Shughuli imemalizika pale Qatar, Argentina ya Lionel Messi inaenda kubeba Ubingwa wa Dunia 2022

Execute

JF-Expert Member
Sep 21, 2022
3,000
7,284
Tumekuwa na wakati mzuri sana kuangalia kombe la dunia na sasa tunakaribia kufika mwisho. Kila timu imevuna ilichopanda. Argentina ndio timu bora zaidi kwenye michuano hii.

Lionel Messi anaenda kuwa kinara baada ya mchezo mkali dhidi ya Ufaransa. Atastaafu kwa heshima kama mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu.

Nafasi ya tatu nampa Croatia na pongezi za pekee kwa Morocco kuweza kufika nusu fainali. Hawa wajifunze kuepuka ubaguzi ili miaka ijayo wafike mbali zaidi.
 
Style ya Morocco haina utofauti mkubwa na Argentina. Wote wanaruhusu uwafikie langoni mwao kisha wakupoke mpira na wafanye counter attack.

Jana Ufaransa alikuwa anapigwa hata goli 5 au 6, hii ilitokana na ubutu wa umaliziaji ndani ya box kwa Morocco. Kwa namna hii, kwa defence hii ya France, kwa mids zile za Ufaransa. Sijui nisemeje.

Messi ashuke chini kusaidia viungo wa Argentina. Wale madogo wawe wanapanda juu punde Messi anapokuwa na mpira, sioni kama Ufaransa itapona. Argentina akiwa karibu na box au akiwa ndani ya Box ni hatari saaaana.

Karata pekee ambayo France anayo ni kumtengenezea mazingira mazuri Mbape. Dembele ana kasi ila hana madhara makubwa, Griezmann ni wa kawaida kwa soka la sasa, hawa wanaweza wakakabika ila Mbape ni kipengele.

Binafsi karata yangu naitupa kwa Argentina japo lolote laweza kutokea.
 
Wafaransa wagumu Sana ...hakuna mwenye uhakika Nani atakuwa bingwa...wao Argentina walikuwa wanaomba Morocco ashinde jana
Usisahau kuwa juzi wafaransa walikuwa wanaomba apite Croatia

Hii fainali haitabiriki ila nitafurahi zaidi iwapo Messi atastaafu na kombe la dunia ili siku moja nitakapokuwa nimekaa na wajukuu zangu nikiwasimulia juu ya hiki kiumbe maswali kutoka kwao nitayajibu kwa ufasaha zaidi iwapo akibeba hili kombe
 
France ni kumkaba Messi tu, kazi yao kubwa ipo hapa. Hakuna kazi nyingine kubwa kwao zaidi ya hii. Na ili ufanikishe hili walau uwe na viungo wakabaji wenye mapafu ya punda kama Ngolo Kante, Kroos n.k

Sioni namna France wanavyoweza kumzima Messi pale kati. Yule dogo Alvarez ni moto mwingine, huyu Varane aliyeanza kuflop Madrid na kwenda Man U sioni kama anaweza akamzima huyu dogo.

All in all, kioengele ni Messi. Kumshika huyu jamaa ni kufanya viungo wako wote wawe attention kwake, na hapo ni kama unabet tu sababu wanaweza wakamuweka chini ya uangalizi na bado wasimuweze.
 
France inapokuwa na mpira, inaweza ikamtazama dembele, griezmann n.k ili timu iende kushambulia au itengeneze goli.

Kwa Argentina haipo hivyo, timu haiwezi kufanya shambulizi endapo Messi hayupo kwenye zone ya kutengeneza goli.

Usifikiri ni wajinga kumtegemea sana jamaa ila wanajua kabisa ukiwa na Messi, ni sawa kuwa na viungo kama akina Modric 3 na mshambuliaji mmoja kama Aguero.

Messi ni hatari saaana.
 
Miaka ya nyuma, Anceloti akiwa Madrid kabla ya kutimuliwa na kurudi tena hivi karibuni, aliwahi kuulizwa unafanya nini ili wachezaji wamkabe Messi asilete madhara?

Anceloti akasema namna pekee ni kutomtaja Messi muwapo mazoezini au mkiwa ktk Game Plan.

Nafkiri Anceloti alimaanisha yaani timu ikienda kucheza imchukulie Messi kama mtu wa kawaida, ukitaka umchambue Messi na namna ya kumkaba, ni kuharibu mipango yako kocha na kuwatia uoga wachezaji.
 
France ni kumkaba Messi tu, kazi yao kubwa ipo hapa. Hakuna kazi nyingine kubwa kwao zaidi ya hii. Na ili ufanikishe hili walau uwe na viungo wakabaji wenye mapafu ya punda kama Ngolo Kante, Kroos n.k

Sioni namna France wanavyoweza kumzima Messi pale kati. Yule dogo Alvarez ni moto mwingine, huyu Varane aliyeanza kuflop Madrid na kwenda Man U sioni kama anaweza akamzima huyu dogo.

All in all, kioengele ni Messi. Kumshika huyu jamaa ni kufanya viungo wako wote wawe attention kwake, na hapo ni kama unabet tu sababu wanaweza wakamuweka chini ya uangalizi na bado wasimuweze.
Croatia hata wao walienda hivyo hivyo lengo kubwa lilikuwa kumzuia messi na Kocha wao akasema wanajua namna ya kumzuia messi matokeo yake wakasahau na Alvarez akaweka goli mbili na hata penalty aliyofunga messi alvarez ndye aliangushwa...

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Style ya Morocco haina utofauti mkubwa na Argentina. Wote wanaruhusu uwafikie langoni mwao kisha wakupoke mpira na wafanye counter attack.

Jana Ufaransa alikuwa anapigwa hata goli 5 au 6, hii ilitokana na ubutu wa umaliziaji ndani ya box kwa Morocco. Kwa namna hii, kwa defence hii ya France, kwa mids zile za Ufaransa. Sijui nisemeje.

Messi ashuke chini kusaidia viungo wa Argentina. Wale madogo wawe wanapanda juu punde Messi anapokuwa na mpira, sioni kama Ufaransa itapona. Argentina akiwa karibu na box au akiwa ndani ya Box ni hatari saaaana.

Karata pekee ambayo France anayo ni kumtengenezea mazingira mazuri Mbape. Dembele ana kasi ila hana madhara makubwa, Griezmann ni wa kawaida kwa soka la sasa, hawa wanaweza wakakabika ila Mbape ni kipengele.

Binafsi karata yangu naitupa kwa Argentina japo lolote laweza kutokea.
Mpira unaangalizia Livescore mjomba?
ff4fa7b14b454dc3aabcbe8c69ae64b2.jpg
 
Croatia hata wao walienda hivyo hivyo lengo kubwa lilikuwa kumzuia messi na Kocha wao akasema wanajua namna ya kumzuia messi matokeo yake wakasahau na Alvarez akaweka goli mbili na hata penalty aliyofunga messi alvarez ndye aliangushwa...

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Zile kosakosa za Morocco jana angekuwepo Alvarez na Messi walikuwa hawakuachi pale.
 
Tumekuwa na wakati mzuri sana kuangalia kombe la dunia na sasa tunakaribia kufika mwisho. Kila timu imevuna ilichopanda. Argentina ndio timu bora zaidi kwenye michuano hii.

Lionel Messi anaenda kuwa kinara baada ya mchezo mkali dhidi ya Ufaransa. Atastaafu kwa heshima kama mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mpira wa miguu.

Nafasi ya tatu nampa Croatia na pongezi za pekee kwa Morocco kuweza kufika nusu fainali. Hawa wajifunze kuepuka ubaguzi ili miaka ijayo wafike mbali zaidi.
Niko pamoja na Africans United in Europe "Les Bleus" na hakika tutawafanya hamna hao Argentina
 
Back
Top Bottom