Shughuli Mbalimbali za Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, Marekani

TandaleOne

JF-Expert Member
Sep 4, 2010
1,644
709
SHUGHULI MBALIMBALI ZA RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE JIJINI WASHINGTON D.C

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete ameshirikia katika Kongamano la Kimataifa la Afya lijulikanalo kama World Health Congress lililofanyika jijini Washington D.C. tarehe 12 Machi, 2016. Katika Kongamano hilo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alikuwa ni mmoja wa Wanajopo katika mjadala unaohusu Mbinu Bora za Kukabiliana na Majanga ya Afya.

Katika mjadala huo, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alielezea uzoefu ambao Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kutafuta Namna Bora ya Kukabiliana na Majanga ilioupata katika nchi zilizoathiriwa na janga la Ugonjwa wa Ebola. Alieleza kuwa dunia iko katika hatari kubwa ya kuathiriwa na majanga ya afya kutokana na kuweko na mfumo dhaifu wa sekta ya afya katika nchi zinazoendelea. Alisisitiza umuhimu wa nchi zilizoendelea kusaidia nchi znazoendelea kuimarisha mifumo ya afya ikiwemo kujenga uwezo wa wataalam wa afya na namna ya kukabiliana na milipuko.

Aidha, ameelezea umuhimu wa kupitia upya muundo na mifumo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kuliwezesha kukabiliana na majanga kwa wakati ambako kwa sasa uwezo wake huo ni mdogo, na unategemea zaidi msaada na utayari wa nchi wanachama. Dkt. Kikwete amesisitiza pia umuhimu wa dunia kuwekeza katika utafiti na ugunduzi wa kinga dhidi ya magonjwa haswa yale yanayokabili nchi masikini. Kwa ajili hiyo, Tume ya Umoja wa Mataifa ya Kukabiliana na Majanga imeshauri kuanzishwe mfuko maalum wa fedha za kwa ajili ya kuchochea utafiti na utengenezaji wa chanjo za magonjwa hayo.

Katika hatua nyingine, Rais Mstaafu jana tarehe 13 Aprili ameshiriki Mkutano wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kushauri Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya Elimu kwa Wote Duniani inayoongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Mheshimiwa Gordon Brown. Tume hiyo inayotegemewa kuwasilisha Ripoti yake mwezi Septemba, 2016 ina lengo la kutafuta namna bora ya kuondoa tofauti iliyopo katika viwango vya elimu duniani ifikapo mwaka 2040. Azma ya Kamisheni hiyo ni kufikia usawa katika elimu ambapo ifikapo mwaka 2040, mtoto atakayesoma shule kutoka nchi yoyote alipo duniani apate elimu yenye ubora unaolingana na wenzake kote duniani. Azma hiyo inatokana na uhalisia kuwa kwa kasi iliyopo sasa, itazichukua nchi zinazoendelea miaka 65 kufikia viwango vya elimu vya sasa vya nchi zinazoendelea.

Kwa kuanzia, Kamisheni inakusudia kupendekeza mapinduzi ya kifikra yatakayowezesha watoto wote wanaosoma katika nchi zinazoendelea wafikie viwango vya ubora wa elimu wa nchi za uchumi wa kati ifikapo mwaka 2030 na wale wa nchi za uchumi wa kati wafikie viwango vya ubora wa elimu wa nchi zilizoendelea ifikapo 2030. Rais Mstaafu Kikwete aliteuliwa kuwa Kamishina wa Kamisheni hiyo kutokana na uzoefu na mchango wake katika kupanua fursa za elimu katika kipindi chake cha miaka 10 ya uongozi wake. Mkutano ujao na wa mwisho wa Kamisheni hiyo utafanyika Oslo, Norway mwezi Julai, 2016.
IMG_20160415_062817.jpg
 
Mwanadiplomasia Nguli Ulimwenguni! Mwenyezimungu amlinde na kila baya analoombewa na kupangwa na Maadui zake kwa siri na dhahiri
 
sasa hao wamarekani si wampe tu uraia akae huko huko mana anasumbuka sana kusafiri safiri bora ahamie huko moja kwa mpja
 
mtu gani asiyetulia kwao kila siku kwa watu ndio mana magu alisema kuna watu wanasafiri nje kuliko kwenda kusalimia mama zao
 
Chuki zingine za kijinga kweli kweli kama sio za kipumbavu!! Zamani mlikuwa mnakwazika tunaweza ku-justfy kwamba alikuwa anatumia kodi zenu! Leo hii anatumia gharama za watu wengine kabisa lakini bado watu wanatoa povu... aaaaaaargh!! Chuki zingine mnaweza kujikuta mnajitengenezea laana kwa Mwenyezi Mungu hivi hivi!
 
Vitu vya ajabu kweli kweli yaani wazungu hawa x2 ambao sasa hivi wanafanya risk assessment ambapo labda ikitokea mtu atamwaga sumu kwenye sources za maji yao na wakianza kupokea idadi ya watu ambao washakunywa maji wanawahi vipi kuokoa maisha ili kupunguza loss of life; hizo changamoto zinafikiriwa kwenye miji yenye watu zaidi ya millioni tano au ikitokea bomb limepigwa emergency imejipanga vipi ku minimize damages, hapo watu wanapanga kama wana enough blood bank, endapo tukio likitokea kati kati ya New York, idadi ya nurses and doctors wenye uwezo wa ku deal na mambo hayo ya kushonana, capacity ya hospitali zao ku deal na large emergency au states za jirani zinaweza fika kwa muda gani kusaidia, gharama za mambo kama hayo.

Leo kweli raisi ambaye nchi yake kipindu pindu tu ni tatizo Zanzibar mwezi huu tu tayari karibu watu 40 wamepoteza maisha kitu ambacho wao washafuta kabisa hata food poison kwenye mighahawa wamezibiti; kweli JK ndio mtu wa kuwashauri kuhusu public health lazima kuna kitu sio bure.
 
Back
Top Bottom