Should the sitting president handle over power during his re-election bid-(katiba mpya maoni yangu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Should the sitting president handle over power during his re-election bid-(katiba mpya maoni yangu)

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by George Maige Nhigula Jr., May 1, 2012.

 1. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #1
  May 1, 2012
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana Jamii,

  Napenda kutoa mapendekezo yangu kuhusu raisi aliyepo madarakani anapogombea kipindi chake cha pili ku kabidhi madaraka ya Uraisi either kwa Speaker wa Bunge au Jaji Mkuu na yeye kubaki mgombea wa kawaida kama wagombea wengine kwa kipindi chote cha uchaguzi.

  Ni ukweli usiopingika kuwa nchi nyingi zilizoendelea duniani hasa mataifa ya magharibi, ulaya na marekani the sitting President huendelea kuwa raisi wa nchi na mgombea wa uraisi kwa wakati huo huo lakini wenzetu wametuzidi Vitu vitatu navyo ni HONEST, CIVILIZATION AND RESPECT TO THE OFFICE OF THE PRESIDENT, Huwezi kuona raisi ambaye ni mgombea anatumia vibaya taasisi ya Uraisi kujinufaisha katika campaign yake. wenzetu huwa wanaeshima na kutenganisha taasisi ya uraisi na timu yake ya kampeni.

  Lakini kwa viongozi wetu wa ki afrika hawana kawaida ya kuheshimu taasisi ya uraisi, yeye ndo anaona ni advantage ya ku exploit ili aweze kuchaguliwa kwa kutumia taasisi ya uraisi, hivyo kuondoa minong'ono na manung'uniko kwenye chaguzi zetu, kwa kuwa sisi ni waafrika tuweke sheria mpya ya kumbana sitting president asiweze kutumia taasisi ya uraisi kujinufaisha kwenye kampeni timu yake. hivyo kama ni raisi na anahitaji kuchaguliwa kwa muhula mwingine basi kipindi chote cha kampeni lazima akabidhi madaraka na taasisi ya uraisi kwa either jaji mkuu au speaker wa bunge mpaka uchaguzi utakapomalizika na mshindi kupatikana.

  Nadhani ndugu zangu wana jamii sisi sote tumekuwa mashahidi pale chama tawala kinapo take advantage na kujichotea mifedha kutoka hazina na mashirika ya uma kwa ajili ya kufanikisha campaign zake za uchaguzi, watu wamekuwa wakipiga kelele bila mafanikio, au ikulu inapogharamikia gharama ya matangazo ya picha za mgombea wa uraisi wa ccm kwenye uchaguzi wa 2010. Hali kadhalika wafanyakazi wa umma wanapotumia rasilimali za umma kwa kupiga kampeni kwa sitting president, ama kwa kujipendekeza kwao au kwa maagizo maalumu kutoka IKULU.

  Hivyo ningependa kuwaomba wazalendo wote tuliangalie hili swala kwa imakini na tulitungie sheria kwenye katiba mpya wakati wa kutoa maoni.

  Wasalaam,
  GMN Jr. (EXECUTIVE)
   
Loading...