Shukrani BBC kwa mjadala makini juu ya Gongo la Mboto.

Sharp lady

Senior Member
Feb 23, 2011
129
13
Nikiwa kama mdau mkubwa wa idhaa ya kiswahili ya BBC leo nimepata kufwatilia vizuri mjadala juu ya mabomu ya G. Mboto, mjadala ulikuwajumuisha wadau mbalimbali wakiwamo wakazi waliodhurika, waziri wa makazi, mbg Selelii, mwakilishi kutoka Kenya na mmoja wa viongozi wa jeshi. Yameongelewa mengi ila asilimia kubwa ya makosa yako upande wa jeshi. Ushauri wangu haya mambo msiyapeleke kisiasa hatua zinazopaswa kufwatwa zichukuliwe.
 
Wanaohusika wajiuzulu na wafikishwe mahakamani kwa kusababisha vifo vya raia
 
nilimsikia mtaalam wa majeshi wa Kenya analaumu milipuko ya Gmboto ni uzembe ulifanyika.
1-mabomu na vifaa vya kulipuka hua havilipukii nje ya camp army...ilitakiwa vilipukie humo humo vila kutoka nje ya kambi kwa mujibu wa utunzaji wa mabomu hayo. Ameongea mengi ya kitaalamu.
Yaani nami nimepata kuyajua mengi kuhusu sababu ya kambi hiyo kuepo hapo na mwaka ulioanzishwa hiyo kambi. Haya mambo ni kudanganyika tu ukweli hawatuelezi sijui kwanini?
Leo kidogo kaukweli kamejulikana ...natamani Chars na kesho awaite tena wachangiaji.
 
....mpk aje mtaalam wa mabomu wa Kenya ndio atuambie nini kilikuwa tatizo?na ni kweli ktwa kwa akili ya harakaharaka huwezi kuhifadhi makombora yaliyounganishwa tayari kwa matumizi,hasa ukizingatia kuwa hatuko ktk hatari yeyote ya kupigana vita....
 
Labda sasa hawa wanajeshi wa mabomu wataamka kutoka usingizini na kuyahifadhi vema.
 
Ni pale JK na makamanda wake wa jeshi walipo umbuliwa hadharani mchana peupe. Msemaji wa jeshi amewaonesha watanzania upeo duni wa kufahamu mambo walio nao makamanda wa jeshi.

Hii itakuwa fundisho kwao, hawasomi alama za nyakati, hivi unathubutu vipi kiongozi mwenye dhamana ya kulinda maisha yawatu unaongea uongo hadharani? Watanzania wa leo wako makini sana sio rahisi kudanganyika.


Pongezi sasna mtaalamu wa masuala ya usalama kutoka kenya kwani ameonesha upeo mkubwa wa masuala ya kijeshi kuliko JK na mwamnyange wake.

Sasa tumebaini kuwa kumbe JWTZ mlikuwa mnahifadhi silaha za hatari kwenye vichanja na vidungu mithili ya nafaka kule kijijini! Sasa huo kama sio uzembe ninini?

JWTZ mnajisingizia nidhamu bora katika Afrika lihali technologically you are poore!

Sio mpaka mlete wachina na wamarekani kuwapatia shule, waoneni wakenya na hata waganda ufahamu msiokuwa nao nyie wao wanao. MSIONE AIBU! Kwani mbona hatusikii milipuko ya mabomu katika nchi jir
ani?

MFICHA MARADHI KIFO HUMUUMBUA!
 
nikweli hayakutakiwa yalipuke nje ya kambi yalitakiwa yadhibitiwe ndani kwa ndani ila kwa vile wamezoea kudanganya watu kila siku tena hadharani ngoja waumbuliwe hadharani kama wanavyotudanganya open
 
Kiukweli ni kwamba ktk mjadala huo, seikali ilipata tabu sana katika kusema ukweli kuhusu milipuko hiyo ya mabomu.Hongera sana Mr Selasini kwa maswali mazuri ya kutaka kujua ukweli upo wapi.
 
Back
Top Bottom