Elections 2015 Shuhudieni CCM walivyoshangilia tishio la kupotezwa kwa Watanzania wenzao wenye mawazo tofauti, halafu eti tunashangaa ndugu zetu wapinzani kupotea!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,756
Naam, hiyo ndiyo Tanzania na hao ndio viongozi wa chama tawala wanaotaka tuwape ridhaa ya kuendelea kututawala kwa miaka mingine mitano. Cha ajabu ni kwamba wapo Watanzania wenzetu ambao wako tayari kutoa ridhaa hiyo bila hata kuhoji.

Kitu kimoja kilicho wazi ni kwamba tukifanya makosa tena, safari hii tutalia sana kwani kama alivyowahi kuonya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (RIP), aliyeonja nyama ya mtu haachi.
 
Binafsi sijaelewa, na huwa nauliza watu wangu mara kwa mara, hivi huyu mtu huwa anamtaja mungu yupi anaedai kumtanguliza, yaani umtangulize Mungu kwenye kupanga kuwapoteza watu ?, na huyu ni muuaji nasema kila siku.
Sitashangaa kama baada ya tishio lake hili lililoonekana kuungwa mkono na uongozi wa juu wa CCM ndio kikosi cha wasiojulikana kikaundwa. RIP Ben Saanane, RIP Azory Gwanda, RIP Watanzania waliopotezwa katika hiyo miaka mitano.

Tarehe 28/10/2020 na bado siku mbili tu tuhakikishe tunakomesha kabisa ukatili huu tulioushuhudia. CCM na mgombea wake OUT!
 
Mtatengeneza kila aina ya video ili mpate kura za huruma
Ila Watanzania hatuna huruma na msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji, visiwani tayari amechinjwa tunasubiria bara keshokutwa tumuadhibu kwenye boksi
Je usichoelewa hapo ni nini au hujui Kiswahili? Je huyo anayetishia kuwapoteza wasiomtaka hukumsikia? Je hao wanaoshangilia huwaoni? Je hiyo video ni fake? Imetengenezwa na Chadema? Kuwa mwana CCM mbona ni laana.
 
Binafsi sijaelewa, na huwa nauliza watu wangu mara kwa mara, hivi huyu mtu huwa anamtaja mungu yupi anaedai kumtanguliza, yaani umtangulize Mungu kwenye kupanga kuwapoteza watu ?, na huyu ni muuaji nasema kila siku.
Kumwogopa Mungu ni tofauti na kumtanguliza Mungu. Mwovu anamwogopa sana Mungu na siku zote ana hofu na kuomba watu wamwombee. Sara zake pekee anajua fika Mungu hatamsikiliza.
 
Huyu mzee hawezi kabisa kudhibiti matumizi ya kinywa chake..

Binadamu yeyote akiwa na weakness ya namna hii, wakati wote ataakuwa mtu wa kuingia matatizoni..

Na huyu asingekuwa na "kinga ya madaraka ya urais", hakika maisha yake yote yangekuwa jela tu..

Maana huyu ni mhalifu tu sawa walivyo wahalifu wengine kama vile majambazi waporao mali za watu kwa kutumia silaha..!
 
Huyu ni binadamu tu kwa jina, lakini kwa roho yake, hana tofauti kabisa na mnyama!

Watanzania tutafanya makosa makubwa mno kumrejesha kwenye madaraka, kwa kuwa matokeo yake tutasaga meno na kulia sana katika kipindi chote cha utawala wake!
 
Huyu mzee hawezi kabisa kudhibiti matumizi ya kinywa chake..
Binadamu yeyote akiwa na weakness ya namna hii, wakati wote ataakuwa mtu wa kuingia matatizoni..
Na huyu asingekuwa na "kinga ya madaraka ya urais", hakika maisha yake yote yangekuwa jela tu..
Maana huyu ni mhalifu tu sawa walivyo wahalifu wengine kama vile majambazi waporao mali za watu kwa kutumia silaha..!
Kinachoogofya zaidi ni huyu mtu kupewa miaka mingine mitano licha ya kwamba hapendwi kabisa. Waoga, wanafiki na walafi wameamua kuvitumia vyombo vya dola kumsukumizia miaka mingine mitano, je tutapona? Hilo ndilo swali ambalo kila Mtanzania itabidi ajiulize.

Mh. Tundu Antiphas Lissu hakuogopa kukabiliana naye face to face na akamiminiwa risasi za kumwangusha tembo lakini Mungu akakataa na hakuanguka, aliendelea kusimama! Na sasa karudi kuendeleza mapambano na safari hii, nadhani hata Jeshi Letu tukufu litatumika.

Wacha Mungu yatubidi tusali sana, shetani atatumia silaha zote lakini Mh. Lissu keshatukumbusha giza si kitu mbele ya mwanga. Lazima tuwe jasiri, historia haitatusahau, itatukumbuka.
 
Back
Top Bottom