzania walijichokea mapema na kuacha kupima kisa umaskini, wameacha kirusi kitamalaki kwao huko, kila anayeingia huko anageuza na kirusi, wenyewe wapo wapo hawajijui kichwa kiko wapi au mkia, pona yao na tushukuru sote kwamba hiki kirusi hakionekani kuua Waafrika kwa kasi, wengi tunaathirika na kupona bila hata kujua, ila ni hatari kwa kuzembea na kugoma kuchukua tahadhari, ni kama mtu unajiachia unafanya mechi na machangudoa bila condom huku ukijisifu kwamba UKIMWI utakuogopa kisa wewe ni mcha Mungu na unaomba sana, hawa kwao vilabu vya pombe wanasongamana kama kawaida, hawajafunga chochote.
Tukubali ipo siku tutakuja kufungiana na Tanzania milele, tufanye hayo mahesabu mapema, hawa huwa hawaendani na yeyote, sisi tu ndio huwa tunawavumilia na kuna kipindi tulifungiana nao mipaka kabisa, miaka ya sabini kila mtu alikaa kwake.
Tunaelewa rais wetu ni mwanadiplomasia, kila wakinuna huwa anapiga simu na kuwatekenya wanachekea hadi akili zinawarudi, ila kuna kipindi diplomasia hufika mwisho, tujiandae ipo siku tutaagana kila mtu abaki kwake milele mpaka mwisho wa dunia, hiyo talaka ipo inakuja na bora tukawa tayari nayo.
Uzuri kila kitu kutoka kwao huwa tunanunua kwa hela zetu hivyo jeuri ya kuringishia mapesa tunayo, tunaweza tukanunua kwingine.
=========
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, ameiambia Nipashe jana kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa Kenya kukiuka makubaliano ya pande hizo mbili, waliyotiliana saini Mei, mwaka huu kwa kuzuia madereva wa Tanzania, kukataa vyeti ili wawaruhusu kuingia Kenya.
“Nadhani wenzetu wana ajenda ya siri kutuhujumu kiuchumi, tumeshakubaliana dereva anapopimwa upande wa Tanzania aruhusiwe upande wa Kenya kwa cheti, sasa wamekiuka makubaliano, wakifika upande ule wanataka wawapime tena sijui wana maana ipi nashindwa kuwaelewa kabisa, tumeamua kuchukua hatua na haturudi nyuma,” alisema.
Chanzo: Nipashe