Shock: Hospitali ya Kairuki yakataa wagonjwa wa ugonjwa wa mifumo ya hewa kijanja, yaweka bei isiyowezekanika kwa Watanzania wengi

Watu wanaotetea bei hizi ghali wasiombee Nimonia ipige hodi majumbani mwao.
Watu watano, mke, wewe, watoto wako watatu wote mbavu zimewabana mnakimbilia hospitali na nyote mnanahitaji huduma mnaambiwa gharama hapa ni shilingi 850000 kwa siku kwa kila mtu na wakae wiki moja!. Kama hujaweka bondi kijumba chako unusuru familia yako sijui!. La sivyo unazika familia yako hivihivi huku ukijiona!

Think big, mnapotetea mambo kama haya kwa kisingizio cha soko huria!.

Soko huria unaweza kuileta kwenye kuuza mbege siyo afya za watu!
 
Hakuna kosa walilolifanya. Wanamwiga Waziri wa Afya. Waziri wa afya alisema kupima corona ni dola 100, yaani kama sh 250,000 hivi. Hapo unaelewa nini, zaidi ya kuwazuia watu wasipimwe corona?
 
SERIKALI ILITAKIWA MLOGANZILE ILE NUSU WAIGEZEUZE ZIFUNGWE VENTILATOR ZINAZOWEZA KUHUDUMIA HATA WATU 500 MNANUNUA UZA HII MINDEGE MI BOING HAINA FAIDA ZOZOTE
 
Hiki ulichokiandika malalamiko hayo umewaandikia wamiliki wa hospitali?

Kwanini umeilenga hospitali hiyo kuweka tuhuma nzito kiasi hicho bila ya kuwapa nafasi kujitetea ndipo uleta hapa kwa ulinganisho?

Wewe ndio mwathirika wa mfumo wa hewa au ulimsindikiza mtu anayedhaniwa kuugua?

Uzi wako umejaa amri (namtaka) kwa tuhuma zako zifanyiwa kazi pasipo uchunguzi ambao utahitaji kupata sababu za hospitali kuweka bei hiyo!!!

Uzi wako umejaa sura ya kisiasa zaidi ukilenga serikali kupitia mlango wa nyuma (umedai kuweka bei kubwa ina lengo la kuzuia upatikanaji wa takwimu halisi za wagonjwa wa mfumo wa hewa ambapo umetaja ni Korona!!!

KUMBUKA: Dunia nzima hewa yake imechafuliwa kutokana na matendo ya shughuli za kibinadamu zilizojaa hila na utukutu kuchafua ama kwa makusudi kwa lengo fulani au kwa bahati mbaya wakati wakiendelea na utafiti.

Ungana na serikali yako kutoa ushauri wenye tija na ulio huru usio na shinikizo toka ughaibuni.

Msikimbilie mtu kuwa na matatizo ya kupumua ndio Korona.

Tazama uainisho wa magonjwa gani yanaua sana binadamu kwa kipindi kirefu kila siku na usiendelee kupotoa kwa matakwa yako ya kisiasa maana wewe umekubuhu sana na mizaha ya kisiasa.
1612262180160.png
 
Acha upumbavu wewe hayawani...
Nenda Aga Khan ndio utaelewa...
Fungua hospitali yako..
Agha Khan, kuna ndugu yangu alilazwa ICU kwa tatizo la Covid 19, kuingizwa tu ICU TZS 6m. Hiyo ndiyo advance payment.

Hizi hospitali zimenunua Respiratory machines kwa gharama kubwa. Serikali walipewa mabilioni ya pesa na taasisi za kimataifa, badala ya kununua vifaatiba, wakapeleka kwenye uchaguzi na kisha kuwadanganya wajinga kuwa eti uchaguzi wa safati hii tumegharamia wenyewe.
 
Hivi Mkurugenzi wa hiyo hospitali ni nani?

Hawa watakua ni wafanyabiashara tena wasiojua maana ya kuwa taasisi inayotoa huduma ya afya. Sijawahi kuona hospitali kukataa wagonjwa kwa sababu yoyote ile.

Halafu shida ya mfumo wa upumuaji sio lazima iwe corona, inaweza kuwa hata blood pressure au tatizo lingine
Msilete siasa kwenye taaluma.

Wewe unajua gharama za mavazi tu ya kujikinga unapomhudumia mgonjwa wa corona, yanagharimu kiasi gani?

Ukiona huna hiyo, wasiliana na Jafo, ili akueleze namna ya kumfukizia mtu ambaye ni mgonjwa mahtuti.
 
Hatuwatetei Agha Khan au hospitali yoyote itakayokuja na gharama za kitalii kwa magonjwa ambayo wananchi wengi wanahitaji huduma!

Tunaiamsha serikali na mamlaka zinazohusika na tiba za wananchi zitupie jicho bei hizi utadhani tuko ulaya!

Kairuki wanatushangaza zaidi maana bei zao zimeshoot zaidi kipindi hiki cha korona kuliko ilivyokuwa awali, Je wanakusudia nini kuzipandisha hizo bei kipindi hiki?
Kwani wewe hujui kuwa ni gharama kubwa kumhudumia mgonjwa wa Covid 19 kuliko mgonjwa wa kawaida?
 
Msilete siasa kwenye taaluma.

Wewe unajua gharama za mavazi tu ya kujikinga unapomhudumia mgonjwa wa corona, yanagharimu kiasi gani?

Ukiona huna hiyo, wasiliana na Jafo, ili akueleze namna ya kumfukizia mtu ambaye ni mgonjwa mahtuti.
Siasa unaleta wewe Hamatan
Unazijua taratibu na sheria za kuendesha taasisi ya afya!? Unajua hawa watoa huduma wanafanya kazi katika miongozo gani?

Hi sio biashara ya kuuza nguo bali ni kutoa huduma na kunusuru uhai wa watu
 
Kama ni kweli hii imekaa vibaya, ila mkuu mbona tangazo halina muhuri?
Duu! Mpaka leo unataka mihuri kama mwenyekiti wa Kijiji? Kwa taarifa yako mihuri imebaki lazima kwa transaction za fedha tu kwingineko kote logo na saini vinatosha kwa taarifa.
 
Duu! Mpaka leo unataka mihuri kama mwenyekiti wa Kijiji? Kwa taarifa yako mihuri imebaki lazima kwa transaction za fedha tu kwingineko kote logo na saini vinatosha kwa taarifa.
Hapo saini umeiona wapi kwenye tangazo?
 
Ni punguani peke yake ndiye anaweza kuamini kuwa tatizo ni Hospitali ya Kairuki!Mleta mada kama unailaumu Hospitali ya Kairuki wewe ni punguani.Fikiria nje ya box utajua tatizo ni nani.Damn!,zama hizi tuna Watanzania ambao uwezo wao wa kifikiri umekuwa mdogo sana!!
 
Back
Top Bottom