Shughuli za Misiba, Maziko na Maombolezo zimeanza kupoteza maadili ya asili na imani zetu, Utu na Ubinadamu katika jamii

Sijaona kosa walilolifanya. Tuna uhuru wa kuabudu na wao hivo ndivyo ibada yao ya kumkumbuka marehemu inavyowatuma.

NCHI HII SIYO DHAMBI KUWA WA TOFAUTI.
 
Huu utamaduni wa kupangia Watu namna ya kuishi ikiwa hawavunji sheria za nchi ni upumbavu mkubwa.
Wakikuambia kwamba walikuwa wakinywa na kula na marehemu Labda msimu wa Sikukuu hivyo Kwa tamaduni zao hapo wamempa heshima ya kushiriki nao kula Siku kuu utakataa?

Wewe fanya kinachokupendeza wewe achia wengine wafanye yao, bia zao, chakula chao,marehemu wao, wewe Unawashwa washwa nini.
Ndio maana hii nchi haiendelea kazi kupangiana maisha..acheni watu waishi maisha yao wanayo pendezwa nayo..kikubwa hawavunji sheria za nchi..hayo maandili wanayoyaongelea utadhani wanayo watu wamejificha kwenye kichaka cha unafiki.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pombe ni sehemu ya kiburudisho,starehe,

Sioni Kama wamekosea.

Inategemeana na mtazamo wako na utamaduni wako.

Kuna jamii mtu akifa, pombe ndio huwa sehemu ya kituliza ubongo, tambiko nk


Jambo la muhimu;
Elewa duniani kuna Mila na desturi nyingi.
Ukiona Jambo Fulani ni Baya, basi jua Kwa wengine ni zuri.
 
Kwanza Mungu aipumzishe roho ya huyo marehemu simon kama sijakosea ,pili yawezekana huyo alikua mgonjwa na hakuna aliyekwenda kumtizama wala kujua hali yake ila baada ya kifo wameamua kufanya karamu ambayo ni haramu maana haimsaidii chochote marehemu zaidi ya ufahari kwa wafu wa baadae ,tatu Niliwahi kusema wakati fulani kwamba social media ni janga kubwa baada ya covid19 ,ila kwa sasa yaweza ikashika hata nambari moja ,simu hizi zimeleta mengi ambayo yametuingiza katika kuishi maisha ya ubatili yasiyo na uhalisia,tumezoea kifo bila kuelewa juu ya fumbo hili ,psychologically maisha binafsi ya mtu ni usiri ila kwa sasa ukitaka kumjua mtu mtafute katika social media utamjua A-Z maana kiuhalisia binadamu anasahau ila technology haiwezi kusahau tuwe makini turudi katika asili yetu
👍🙏
 
Hapo kuna mambo mawili.

1. Aliyekufa ni dogo ambaye picha yake ipo hapo pembeni na hajazikwa hapo nyumbani. Yeye kazikwa huko makaburini, hapo ni nyumbani.

2. Hilo kaburi ni la baba yao lipo hapo nyumbani, alizaliwa 1947 akafariki 2019 na hao ni watoto wake.

Ushauri: Tusipende kuongea sana kwa mambo yasiyotuhusu. Hao ni watu wazima wenye akili timamu, wanajifariji kwa misiba waliyopitia.
Tuwape pole ila tusiwahukumu. Hayo ni mambo yao binafsi.


Taratibu za misiba, maziko na shamba la maziko au makaburi kwa imani mila na desturi zetu zinajulikana
 
Back
Top Bottom