Shujaa: Maj Gen Mwita Chacha Marwa "Kambale" Afariki

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,518
8,583
SHUJAA wa vita vya kagera ..maj general mwita chacha marwa amefariki dunia akiwa kwenye matibabu ...huko south afrika...kamanda huyu shupavu ndiye aliyekuwa wa kwanza kuingiza majeshi yetu entebbe..na kuukamata,baada ya mapambano makali...

amepata kuwa mkuu wa mkoa singida na mikoa mingine ,katibu wa chama,ets ,,pia kuna wakati alijiunga na CNADEMA kwa muda ..baada ya kuhisi kusahaaulika..kabla ya rais [nafikiri mkapa au mwinyi] kumuita ikulu na kumuuliza shida iliyopelekea kujiunga upinzani..baada ya hapo aliombwa ajitoe na mara moja tangu apo akarudishwa ikulu kama MSHAURI MAALUM WA RAIS...

HII ni thread ya kukumbuka legacy yake kama kamanda shupavu pamoja na vijana aliopigana nao bega kwa bega na wote wakiwemo makamanda ,maafisa na askari waliokomboa afrika ..kamamnavyojua role ya jeshi letu kivita angola,msumbiji,namibia,comoro ets...kwa waliopo na waliotangulia mbele za haki.....
 
RIP SHUJAA WETU
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi na awape nguvu wote waliofikwa na msiba huu wawe na moyo wa uvumilivu. Ni kazi ya Mungu haina makosa. Naamini watanzania wengi wanatambua mchango wake kwa taifa letu na wanampenda ila Mungu anampenda zaidi tumuombee apumzike kwa Amani.
 
Ndiyo! Tarehe 22 Januari 1979 sauti yake kakamavu ilisikika katika radio za kijeshi akitangaza "Mutukula" kuashiria kuwa hatimaye majeshi ya Idi Amin yameondolewa katika Ardhi ya Tanzania. Hiyo ilikuwa ni hatua ya kwanza ya ushindi na Mkuu wa Majeshi alipotembelea Mutukula alipewa hilo jina la "Mutukula". Meja Jenerali Marwa atakumbukwa katika historia yetu na ninaamini mashujaa wengine kama yeye ni lazima waanziwe kwani ni wao wanaotia moyo vijana na wapiganaji wengine kujitoa muhanga kwa ajili ya Taifa lao!

Attention! .. Lala Salama Shujaa wetu! Taifa lako lilipokuita uliitika na sasa mola amekuita na umetii milele!
 
Kamanda umetutoka hatutakusahau kamwe! ulijitolea maisha yako kutulinda na kupigania nchi yetu kipenzi na sisi tunasema asante na Mungu akuweke mahali pema peponi

Serikali nayo iache mtindo wake wa kuwasahau hawa makamanda wetu ambao walipigana kule Uganda na katika ukombozi kusini mwa Afrika.

-Wembe
 
Ndiyo! Tarehe 22 Januari 1979 sauti yake kakamavu ilisikika katika radio za kijeshi akitangaza "Mutukula" kuashiria kuwa hatimaye majeshi ya Idi Amin yameondolewa katika Ardhi ya Tanzania. Hiyo ilikuwa ni hatua ya kwanza ya ushindi na Mkuu wa Majeshi alipotembelea Mutukula alipewa hilo jina la "Mutukula". Meja Jenerali Marwa atakumbukwa katika historia yetu na ninaamini mashujaa wengine kama yeye ni lazima waanziwe kwani ni wao wanaotia moyo vijana na wapiganaji wengine kujitoa muhanga kwa ajili ya Taifa lao!

Attention! .. Lala Salama Shujaa wetu! Taifa lako lilipokuita uliitika na sasa mola amekuita na umetii milele!

RIP kambale

mwanakiji una info za kutosha..una Library?
 
Poleni wana familia na jamaa, poleni TPDF, pole kwa waTanzania wote kumpoteza shujaa wetu.....

RIP
 
Kwa mara ya mwisho nilionana na huy kamanda pale Pugu Kajiungeni sote tukiwa ni wahanga Dampo jipya lililopo Pugu kinyamwezi,maana sote tulinyanganywa ardhi yetu na kuambulia laki moja n kumi na saba elfu . Alishauri tuache serikali ibebe ardhi hiyo kwa amani.

Nenda mtumishi wa bwana,kalale mahala pema; Amen
 
RIP MARWA
Thats all what i can say for now,alikua muhimu mno kwetu,ni alama ya kuduma ya jeshi letu,ni SI UNIT ya ushujaa jeshini,
bwana,alitoa,na sasa katwaa.
 
Tusisahau vile vile askari waliopigana toka kikosi cha nyuki na wengine ambao hawakupewa hizo status kama za akina Mwita Marwa
 
GAME THEORY said:
Tusisahau vile vile askari waliopigana toka kikosi cha nyuki na wengine ambao hawakupewa hizo status kama za akina Mwita Marwa

GAME THEORY,

..kamanda wa kwanza wa JWTZ kupambana na uvamizi wa Iddi Amini alikuwa Brig.Gen.Yussuf Himidi.

..Namkumbuka Brig.Gen.Ramadhani Haji Faki kama mmoja wa makamanda toka Zenj waliotunukiwa nishani na Mwalimu Nyerere uwanja wa taifa.

..kulikuwa na tuhuma kwamba Maj.Gen.Mwita Marwa alihusika na matumizi mabaya ya fedha za michango ya chama kule Singida na Kilimanjaro.

..Mchango wa Mwita Marwa ktk vita vya Kagera ulikuwa mkubwa.

..MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI MWITA MARWA.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom