Should Maximo stay and enjoy the money 4 nothing? - Contract to be renewed?

mi naona mpira wetu ulichezwa na vyombo vya habari na wanasiasa,yaani vichwa vya habari siku hiyo vilikuwa vinaudhi sana,utafikiri mambaz walikuwa hawataki ushindi...ila kubwa kuliko yote ni kuwa KAMA tungeshinda basi mabo yote ya msingi na mustakabali wa nchi hii yanefunikwa kabisaaaaaaaaaaa!!!!!!!duh kumbe mungu naye anaona...
 
kp_95.jpg
 
hivi nyie hamjui kuwa soka la bongo linachezwa zaidi kwenye vyombo vy habari kuliko uwanjani???

wachezahi wanapambwa mpaka wanajiona wao ndi wao hakuna wa kuwazidi kwa nini TUSIENDELEE KUBAKWA?

Vyombo vyetu viache USIMBA NA UYANGA kwani hivi sasa watu wanaanza kulaumu kwa nini PAWASA,MACHUPA hawakuitwa timu ya taifa?

kwa hiyo kama kufungwa ndio tayari so tuanze mikakati ya kuendeleza vijana kuanzia miaka 17 ili 2010 tuwe na timu kabambe tofauti ha hawa wa sasa ambao HAWAFUNDISHIKI KWA NAMNA YOYOTE
 
Kujua kuucheza mpera sio lazima ufundishwe na kocha kutoka Brazil.Tanzania tumepoteza vipaji vingi sana vya mpira,Timu yayanga iliwahi kumleta kocha kutoka nchini Romania kwa jina Victor ambaye ndiye aliyetoa wachezaji kama vile Adolph Rishad,Mkweche ,Jaafar na wengine wengi tuu.Halfu akaletwa Tambwe Leya kutoka Zaire naye akaja kuonyesha vitu vyake .Kasumba ya wabrazil tunayo sana sisi waafrika na tunashindwa kufahamu kuwa mpira umebadilika sana duniani ,wee angalia mpaka leo ni worl cup ngapi zimepita hao tunaowaabudu wanashindwa kuchukua kombe la dunia?,kuleta kocha mbrazil sio jibu la kuujua mpira tungeweza kutumia local talents zetu na tungeweza fanikiwa,sijui kama bado mnamkumbuka kocha Marijan Shaaban huyu mtu aliwahi kutufikisha mbali sana ,enzi za akin Ramadhan Mwinda Maajabu.Kuwa na kocha kutoka Brazil hatutotufikisha popote pale,expectations zinakuwa kubwa sana na ilhali wachezaji wenyewe ni viuja watupu hata physic wachezajihawana miguu imekonda na afya zao zinaonekana dhoofu sana,ni vigumu sana kucheza mpira wakati ukiwa katika hali ya kudhoofika kama wengi wa wachezaji wetu wanavyoonekana.wewe angalia majitu kama jinsi alivyokuwa Peter Tino,Sunday Manara,Omar Zimbwe na wengine wengi,yale yalikuwa machitu yanayotazamika.Sijui ni kitu gani kimewasibu wachezaji wetu siku hizi,labda mpango wa ulevi na ngono,hebu watazameni viguu vyao utafikiria ni watoto wadogo ,huwezi kucheza mpira vizuri kama huna nguvu za miguu.Bado sijaona mchezaji wa calible za akina Tino siku hizi,sifa zimekuwa nyingi sana na ahadi zimeongezeka mpaka wachezaji wetu wakapata panic na confidence ya kushinda ikaondoka,Wenzetu wamakonde wametuletea karibu wachezaji wote waop wanaocheza mpira nje ya nchi yao,na wengi wao ni bado watoto wadogo sana na wamekuja na plan ya kutufunga,bao moja tuu mpaka mpira ukaisha tumelala.Nawashaurini mahali popote mlipo duniani kila mtu angejaribu kufanya kozi ndogo ndogo za kufundisha mpira na halafu mkirudi nyumbani mjaribu kutoa mfunzo kwa watoto wadogo,huko ndio kuukuza mpira,hebu jaribuni kuangalia watu wa Cameroon jinsi walivyoweza kuukuza mpira nchini mwao,wenzetu walihamasisha natrional talent kufundisha mpira nchini mwao na matokeo yake wameweza kupandisha kiwango cha mpira kwa kiasi kikubwa sana,tusikae na kutegemea watu kutoka nje peke yake .Tutaendelea kulala kila siku .
Peace
Maulana Willo
 
Taifa stars ilitumika kama chombo cha 'kuuzia sura'yaani kujipatia umaarufu!mbele ya Mheshimiwa JK,ndio maana walijitokeza wadhamini wengi dakika za mwisho,Safari za ulaya zilikuwa zikitangazwa waziwazi tena kwa majigambo hata wapinzani wetu mambaz walikuwa wakijua mipango ye2 au hata ile ya Brazil Senagal walikuwa wakiijua.

Abajalo-dhw

Wachzaji we2 viwango vyao vidogo sana kulinganisha na uwezo mkubwa wa Kocha.Ikumbukwe Maximo alipohojiwa kwa mar aya kwanza kabisa alisema wazi Tanzania hakuna mchezaji anafaa kwa Timu ya Taifa(kama manfuatilia uzuri).Mie sishangai,Kma Maximo anaisifu Taifa stars basi ni ktka kumridhisha bosi wake JK.

Kocha Msaidizi ni lazima angekuwa Mzalendo ili kurahisisha utendaji kama vile mawasiliao,unajua ligha ni tatizo sana bongo!Saikolojia ya wachezaji!Kuna wachezaji tz wanawake kumikumi watoto kibao+matatizo kibao na posho yenyewe elf 10 kwa siku wakiwa kambini.M2 kma huyu kwa kweli hafai kuwa mchezaji kwani posible kbsa hata anapokuwa uwanjani akawaza familia yake ataitunza vipi?

Pia ikumbukwe wachezaji karibu wote wa mambas wanacheza soka ktka moja ya ligi bora kbsa barani africa-South Africa na baadhi yao Europe.Lazima tukubali soka lao liko juu zaidi ye2.
 
3D6CBC5D5DB4945342EB77893D9B7.jpg

Steve MacClaren was sacked this morning after humiliation at the hands of Croatia yesterday at Wembly stadium.(3-2)

They will not participate at the European best football nations next year.

LEAD STORY

The Football Association is to hold an emergency board meeting after England's dismal failure to qualify for the European Championships. Millions of fans were left devastated after England's 3-2 loss to Croatia at Wembley Stadium ended hopes of the team playing in next year's tournament in Austria and Switzerland.

It is the first time England have failed to qualify for the Championships since 1984, and they join Scotland, Northern Ireland, Wales and the Republic of Ireland on the sidelines next summer after they all failed to get through their groups. England boss Steve McClaren refused to resign in the aftermath of the defeat, but he now looks certain to get the sack at the FA executive meeting.

McClaren said in an interview after the final whistle: "Ultimately I take responsibility and I accept that. "It was my job to get us qualified and I failed to do that.

"I don't want to discuss my future at the present moment. I am trying to get over that result. "We feel exactly the same (as the fans), believe you me, we know how they are feeling. You should see the dressing room, they are so disappointed to have let so many people down."

Bookmakers William Hill announced they are refusing to take bets on McClaren standing down as England coach.

Former Chelsea boss Jose Mourinho is now 5/1 favourite to succeed McClaren as England manager.
 
Vipi Wabongo yule kocha wa Brazil bado tunaye tu baada ya kushindwa kutupeleka fainali? BADO ANAENDELEA KUTAFUNA PESA YA WALIPA KODI?
 
Hahaha I knew. England never knew what's losing a match!

That's it. Now: Maximo must go au sio? Kisa: hatukwenda Ghana!
 
Hahaha I knew. England never knew what's losing a match!

That's it. Now: Maximo must go au sio? Kisa: hatukwenda Ghana!

Hapana, nadhani Maximo abaki kwa sasa, ila kwa maoni yangu ni kuwa kama baada ya kipindi kingine cha mwaka mmoja na nusu au miwili hivi, Taifa Stars hawatakuwa na ushindi wa uhakika katika mashindano mengine mbalimbali, miye naona atatakiwa aondoke mara moja.

Namtetea hivi sasa kwa vile naona hali aliyoikuta timu hiyo ilikuwa ya kufikirika tu... mengi yalikuwa ya kubadili, likiwemo la nizamu kazini.

Katika sakata la huko Uingereza, kikubwa nilichokisikia hivi sasa na ni mfano wa kuigwa hapa kwetu, ni jinsi wao wanavyo fanyia kazi tukio lolote lenye utata, kuhuzunisha, kukera au kutia aibu. UTEKELEZAJI uko mbele katika yote. Tukio hili limetokea jana, kamati zimekaa moja kwa moja leo na kutoa uamuzi... i really do wish Tanzania yetu ingekuwa na ufanisi wa kiaina hii.. Statement ifuatayo ni imetolewa asubuhi hii huko kwao:
At a meeting this morning, The FA Board unanimously decided to terminate the contract of England Head Coach Steve McClaren with immediate effect.

The Board also terminated the contract of Assistant Coach Terry Venables.

The Board have agreed that there will now be a full root and branch examination of the whole England senior team set-up, which will begin with immediate effect. This will be led by Brian Barwick reporting into the Chairman, who will update the Board.

Chief Executive Brian Barwick has been given authority to identify the new Head Coach and to report back to the Board with his recommendation. There is no definitive timeframe for the recruitment of the new Coach.

FA Chairman Geoff Thompson said, "Like every England fan, we are all bitterly disappointed that we have failed to qualify for Euro 2008, and I know Steve feels that disappointment more than anyone.

"Of course we have no divine right to play in major tournaments, but it is quite right that qualification is expected.

"I would like to thank Steve for the work he has done since taking on the position last summer. His commitment to the job could not be questioned and I wish him the best for the future.

"The recruitment process for the new Coach begins now and we will do everything to get the right man for the job."
Source: THE FA.

Kikubwa kingine ni nani atapewa kazi hiyo?!

Check BBC wanavyosema... Josea Mourinho yuko kwenye list ya wanaoweza kuchukua ukocha..
McClaren sacked as England coach

Steve McClaren has been sacked as England coach following his side's failure to qualify for Euro 2008.
Assistant coach Terry Venables has also lost his job in what the Football Association said was a unanimous decision by its board.

The FA brought a swift end to McClaren's 18-month reign as England's head coach at an emergency meeting.

McClaren's position had become untenable after the 3-2 defeat to Croatia at Wembley on Wednesday.

FA chairman Geoff Thompson said: "Like every England fan, we are all bitterly disappointed that we have failed to qualify for Euro 2008, and I know Steve feels that disappointment more than anyone.

"Of course we have no divine right to play in major tournaments, but it is quite right that qualification is expected.

"I would like to thank Steve for the work he has done since taking on the position last summer. His commitment to the job could not be questioned and I wish him the best for the future.

"The recruitment process for the new coach begins now and we will do everything to get the right man for the job."

McClaren, 46, who had a four-year deal, is expected to be paid more than £2m in compensation and ex-Chelsea boss Jose Mourinho and Martin O'Neill are the bookies favourite to succeed him.

The FA has plenty of time to search for a replacement with the next scheduled fixture a friendly in France at the end of March.

FA chief executive Brian Barwick confirmed that nationality would not be an issue as he leads the search to find McClaren's successor.

Barwick also admitted that errors were made in the selection process when McClaren, who had just 18 games in charge, the shortest tenure of any England coach, was appointed in May 2006.

"The recruitment process for the new coach begins now and we will do everything to get the right man for the job," said Barwick.

"It will be done differently. We've got to learn lessons from the way we did it."

McClaren's failure to qualify for Euro 2008 cost him his job, said Barwick.

"I spoke to Steve this morning - we get on very well with him. I've had many grown-up conversations and had another one with him this morning - and I can only wish him well. But in the end, not qualifying for Euro 2008 comes up short," said Barwick.

"Qualification for a major tournament is probably a minimum requirement."

Barwick also denied he regretted giving McClaren a four-year contract.

"The contract is a private contract. I don't regret that now; I think he has tried very hard."

FA board director and Premier League chairman Sir Dave Richards defended Barwick, saying: "Brian has taken a lot of stick about him being the sole person to appoint McClaren.

"This responsibility has to be shared among us all. It's unfair to say he was Brian's man - he was the FA's man."

Barwick said he felt embarrassed and disappointed about the situation

"I'd like to apologise to the fans personally.

"I care about this passionately, it has never been just a job. I'm in it because I care about football, football fans and football teams.

"Last night was a tough, tough night. We care about this very much. I understand we have let them down and apologise for that."

Former Middlesbrough boss McClaren admitted before the Croatia match that he would "take responsibility" if England failed to reach the European Championship finals in Austria and Switzerland.

The FA took action to dismiss McClaren ahead of the 2010 World Cup qualifying draw in Durban, South Africa, on Sunday.

England's failure to reach a major tournament for the first time since the 1994 World Cup finals will cost the FA at least £5m in lost revenues.

Thompson promised the FA would conduct a "root-and-branch" review of the England team set-up, and would be led by chief executive Brian Barwick and would begin with immediate effect.

Source: BBC Sports

SteveD.
 
Vipi Wabongo yule kocha wa Brazil bado tunaye tu baada ya kushindwa kutupeleka fainali? BADO ANAENDELEA KUTAFUNA PESA YA WALIPA KODI?

Kwa haraka haraka kama hujataka kujipa muda wa kufikiri unaweza kutundika kama ulivyotundika.
Kwa wanaofuatilia masuala ya mpira wa miguu wanafahamu fika Utawala wa Soka wa England si sawasawa na wa kwetu hapa Tanzania.
Unapokuwa Manager wa timu kama ya taifa ya England huendi pale kufundisha wachezaji jinsi ya kucheza mpira, la hasha, kinachofanyika ni kukusanya wachezaji na kuwapatia mbinu mbalimbali za kuleta ushindi. Kwa hiyo kama ushindi haupatikani, guess what? mbinu zako hazikufanya kazi, kwahiyo kazi imekushinda. Sasa unaangalia mkataba wako ukoje, ujitoe mwenyewe au maslahi zaidi ukiondolewa kwa nguvu.

Juu ya Maximo wote tunaelewa amekuja hapa kufundisha wachezaji kucheza mpira. Na kwa kiwango chetu cha soka ilibidi aanzie mahali fulani, ambapo ni pale unapokuwa na wachezaji waliopo unawatengeneza kiasi fulani, ili nchi isikose uwakilishi pale panapotakiwa kuwakilishwa.
Lakini dhamana kubwa juu ya maendeleo ya soka Tanzania ipo mikononi mwa watanzania wenyewe kwenye ngazi tofauti na hasa mashuleni na katika vilabu. Kunatakiwa kuwe na mabadiliko makubwa ya kiutawala katika vilabu vya michezo hasa soka. Hali inachosha kabisa kuona vilabu vikubwa havina mipango inayoeleweka juu ya kuendeleza soka. Vilabu hivyo kwa takribani zaidi ya miaka 20 sasa vina matatizo ya uongozi havina habari kabisa ya kukuza soka, ugonjwa ambao hauonyeshi utapona lini na umedhoofisha kwa kiasi kikubwa siha ya mchezo wa mpira miguu hapa nchini.
Kwa hiyo hapa Maximo achuliwe kama chachu ya kuleta maendeleo ya soka na nadhani azidi kupewa ushirikiano wa kutosha na vyombo husika ili aweze kutekeleza program zake mbalimbali alizozieleza hapo awali.
Tunahitaji muda zaidi kuwekeza katika mpira wa vijana wenyewe umri mdogo sasa hivi ili tuweze kuwa na wachezaji au timu nzuri hapo baadae.
 
Unamtetea aendelee kula pesa ya walipa kodi kwa kazi ambayo imemshinda? Huyu kocha analipwa pesa chungu nzima ya walipa kodi kwa kazi gani kama hawezi ku-deliver? Mfano hai upo hapo UK jamaa kashindwa kwa heri.

Nakumbuka yeye aliahidi kwamba atatupeleka Ghana kwenye fainali na alisema la world cup hawezi kuahidi lakini la Ghana alitoa ahadi na alipewa pesa lukuki kwa kazi huyo, rejea safari ya Brazil na Europe. Hata mwaka 1980 wakati tulikwenda Nigeria hawakutumia pesa nyingi kiasi hicho. Kama mnataka Maximo afundishe basi apewe kazi nyingine ya kufundisha soka na sio timu ya taifa pekee kwani kwa hivi sasa anafanya shughuli gani wakati timu ya taifa haina mazoezi na mechi zake ni za musimu tu?

Tubadilike na tuanze kuonyesha kujali kile ambacho tunataka kitokee, hatuwezi kusubiri failure nyingine.

Kwa pesa anayokomba huyu tutapata makocha wengine 20 wafundishe soka kwenye grass root.
 
Ukileta Kocha mwingine yeye hatakula pesa ya walipa kodi kama Maximo? Maximo tumwache tu- aiimarishe timu taratibu- Stars wameshinda Chipolopolo- inatoa matumaini angalau kwa sasa!
 
Unamtetea aendelee kula pesa ya walipa kodi kwa kazi ambayo imemshinda? Huyu kocha analipwa pesa chungu nzima ya walipa kodi kwa kazi gani kama hawezi ku-deliver? Mfano hai upo hapo UK jamaa kashindwa kwa heri.

Nakumbuka yeye aliahidi kwamba atatupeleka Ghana kwenye fainali na alisema la world cup hawezi kuahidi lakini la Ghana alitoa ahadi na alipewa pesa lukuki kwa kazi huyo, rejea safari ya Brazil na Europe. Hata mwaka 1980 wakati tulikwenda Nigeria hawakutumia pesa nyingi kiasi hicho. Kama mnataka Maximo afundishe basi apewe kazi nyingine ya kufundisha soka na sio timu ya taifa pekee kwani kwa hivi sasa anafanya shughuli gani wakati timu ya taifa haina mazoezi na mechi zake ni za musimu tu?

Tubadilike na tuanze kuonyesha kujali kile ambacho tunataka kitokee, hatuwezi kusubiri failure nyingine.

Kwa pesa anayokomba huyu tutapata makocha wengine 20 wafundishe soka kwenye grass root.

Je, mazingira na kiwango cha soka cha wachezaji waliokuwepo mwaka 1980 na sasa kiko sawasawa?

Pili, ni kocha gani au katika mazingira yapi unakabidhiwa timu then unasema , ah hapa hatuendi Ghana, nadhani hiyo haipo.

Tatu, kama ulimsikiliza Maximo siku za mwanzo wakati anaelezea program zake, alisema kuwa tanzania itatuchukua hadi miaka 20 kuweza kufikia viwango vya juu soka duniani. hii inaeleweka hatuna ligi za wachezaji wa kiumri.

Kiwango chetu cha soka kipo chini sana Dua, tusifikiri tutakurupuka na kuwa sawasawa na England hata ndani ya miaka 20.

Mwisho, natambua na kuheshimu kuwepo kwa mawazo tofauti kutoka mtu mmoja hadi mwingine, lakini nadhani kulaumu bila ya kuonyesha njia ya kweli yenye tija ni sawa na kupoteza muda.
 
Huyu kocha alipoletwa alipewa mission ya kutupeleka Ghana hawakusema aendeleze mpira kutoka grass root. Hiyo kazi pamoja na kupewa pesa nyingi imemshinda kwa hiyo ni jukumu letu kufuta huo mkataba labda kama wanakatiana kisiri siri maana hata huo mshahara wake hao TFF hawaufahamu sasa wewe unafikiria pana usalama hapo?

Unawezaje kumthibiti kocha ambaye hata mkataba wake huufahamu? Hii issue ya malipo yake ilikuwepo hapa JF kwenye thread mojawapo nitaitafuta niiweke hapa. Makocha wengine 20+ ambao watalipwa na kiasi cha kumlipa kocha moja kwa kuendesha mafunzo kutoka grass root ndio tunahitaji sio huyu wa kungojea kuchagua wachezaji kwa musimu na kukomba pesa zote hizo.
 
We Dua,
1. Maximo akikusikia leo- hataelewa! Unga wake bwana tena JK ndo analipa from Consolidated Fund! Maximo apewe tena kama 3 years- kama Angola 2010 tusipofuzu- basi hatima yake ieleweke!

2. Kuajiri makocha wengi for under 20 hii ni wazo zuri! Itolewe pesa ingine tu- mbona kuna pesa kibao tu sinafanya kazi sisizokuwa na umuhimu mkubwa?
 
Nafurahia mchango wako, lakini naomba nisitishe kujadiliana hoja hii na wewe kwani naona hakuna tija yeyote itakayopatikana. Ukipata muda tafuta habari za mwanzoni kabisa zilizokuwa zinaeleza au Maximo alipokuwa akieleza program zake, utaelewa nini kinataka kufanyika kufufua soka la Tanzania.
Nakutakia siku njema.
 
We Dua,
1. Maximo akikusikia leo- hataelewa! Unga wake bwana tena JK ndo analipa from Consolidated Fund! Maximo apewe tena kama 3 years- kama Angola 2010 tusipofuzu- basi hatima yake ieleweke!

2. Kuajiri makocha wengi for under 20 hii ni wazo zuri! Itolewe pesa ingine tu- mbona kuna pesa kibao tu sinafanya kazi sisizokuwa na umuhimu mkubwa?

Unanichekesha sana, Max akinisikia atafahamu kwamba kumbe Tanzania sio wote vilaza. Unakumbuka miaka ya 1980's baada ya kwenda Nigeria kwenye zile fainali kuna wakati tulikuwa tunamiliki vikombe vyote vya EAC kuanzia vijana. Seniors na klabu bingwa, UMISETA ilikuwa kila mwaka na ndio walikokuwa wanatoka wachezaji wenye vipaji. Ni makosa makubwa kumlipa mshahara mkubwa mtu moja na kutegemea kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote.

Hivi unajua programme yake ya mafunzo huyu kocha? Nitaitafuta ile mada nimwombe Admin aiweke hapa.
 
Back
Top Bottom