Shocking truth of how I got Secret Powers as a Fake Pastor

Aqua

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
1,625
2,000
Ndugu zangu watanzania, na wale wanaompenda Mungu na wanaoamini kuna maisha baada ya kifo.Hizi ni nyakati za hatari katika dunia hii,kipindi ambacho biblia inasema kutakuwa na manabii,mitume na watumishi wa Mungu wa uongo.Biblia inawaita mbwa mwitu waliovaa ngozi ya kondoo.

Sikiliza ushuhuda wa mchungaji huyu yamkini ukaamka,nawaonea huruma kuna watu viongozi wenu wanawaambia msisikilize watu.Unapojifungia kuna mambo mawili unaweza ukawa salama au ukazuia msaada usije kwako na mwishoni ukafa.

Biblia inasema katika Mithali 14:12 "Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti"

Wengi kuna sehemu mpo na mnaona ni akili kwa macho yenu na akili zenu za kibindamu,lakini njia hiyo ikichunguzwa kwa kutumia maandiko ya Mungu inaonekana si salama.

Tanzania hatuko salama katika mambo ya imani mbwa mwitu ni wengi na wanaushirikiano sana,ukitulia kwa Mungu utawajua na hawakuanza leo kukataliwa katika mambo wanayoyahubiri na njia wanazotumia,wengine ukifuatilia video zao wenyewe watakuambia,watu hawakuwaamini walipokuwa na uwezo wa kuwaombea watu wanaanguka tu.

Hii ilikuwa miaka ya 90,leo haohao wanasupport mafuta ambayo nayo watumishi wengine wanayapinga.
Inakuwaje watumishi hawa mambo yao yanakataliwa na watumishi wengine wa Mungu?Je, kama Roho wa Mungu ni mmoja kwa nini watumishi wenye Roho mmoja wa Mungu watofautiane katika mafuta,chumvi,maji na vingine vya upako?Hapa hauhitaji kuwa msomi,maana yake kuna kundi moja hayuko sahihi.

Tazama video hii ladda Neema ya Mungu ninaweza ikakujia ukafunuliwa kutoka kwenye giza ulilomo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom