Shock: Hospitali ya Kairuki yakataa wagonjwa wa ugonjwa wa mifumo ya hewa kijanja, yaweka bei isiyowezekanika kwa Watanzania wengi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,135
2,000
Katika hali inayoonekana ni muendelezo wa maisha magumu kwa wananchi.

Hospitali ya Kairuki nchini imekuja na utaratibu wa kushangaza wa kutoza malaki ya hela kwa siku kwa mtu atakayeenda katika hospitali hiyo kutibiwa ugonjwa wa mifumo ya hewa.

Katika utaratibu huo mgonjwa yeyote atakayekwenda kupata huduma ya ugonjwa wa mfumo wa hewa, Hospitali hiyo itamtoza shilingi Laki sita kwa siku (600,000)kama hatahitaji huduma ya Ventilator. Na kama atahitaji huduma ya ventilator basi atalazimika kulipa shilingi Laki nane na nusu (850,000).

Nilipokuwa naongea na wananchi kuhusiana na suala hili, wengi wameonyesha kuwa na wasiwasi kuwa hospitali hiyo inataka kuwakimbiza wananchi wenye matatizo hayo wasiende kwenye hospitali hiyo. Na kwa kuwa ni kinyume cha maadili ya kidaktari kukataa kuhudumia mgonjwa basi hospitali hiyo inataka kukwepa kuhudumia wananchi katika maradhi hayo kijanja.

Kwa kweli hili jambo ni la kusikitisha na la kutia aibu kwa wamiliki na waendesha hospitali hiyo.

Kwanza kuna maswali ya kujiuliza, kwa nini hatua hii ya ajabu ije kwenye kipindi hiki cha Korona?.

Je, ni kweli kuwa kwa utaratibu huu hospitali hiyo inafukuza wananchi wanaohitaji huduma hiyo kijanja kwa kisingizio cha pesa?

Na kama hailengi kukwepa wajibu wa kuhudumia wagonjwa, je wamiliki wa hiyo hispitali wameamua kuigeuza Korona kuwa dili, yaani kuvuna mamilioni ya pesa kupitia wananchi wanaohitaji huduma ya hospitali?

Je, kuna baraka za serikali katika hatua hii, ili kulazimisha wananchi wafanye tiba mbadala majumbani ili takwimu halisi za wenye ugonjwa wa Korona zisipatikane?

Tunaitaka serikali kupitia Waziri wa Afya aingilie kati suala hili.
Tunajua serikali inayo mamlaka ya kuingilia kati utendaji wa hospitali zote nchini katika mfumo wao wa utoaji huduma nchini.

Tunamtaka Waziri wa Afya aje public atueleze kama anaunga mkono kitendo kama hiki cha hospitali ya Kairuki ili hiki walichokifanya kisije kikageuka kuwa ni mfano wa hospitali nyingine nao kufanya kama wao.

Ubaya wa kitendo cha hospitali ya Kairuki, hawajaspecify hata ugonjwa husika, wametumia jina la jumla la "magonjwa ya mfumo wa hewa!" . Kwa hiyo watoto wetu wachanga wakipata nimonia ya kawaida kabisa isiyokuwa hata hiyo Korona ndo mnataka kuwatoza Laki nane na nusu kwa siku? - Hii hospitaki inataka tupoteze hata watoto wetu kwa sababu ya watu wenye mawazo. mfu wachache!

Tunataka hii hospitali ibadirishe huu utaratibu maramoja!. Mwanzilishi wa hii hospitali hayati profesa Kairuki atakuwa anajigeuza kaburini sasa kwa baadhi ya cowards wachache kutaka kuwatosa wananchi katika kipindi hiki kigumu cha kiafya duniani!

Hili halikubaliki:
Angalia fomu hii hapa chini kutoka hospitali hiyo.

IMG-20210202-WA0031.jpg
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,135
2,000
Ndugu unatakaje sasa, watu watibiwe bure? Hospitali za serikali zipo, watu waende huko.
Hakuna kitu kisichoratibiwa na serikali hasa huduma za afya.

Kama ulidhani kwa kuwa ni hospitali binafsi basi inaweza kupanga bei kiholelaholela utafikiri wana nchi yao binafsi wasiyobanwa na regulatory authority yoyote basi pole sana!
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
6,563
2,000
Hakuna kitu kisichoratibiwa na serikali hasa huduma za afya.
Kama ulidhani kwa kuwa ni hospitali binafsi basi inaweza kupanga bei kiholelaholela utafikiri wana nchi yao binafsi wasiyobanwa na regulatory authority yoyote basi pole sana!
Ndio maana hata watoa huduma wanashindwa, haiwezekani hospitali binafsi ipangiwe bei. Hospitali za serikali zinapokea ruzuku za kutosha na misamaha ya kodi mingi. Unataka hospitali binafsi zitoe huduma sawa na serikali?

Peleka mwanamke Aga Khan kujifungua uone bei zao. Tuache siasa, wakishindwa kulipa wafanyakazi, mtakuja hapa Jamiiforums kusema Kairuki wameshindwa kulipa wafanyakazi wao.
 

Jmc06

JF-Expert Member
May 11, 2016
1,924
2,000
Hakuna kitu kisichoratibiwa na serikali hasa huduma za afya.
Kama ulidhani kwa kuwa ni hospitali binafsi basi inaweza kupanga bei kiholelaholela utafikiri wana nchi yao binafsi wasiyobanwa na regulatory authority yoyote basi pole sana!
Unajua bei ya Aghakhan, TMJ na nyingine za Masaki ni bei gani!? By the way nyie si hamuamini tiba asili mnataka mkimbilie kwa Kairuki huku hamna ela, mnalalamika nini Sasa!?

Unatakiwa upiganie maisha yako kwa namna yoyote, Kama huna hiyo laki 6 au 8 kutoa kwa Kairuki anza kujifukiza mapema, au nenda muhimbili/mwananyamala. Kama hutaki baki JamiiForums unabwabwaja huku ukisubiri ufe tukuimbie parapanda ,tukuzike na kukuwekea R.I.P Missile of the Nation.
 

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
10,135
2,000
Ndio maana hata watoa huduma wanashindwa, haiwezekani hospitali binafsi ipangiwe bei. Hospitali za serikali zinapokea ruzuku za kutosha na misamaha ya kodi mingi. Unataka hospitali binafsi zitoe huduma sawa na serikali? Peleka mwanamke Aga Khan kujifungua uone bei zao. Tuache siasa, wakishindwa kulipa wafanyakazi, mtakuja hapa Jamiiforums kusema Kairuki wameshindwa kulipa wafanyakazi wao.
Pale unapopandisha bei mara nyingi katika kipindi fulani cha ugonjwa wa mlipuko ni dhahiri kuna question mark. Kwa nini hizi bei hazikushoot kiasi hiki miezi kadhaa nyuma wakati tatizo la korona halikuwa kubwa nchini?
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,363
2,000
Hivi Mkurugenzi wa hiyo hospitali ni nani?

Hawa watakua ni wafanyabiashara tena wasiojua maana ya kuwa taasisi inayotoa huduma ya afya. Sijawahi kuona hospitali kukataa wagonjwa kwa sababu yoyote ile.

Halafu shida ya mfumo wa upumuaji sio lazima iwe corona, inaweza kuwa hata blood pressure au tatizo lingine
 

pure man

JF-Expert Member
Mar 10, 2015
535
500
Hivi Mkurugenzi wa hiyo hospitali ni nani?

Hawa watakua ni wafanyabiashara tena wasiojua maana ya kuwa taasisi inayotoa huduma ya afya. Sijawahi kuona hospitali kukataa wagonjwa kwa sababu yoyote ile
Weee mama d unajua uwekezaj wa hivyo vifaa au unabwabwaja tu kmbwa alikuwa kwenye heat,nenda aghakan wanalipa zaid ya 1m.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom