Shoga (Abdul) aiomba serikali iwakumbuke kwenye mchakato wa katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shoga (Abdul) aiomba serikali iwakumbuke kwenye mchakato wa katiba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Saint Ivuga, Sep 20, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  Stella Aron na Mohamed Hamad


  SERIKALI imeombwa kuangalia kwa upana suala la mchakato wa uandaaji wa katiba mpya kwa kuweka kifungu kitakachowasaidia mashoga kuondokana na adha na kero ya kunyanyapaliwa.

  Ombi hilo lilitolewa jana Dar es Salaam na Bw. Abdul Zungu ambaye ni shoga na mwanaharakati katika tamasha la jinsia lililoandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

  Alisema kuwa kutokana na hali waliyonayo asilimia watu wengi katika jamii wamekuwa wakiwatenga na kuwanyanyapaa na kusababisha kuishi kwa hofu na hata kutishiwa kuuawa kwa silaha.

  Alisema pia wapo baadhi ya mashoga waliopoteza maisha kutokana na kuuawa na wanapofuatilia huwa kesi zao hazitiliwi maanani kutokana na kukosa utetezi.

  "Tuna haja ya sisi kupata mwakilishi katika ngazi za maamuzi na ndio maana tunataka katiba yenye kututambua kama sehemu ya jamii inayopaswa kulindwa na kupata huduma za kibinadamu, " alisema Abdul.

  Bw. Zungu alisema wanashangazwa na jamii kuwatenga na kuwanyima kuwapa huduma muhimu kwa tuhuma kuwa vitendo wanavyofanya havimpendezi Mungu."Tunaiomba Serikali iangalie upya kwa kuweka kifungu ambacho kitatulinda kwani kutokana na hali yetu tumekuwa tukikumbana na kero mbalimbali ikiwemo ya kutengwa na jamii, " alisema.
  Mshiriki huyo alisema kuwa licha ya umoja wao kuwa na sifa mbalimbali lakini wanapofanya maombi ya kazi katika ofisi mbalimbali wamekuwa wakinyimwa bila ya sababu.

  Alidai kuwa si kwamba hawana uwezo wa kufanya kazi yoyote ya kuwapatia maslahi bali kinachofanyika ni kukosa nafasi hizo na kujikuta hawana kazi ya kufanya na badala yake huendeleza

  ushoga ili kupata kipato cha kuwawezesha kuishi."Kama Mungu angekua hatupendi basi hata leo sisi tusingeweza kuishi hapa duniani nanyi hivyo hakuna sababu ya kututenga kuishi nanyi. Haya ni matwakwa yake," alisema.

  Kwa upande wa suala la afya alisema wamekuwa wakinyanyapaliwa hasa pale wapohitaji huduma hizo na wakati mwingine huduma hizo huzipata kwa ubabe kwa baadhi ya madaktari ama kutopata kabisa.

  Alisema ni vyema Serikali ikawatambua mahali walipo ili nao waweze kuchangia katika mapambano ya kuunda katiba mpya ambayo itajibu mahitaji yao.

  "Kama katiba haitatutambua hakuna mtu ambaye anaweza akasimama kidete kututetea na badala yake ushoga utaendelea kila kukicha huku makundi yasiyokuwa na maadili yakiibuka ndani ya jamii," alisema.

  Alisema mbali ya kundi lao ambalo linaonekana kutengwa pia kuna makundi mengi ambayo Serikali imeshindwa kuyatambua na kusema katiba nzuri ni ile inayogusa makundi yote ndani ya nchi yao.

  Naye Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), Bi. Ananilea Nkya alisema njia pekee ya kujibu matatizo ya wananchi ni kupatikana kwa katiba inayotokana na matatizo ya wananchi wenyewe hivyo hakuna sababu ya kuanza kujadili idadi ya kurasa wakati matatizo hayajainishwa.

  "Wakati mwingine utasikia viongozi wa Serikali wakikosoa jitihada za wanaharakati wakidai kuwa wanaleta mlolongo wa mambo mengi ni katiba gani tutakayoandika yenye kuingiza mambo yote hayo?, " alisema

  Hata hivyo kulikuwa na idadi kubwa ya mashoga katika tamasha hilo na kuwa kivutio kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria ambao hawajapata kuwaona 'laivu' huku wengine baadhi ya wakiangua kilio na wengine kicheko.
  habari hii kutoka gazeti za Majira
   
 2. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2011
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Vifuu tundu..
   
 3. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,148
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  Kama ndo hivyo basi, Makahaba nao pia wakumbukwe.
   
 4. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hata majambazi,makahaba,wasagaji,wafilaji, wanga etc wakumbukwe kwenye katiba mpya.
   
 5. Mr.Toyo

  Mr.Toyo JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 9, 2007
  Messages: 433
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ewe Mwenyezi Mungu, Mungu wa Abraham, Yakobo, Musa, Maria (Muumba wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo)
  Tunaomba utusamehe na utuepushe na ufedhuli huu unaotaka kuhalalishwa kwa nguvu za Jeshi la Shetani (wafuasi), Ee bwana tazama wamesha halalisha mambo kama haya huko Afrika Kusini, Uganda na sasa wanakuja Tanzania.
   
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Atakuwa ni Mwanachama wa CCM A ama CCM B huyo Abdul
   
 7. G

  Giddy Mangi JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 14, 2011
  Messages: 833
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mambo ya Jakaya vipi Mataka yupo hapo?
   
 8. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Eeh mungu tunusuru. Kiama kimekaribia.
   
 9. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,910
  Trophy Points: 280
  kweli Mungu atunusuru..ila hawa mashoga sijui wameolewa na kina nani
   
 10. M

  Mr.creative JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 504
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Jamani!
   
 11. NG'ADA

  NG'ADA Senior Member

  #11
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nahisi kuna wakubwa ambao labda nao ni wadau...wasingeruhusu kuckiliza upuuzi huu!!!
   
 12. M

  Mbwambo JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  kweli tumefikia zile siku zilizo nenwa za mwisho. Yaani ushenzi huu uliotokea ulaya na marekani wanataka uhalalishwe tanzania?. Mungu tunusuru na upuuzi huu watanzania tusikubali ushoga kwenye nchi yetu hata kwa gharama yeyote tukatae..... Mungu ibariki tanzania.....tuepushe na ushenzi huu.... Amina
  wewe kaka abduel, nenda nchi zinazokubali upumbavu huu sisi hatukubali ushenzi huu uingizwe kwenye katiba ya nchi takatifu kama tanzania
   
 13. Apollo

  Apollo JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 4,889
  Likes Received: 1,377
  Trophy Points: 280
  Ndio maana tz tunalaaniwa na majanga yanatusumbua.
   
 14. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,624
  Trophy Points: 280
  tanzania ni kama usa sasa hivi.
   
 15. moblaze

  moblaze JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  anapatikana wapi wakuu?
   
 16. NG'ADA

  NG'ADA Senior Member

  #16
  Sep 20, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jombaa unamtaka eeeh?lmaoo
   
 17. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  TGNP
  <br />
  <br />
   
 18. mdeki

  mdeki JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2011
  Joined: Mar 28, 2011
  Messages: 3,303
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  haikubaliki kabisa jamani loh!
   
 19. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  pumbav ye anasema hawana shughuli za kufanya
  mi sitakagi kuskia hayo majamaa yanayojiita mabwabwa
  akafagie barabara,auze uremboa,akaange vyepe
  hawa wanakuwaga wavivu kufanya kazi na wanachagUA KAZI
  na wengine maunga na ujinga tu unawasumbua/kuiga mambo
   
 20. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #20
  Sep 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  hali yazidi kuwa mbaya kwa mtindo huu sijui, MUNGU ndiye anayejua.
   
Loading...