Shughuli za Misiba, Maziko na Maombolezo zimeanza kupoteza maadili ya asili na imani zetu, Utu na Ubinadamu katika jamii

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
19,760
35,205
Ninavyojua mimi kwenye misiba huwa kuna utani kati ya watani ambayo inasaidia kupunguza uchungu na kubadili hali ya hewa kwa muda kwa kuwaondoa wafiwa kwenye tension ya msiba walau kwa dakika chache, bila kumvunjia marehemu heshma au kuleta taharuki

Lakini leo nimekutana na hii clip nikabaki na mshangao. Nimejiuliza kweli hii ndio style ya ku celebrate maisha ya aliyetangulia?

Huyu marehemu yawezekana akawa mzazi wa mtu, mtoto wa mtu, mume au mke wa mtu. Hivi watu wake wa karibu wanalichukuliaje?

Wengi wetu tuna imani zetu zinazotufundisha heshma na tararibu za kumhifadhi marehemu, maiti, taratibu za maziko, utunzwaji wa makaburi na mambo mengine yahusuyo.

Kwa hili lililotokea hapa sijui viongozi wa kiimani wanasemaje ila kwakweli ipo haja ya kujifunza na kuwafundisha vijana wetu mambo mengi ya kiimani na kijamii




Mimi ninachojua ni kwamba watu huyazuru makaburi kufanya kumbukumbu ya wapendwa wao wakiwa na imani kwamba wanawapenda na wanawatendea wema kwa kuheshimisha hata pale walipohifadhiwa

Uislam​

Niliwahi kuambiwa na babu yangu kwamba Kwenye uislam tunayazuru makaburi ili yatukumbushe akhera kwamba ipo siku tutalala

Ukristo​

Hesabu 19 16
Mtu yeyote akigusa mwili wa mtu aliyeuawa au aliyekufa kifo cha kawaida nje ya nyumba, au akigusa mfupa wa mtu au kaburi, atakuwa najisi kwa siku saba.

Sijui hiki kilichofanyika hapa ni matokeo ya ushamba, ujinga, ukafiri au ni nini. Huyu marehemu sijui ni wa jamii gani
 
Kabila gani hawa

Screenshot_20210811-193345~2.png
 
Let people live.....

Maisha yamekua magumu

Tukiweka makatazo kila kona nchi inakua haina ladha

Mara huku unaskia madada poa waamezuiwa
Mara baa mwisho sa sita
Mara wanawake wasivae nguo fup

Makatazo meng yasiyo na msing

Yabak makatazo yenye msing tu

Kama marufuk ya ushoga
Na imoralities nyingne

Mengne yaachwe ..watu wanamaisha magum sana.
 
Watanzania bhna..yani wanataka tuishi kwa kufanana kama mapacha..mtu akitenda tofauti anaonekana wa ajabu..kila mtu aishi maisha yake..mnaua uwezo wa kufikiri tofauti.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hivi vifungu manavitumia sana kujitetea mtatafuta kokote viliko hata agano la kale..ila likija suala la kula kitimoto na bia..agano la kale mnalikataa na kuliona halifai..bure wa hedi ninyi.
 
Let people live.....

Maisha yamekua magumu

Tukiweka makatazo kila kona nchi inakua haina ladha

Mara huku unaskia madada poa waamezuiwa
Mara baa mwisho sa sita
Mara wanawake wasivae nguo fup

Makatazo meng yasiyo na msing

Yabak makatazo yenye msing tu

Kama marufuk ya ushoga
Na imoralities nyingne

Mengne yaachwe ..watu wanamaisha magum sana.
Kwanza kabisa hakuna mtu kapiga marufuku. Tumehoji uhalali wa hicho kitendo kulingana na maadili yetu sisi wanajamii wa kitanzania.

Hivyo vitu umelist havina uhusiano na tukio hili la kustaajabisha.
 
Watanzania bhna..yani wanataka tuishi kwa kufanana kama mapacha..mtu akitenda tofauti anaonekana wa ajabu..kila mtu aishi maisha yake..mnaua uwezo wa kufikiri tofauti.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app

Uhuru bila kuvunja sheria
# za nchi yako
# imani yako
# jamii yako

Wangeondo huo msalaba wakaendelea na jambo lao
 
Back
Top Bottom