Shuhuda: Gaidi alishuka kwenye gari akiwa na bastola na kuanza kuwapiga risasi polisi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,853
141,783
Nimeangalia taarifa ya habari Star tv na kuona mwandishi wao akimuhoji kijana mmoja aliyeshuhudia tukio mwanzo mwisho.

Kijana anadai gaidi Hamza alishushwa na gari fulami ( sijasikia vizuri kama ni ST au IST) na kuanza kuwashambulia polisi kwa bastola huku akitamba kila kona na kuonekana ni mzoefu.

Hii taarifa ya habari ya kituo cha Diallo ndio imenichanganya zaidi lakini hata Wasafi wamemuhoji huyo kijana na stori ni hiyo hiyo.

Kilichonishangaza ni taarifa ya dada mwingine aliyedai gaidi akitokea baharini na aliwasalimia kisha ndio akawaelekea polisi na kuanza kupiga risasi.

Anyway uchunguzi wa polisi utatupatia ukweli.
 
Nadhani uchunguzi hapa uanzie hapo kwenye umiliki wa hiyo Pistol,uraia wake na maisha yake kabla ya tukio,maana mapicha tayari yako mitandaoni,hii inaonyesha kuwa ni mtu tuliekuwa tunaishi naye...
 
Hata
Nadhani uchunguzi hapa uanzie hapo kwenye umiliki wa hiyo Pistol,uraia wake na maisha yake kabla ya tukio,maana mapicha tayari yako mitandaoni,hii inaonyesha kuwa ni mtu tuliekuwa tunaishi naye...
Hata mjusi tuliishi naye mtaani kwetu akiwa na mavazi hayahaya ya kwetu.Hatuwezi kwepa hizi lawama.
 
Badoo wengine wananichanga,,
Ninahaki yakupata habari bila kujari mipaka.lakini mbn nmeskia alikuwa kada wa CCM,
 
Hivi jamani RAMADHANI NTUZWE alilipwaga na tra ama ndo wameamua kumuonyesha umwamba. Yaani nchi masikini. Yaani mtu anajiona ni halali kupewa rushwa. Yaani nchi hii.traffic hata hajapata kosa anaishia kuomba ya maji. Sasa utakuwa unawatunza wao na huku una majukumu ya familia yako
 
Kumbe na nyinyi mnafuga magaidi? Naona kwenye kampeni mlikuwa naye.
Huyo mtu ana anasababu maalumu. Hiyo yote ni dhuluma ndiyo inatufikisha hapa.
 
Hapa watuhumiwa sugu watatengeneza mashuhuda hewa.

Alisema mwendazake nchi hii kila kitu hewa. Hata huyu shuhuda akiwa hewa si ajabu:

IMG_20210826_094001_471.jpg


Dhulumati wa dhahabu watafanya yote kufunika hili kwa namna yoyote.
 
Back
Top Bottom