Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
GP hapo ni sawa kabisa kuwepo na hayo mawasiliano,kwani kuna mtoto hapo amabye alikuja si kwa ridhaa yake bali wawili hawa ndio chanzo cha kinda huyo kuja katika ulimwengu huu.
sasa tukisema no communication between the two tuna mpoteza huyu wa kati yao.ila yatakiwa yawe na mipaka na ikibidi muolewaji ama muoaji aje na mwenza mpya kumjulia hali huyo kiumbe.Natumai itakua amefahamika pande zote kuwa mie nimezaa na kaka/binti fulani.
Ni mtizamo tu.
Kuna siku mume wa demu wangu wa zamani aliwahi kuniita tukutane mahali ana jambo la kujadili nami. Bahati nzuri tunafahamiana kiasi kwani wakati anamchumbia huyo demu bado nilikuwa nae, tulikuwa chuoni na mambo yangu yalikuwa hayajawa na msimamo, kwa hiyo demu aliponieleza kuna mtu kaonesha interest nimpe msimamo wangu, tukakubaliana aendelee nae. Hata hivyo hakuwa amemwambia tuna uhusiano, kwa hiyo jamaa akawa ananiita "shemeji". Tukakubaliana na yule msichana kuwa tuwe kaka na dada, na tumeendelea hivyo hadi leo. Basi hiyo siku jamaa alivyoniita (ilishapita miaka 4 na walikuwa na mtoto), kwa kuwa hatukuwa tumepanga lolote, "chale" likanicheza nikampigia "dada" simu, akanijibu hana habari kuwa mwenzie ana kikao nami, nikajua kuna mtego. Nimefika pa kukutania nikamkuta yuko peke yake, keshaagiza nyama choma na bia, tukaendelea. Akiwa ameshalamba bia nne za fastafasta (haikuwa tabia yake, nadhani alikuwa anaondoa nishai), akaanza kunihoji kipolisi, nimwambie ati mkewe nilishamlala mara ngapi?
Kama ni wewe ungemjibu nini "shemejio" huyo?
.......... Huyo naye alikuwa analo analolitafuta we uache kushughulikia mambo ya maana uanze kufukua ya kale
ningemjibu mavi ya kale hayanuki shemeji
Labda kama nawe ulikuwa bado unapigamo baada ya dadio kuolewa
To maintan contact with your ex-partner kuna madhara yake. Mara nyingi wengi walio maintain contacts wamekuwa wakirudia kufanya mapenzi na wapenzi wao wa zamani ,Ingawaje tayari wako kwenye mausiano mapya.
Kukumbushia muhimu wakuu wadau wanasema ya kale hayanuki.
Wewe ndio unavyofanya hivyo? Ndugu yangu nakushauri usipende kukumbushia ni hatari sana!