Shujaa wa karne.

Zero One Two

JF-Expert Member
Sep 16, 2007
9,347
3,023
Heshima mbele wakubwa.

Nimesoma kwa masikitiko taarifa ya mapokezi aliyoandaliwa EL kule kwenye jimbo lake kama shujaa,sasa sijui ni shujaa wa kabila lake au shujaa wa ufisadi!!!!!!!!!!

Kitendo cha kuachia ngazi ni utambulisho tosha kuwa yametokea mapungufu katika utendaji wake mbele ya jamii ama kwa kuhusika moja kwa moja au kwa watendaji walio chini yake.

Tukichukua hasara iliyopatikana kutokana na utendaji wake ni dhahiri kuwa hastahili kupewa heshima aliyopewa labda pengine ni nidhamu ya uoga wa wadanganyika walio wengi kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

Shujaa huyu kwa mtazamo wao kama ni sahihi ,basi ni shujaa wa karne ambaye ameliwezesha taifa kulipa mamilioni ya pesa (shs 152 milioni)kwa kampuni hewa kila siku iendayo kwa Mungu kwa kipindi ambacho kingelifika miaka miwili.

Ni shujaa wa karne huku akijua kuwa kuna watanzania wengi wanashindia mlo mmoja,na fedha zao zinaingia mifukoni mwa mafisadi ambao huku akijua kuwa kampuni hilo halipo na ni kikundi cha matapeli aliendelea kulikumbatia.

Ushujaa wake umeendelea kutukuka kutokana na kushindwa kujieleza bungeni na kulalama kuwa hakutendewa haki na kudiriki hata kuitusi kamati teule iliyoteuliwa na chombo chenye mamlaka ambacho ndicho kilimthibitsha yeye kupata u PM kuwa kimesema uongo ndani ya NYUMBA.

Kwa mtazamo wangu shujaa huyu anaonyesha hakuwa tayari kuachia ngazi na huu ni mwanzo wa safari yake kuleta mpasuko ndani ya chama chake kitu ambacho alama za nyakati zinaonyesha ANGUKO la lile JOKA kuu.Wakati ukifika haya yote yatadihiri.

Mwisho tunampa MKULU aliyeko sasa,achukue hatua madhubuti kwa wale wote waliohusika na sakata hili.Kwa shujaa huyu solution ni mahakama ili aweze kuthibitish kuonewa kwake na mengineyo yatakayodhiri sheria ichukue mkondo wake.

Asalaam.
 
Walikuchunia.

Kweli hawakukutendea haki.

Ngoja nikuondolee MKOSI
 
Back
Top Bottom