Shuhudieni wanaume waliochoka na kupanda kwa gharama ya maisha !

Hawa polisi wapole sana, wangekuwa polisi wetu, hapo maji washa, mabomu na risasi zingekuwa zimeshatumika
 
Ngoja maisha yatunyooshe ipo siku na sisis tutaingai mtaani kuwangoa hawa majambazi.
 
Huyu jamaa naye amekaa madarakani. Miaka 30? Yaani mtu unazaliwa unamkuta tayari yuko madarakani unazeeka na kufa bado yupo madarakani. This is too much.
 
Hawa polisi wapole sana, wangekuwa polisi wetu, hapo maji washa, mabomu na risasi zingekuwa zimeshatumika
Tatizo la mapolisi wetu ni kuwa wamefundwa kuwatetea na kuwalinda viongozi mafisadi hata kama kwa kufanya hivyo wanajenga uadui kati yao na raia wema. Kwao amani hudumishwa kwa kuwalinda viongozi wezi hata ikibidi kuwaua raia wema ambao kosa lao ni kudai utawala wa kisheria na maisha bora. Wanachosahau ni kwamba siku umma ukiamua, hakuna risasi wala mabomu yatakayoweza kunyamazisha kilio chao. Upepo huu wa mageuzi wa mwaka 2011 utawasomba mafisadi malimbukeni wote pamoja na vyombo wanavyovitumia kuwanyanyasa wananchi.
 
Polisi wetu karibu wote ni form four failure au wamechakachua vyeti vyao. Wakiacha upolisi wataajiriwa na nani? Ndiyo maana wapo tayari kutumikia mafisadi maana hata wao waliipata hiyo ajira kifisadi.
 
Ukiona mwenzio ananyolewa, wewe tia maji..........
hakuna atakaesalimika, kama si leo kesho mafisadi wajitayarishe; watafute nchi za kukimbilia mapema!
 
tumewaa sisistiza sana Serikali ya JK, kwa hali ilivyo na ameshindwa kuzuia inflation, na huku ufisadi unakidhiri, na ajabu kwenye
kalamu na daftari viongozi wanasema UCHUMI unakua, aaaarrghh, umeona wapi uchumi unakuwa huku hali ya maisha inazidi kuwa duni?
wananchi PPP inashuka kila siku? huku ndio kutapelekea wananchi kuenda barabarani, tumepiga keleleeeeeeeee, wapi, give it 6 months
maisha yatakuwa balaa, u can focus it
 
Mkuu Mag3,

Kuna ile methali isemayo kwamba ukiona mwenzio ananyolewa…. Hawa mafisadi wa CCM wanafanya mchezo wanashindwa kabisa kusoma alama za nyakati. Ngoja walipe hayo malipo ya kifisadi kwa DOWANS ndiyo wataona kilimchonyoa kanga manyoya. Wanalazimisha kulipa mabilioni ya walipa kodi kwa kampuni haramu ya DOWANS, wale RITES nao wameingia nchini bila hata senti tano katika mkataba wao wa kuiendesha TRC. Wakatumia assets za TRC kujipatia mkopo wa $400m ambao haujuilikani umetumika vipi maana tangu waingie wao huduma za TRC zilizidi kudorora pamoja na kupata mkopo huo wa $400m. Sasa wanakaribia kupatiwa kitita cha $87m halafu wale wapumbavu ndani ya serikali wanajisifu kwamba wamefanya savings kubwa sana maana malipo yangekuwa karibu maradufu ya hiyo $87m. Hapa unabaki mdomo wazi na kuwashangaa hao wapumbavu ndani ya Serikali kwa kuruhusu malipo makubwa kiasi hicho kwa watu ambao waliingia nchini bila senti tano, wakajipatia mkopo mkubwa hakuna aliyefuatilia mkopo huo wa $400m ulitumika vipi, walishindwa kabisa kuiendesha TRC sasa wanaondoka na kitita hicho cha mabilioni.
 
Ukiona mwenzio ananyolewa, wewe tia maji..........
hakuna atakaesalimika, kama si leo kesho mafisadi wajitayarishe; watafute nchi za kukimbilia mapema!

Mkuu Mag3,

Kuna ile methali isemayo kwamba ukiona mwenzio ananyolewa…. Hawa mafisadi wa CCM wanafanya mchezo wanashindwa kabisa kusoma alama za nyakati. Ngoja walipe hayo malipo ya kifisadi kwa DOWANS ndiyo wataona kilimchonyoa kanga manyoya. Wanalazimisha kulipa mabilioni ya walipa kodi kwa kampuni haramu ya DOWANS, wale RITES nao wameingia nchini bila hata senti tano katika mkataba wao wa kuiendesha TRC. Wakatumia assets za TRC kujipatia mkopo wa $400m ambao haujuilikani umetumika vipi maana tangu waingie wao huduma za TRC zilizidi kudorora pamoja na kupata mkopo huo wa $400m. Sasa wanakaribia kupatiwa kitita cha $87m halafu wale wapumbavu ndani ya serikali wanajisifu kwamba wamefanya savings kubwa sana maana malipo yangekuwa karibu maradufu ya hiyo $87m. Hapa unabaki mdomo wazi na kuwashangaa hao wapumbavu ndani ya Serikali kwa kuruhusu malipo makubwa kiasi hicho kwa watu ambao waliingia nchini bila senti tano, wakajipatia mkopo mkubwa hakuna aliyefuatilia mkopo huo wa $400m ulitumika vipi, walishindwa kabisa kuiendesha TRC sasa wanaondoka na kitita hicho cha mabilioni.

Ile methali ya Ukiona mwenzio ananyolewa, wewe tia maji haina deal tena siku hizi. Methali ya kizamani mno na hatumiki tena hapa Bongo. Siku hizi ukiona mwenzio ananyolewa za kwako unaweka waves.
 
ipo siku tutawaibukia kama hivi
avatar23409_1.gif
 
Back
Top Bottom