Shivji na wenzake wampigia mbuzi gitaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shivji na wenzake wampigia mbuzi gitaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jan 16, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi kweli Shivji na wenzake wanaamini kabisa kwamba Mkwere atakubali kitu wanachopendekeza – cha Katiba kupatikana kwa njia ya midahalo nk? Na kwa nini hawajaweka time-frame – kwamba kabla ya Mkwere kumaliza kipindi chake Katiba mpya iwepo tayari?

  Nashangaa sana kuona wasomi hao waliobobea hawaoioni hali halisi. Mkwere aliingizwa na mafisadi kwa ‘makubaliano' maalum, kwamba baada ya yeye kumaliza kipindi chake afanye kila liwezekanalo aingie yule fisadi mwingine. Kipindi chake hiki cha pili, kama tulivyoona katika kampeni za mapesa mengi, na uchakuachuaji wa kura, kilipatikana kwa nguvu hizo za pesa. Vinginevyo……

  Sasa vipi tena sasa aridhie Katiba mpya ambayo kwa asilimia 100 itaiondoa CCM madarakani? Watamwambia, "Ndugu yetu, vipi tena unakwenda kinyume cha makubaliano? Kwa kuwa wewe umeshaula miaka 10 kwa nguvu na mapesa yetu, sasa unataka kufanya umafia ya kututosa?"

  Mkwere ataendana na geresha tu (going through the motion" ya kuridhia Katiba lakini hatakubali iwepo hadi mafisadi wenzake nae waingie Ikulu. Hapo hafurukuti.

  Hawa jamaa walivyokuwa wahovyo wako hata tayari nchi iingie kwenye ghasia kubwa kama vile Kenya ili Katiba Mpya ipatikane.
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe. Njia ni moja tu nayo ni peoples power
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Akina Shivji wanalijua hilo -- kwamba bila hiyo people's power nchi hii haiwezi kupata katiba mpya. Lakini wasomi hao hawataki kuonekana wao ni wachochezi wa vurugu.

  Ikipatikana Katiba mpya kwa njia kama ya Kenya Shivji na wenzake watakuwa wa kwanza kusapoti.
   
 4. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  When the woman is fed up there is nothing you can do about it.
  Tanzanians are fed up SO WE MUST GET WHERE WE WANT TO BE.
   
 5. i

  ibange JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  kama ulisikiliza vizuri wasomi waliishauri serikali ikubali mchakato wa katiba mapema kabla watu hawajadai kwa nguvu na kumwaga damu
   
 6. k

  kingtuma Member

  #6
  Jan 16, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakika we unaona mbali na kwa hali ilivyo ya viongozi uchwara kubaka mada na kuziteka wananchi tunatakiwa kuchukua hatua za haraka " Ni lazima nchi nzima tugome na kuandamana mpaka ikulu"
   
 7. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Tatizo lako ni kwamba huelewi kuwa ule ulikuwa ni mjadala wa kwanza kuzungumzia katiba toka JMK kutangaza kuunda tume ya katiba. Mjadala maana yake ni kujadiliana na kila mmoja anatowa mada kutokana na muono wake, ilikuwa si kumwambia Kikwete fanya hivi au vile, ilikuwa simply sisi tunaona iwe hivi, kila mmoja kwa mtazamo wake. Zikifanyiwa kazi zote na za mijadala mingine na makongamano na, na, na hapo ndipo tunapoweza kuja kupata kusema Mheshimiwa Rais, sisi tunataka hiyo tume iwe hivi na ifanye kazi hizi, na muda uwe huu. Huwezi kuyapata yote hayo katika mjadala wa Mwanzo.
   
Loading...