Shukrani sana wataalam na wakuu wa Kenya kwa kuendelea kuwapima Watanzania hata wakija na makaratasi eti vyeti

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
19,863
2,000
Hawa majirani tunaowajua sio wa kuchekwa nao, lazima uwe makini, vyeti watafoji kariokoo na kuja navyo eti wamepimwa, au hata wapewe tu na mamlaka zao huko bila kupimwa, kwa sasa wameshajidanganya hawana corona, hivyo utakuta hata vipimo vyenyewe hawavifanyi ili wasimuaibishe rais kwa kauli zake kwamba corona imeisha kwao.

Natanguliza shukrani kwa uongozi wa Kenya kwa kukomaa kwenye hili, muhimu sana kuwa makini, leo hii Sweden ambao walikaidi na kuachia wameanza kujuta, kumbe kirusi kilikua kinawalia timinig, wameanza kupukutika kwa kasi.

Majirani zetu Tanzania walijichokea mapema na kuacha kupima kisa umaskini, wameacha kirusi kitamalaki kwao huko, kila anayeingia huko anageuza na kirusi, wenyewe wapo wapo hawajijui kichwa kiko wapi au mkia, pona yao na tushukuru sote kwamba hiki kirusi hakionekani kuua Waafrika kwa kasi, wengi tunaathirika na kupona bila hata kujua, ila ni hatari kwa kuzembea na kugoma kuchukua tahadhari, ni kama mtu unajiachia unafanya mechi na machangudoa bila condom huku ukijisifu kwamba UKIMWI utakuogopa kisa wewe ni mcha Mungu na unaomba sana, hawa kwao vilabu vya pombe wanasongamana kama kawaida, hawajafunga chochote.

Tukubali ipo siku tutakuja kufungiana na Tanzania milele, tufanye hayo mahesabu mapema, hawa huwa hawaendani na yeyote, sisi tu ndio huwa tunawavumilia na kuna kipindi tulifungiana nao mipaka kabisa, miaka ya sabini kila mtu alikaa kwake.

Tunaelewa rais wetu ni mwanadiplomasia, kila wakinuna huwa anapiga simu na kuwatekenya wanachekea hadi akili zinawarudi, ila kuna kipindi diplomasia hufika mwisho, tujiandae ipo siku tutaagana kila mtu abaki kwake milele mpaka mwisho wa dunia, hiyo talaka ipo inakuja na bora tukawa tayari nayo.

Uzuri kila kitu kutoka kwao huwa tunanunua kwa hela zetu hivyo jeuri ya kuringishia mapesa tunayo, tunaweza tukanunua kwingine.

=========

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frank Mwaisumbe, ameiambia Nipashe jana kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya upande wa Kenya kukiuka makubaliano ya pande hizo mbili, waliyotiliana saini Mei, mwaka huu kwa kuzuia madereva wa Tanzania, kukataa vyeti ili wawaruhusu kuingia Kenya.

“Nadhani wenzetu wana ajenda ya siri kutuhujumu kiuchumi, tumeshakubaliana dereva anapopimwa upande wa Tanzania aruhusiwe upande wa Kenya kwa cheti, sasa wamekiuka makubaliano, wakifika upande ule wanataka wawapime tena sijui wana maana ipi nashindwa kuwaelewa kabisa, tumeamua kuchukua hatua na haturudi nyuma,” alisema.

Chanzo: Nipashe
 

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
13,824
2,000
Hehe nilijua tu utakuja uanzishe uzi!!! Ila nyie majamaa kumbe mnaitegemea Tz kihivyo! Si mngetangaza tu mmefunga kila mtu abaki kwao.Mnapiga simu tulegeze halafu mnaendeleza uhuni wenu mnaowafanyia majirani wachovu!! Sasa tutaona!!
 

goodluck5

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
4,328
2,000
Ukweli ni kwamba korona imepungua(ushahidi wa kimazingira) sana TZ, pamoja na hayo mbona takwimu mamlaka haitaki kutoa, shida iko wapi?
Tunaonekana tunafanya mambo kienyeji(Kiswahili) sana.
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
18,803
2,000
Stori ndefu za nini? Tumefunga mpaka kila mtu akae kwao. Tusubiri na kuona nani atakua wa kwanza tena kuomba suluhu.
 

pingli-nywee

JF-Expert Member
Sep 16, 2015
10,933
2,000
Hawa wakenya bana,,kwanini hawataki kutuamini lakini?,
Hamuaminiki tena, sio baada ya kuitangazia dunia kwamba mapapai yana Corona, wakati ni nyinyi ndio mlikuwa mnapima sampuli na mashine mbovu. Tena kwa utepetevu wenu kwenye maabara yenu kuu, ambayo haikuwa na wataalamu wa kutosha, mlichemsha hadi kwenye vitu simpo sana kama kuhifadhi sampuli. Waziri wenu mwenyewe ndiye aliyetoa ripoti ya aibu ambayo iliwaumbua vibaya sana.

Tanzania's laboratory for testing COVID-19 faulty: Minister - Xinhua
 

Bugucha

JF-Expert Member
Jan 3, 2020
498
1,000
Hamuaminiki tena, sio baada ya kuitangazia dunia kwamba mapapai yana Corona, wakati ni nyinyi ndio mlikuwa mnapima sampuli na mashine mbovu. Tena kwa utepetevu wenu kwenye maabara yenu kuu, ambayo haikuwa na wataalamu wa kutosha, mlichemsha hadi kwenye vitu simpo sana kama kuhifadhi sampuli. Waziri wenu mwenyewe ndiye aliyetoa ripoti ya aibu ambayo iliwaumbua vibaya sana.

Tanzania's laboratory for testing COVID-19 faulty: Minister - Xinhua
Lia mliavyo, tumefunga mpaka,hakuna nyangau kuingia TZ bila cheti, alaf hakuna kumpima mtz, mwisho, hakuna kumtangaza mtz hata kama akipatikana na Corona. Tumeisha wapiga pini, lazima mtii.
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
37,572
2,000
Kwanin Tanzania nayo isiwapime Wakenya ili ukweli ujulikane?
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
6,249
2,000
Ahsante sana kwa wakuu wa mikoa wote waliyofunga mpaka na Kenye Mungu awabariki sisi waTZ tunawapenda.
 

The weekend

JF-Expert Member
May 3, 2020
250
500
They have to know that they are dealing with Kenya and not Zambia or Burundi.
To be honest Kenyan's are too smart when it comes to professionalism, Tanzania ujanja ujanja mwingi hata kwenye mambo ya kitaaluma ni vizuri kuwapima tena hao madereva wanapoingia na kutoka kla upande in order for each to be in the safe side, watz tupunguzen ushabk
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom