Nimekuwa najiuliza maswali mengi kuhusu hizi nchi zetu za Kiafrika nakosa majibu,hivi inakuwaje tunashabikia maendeleo ya nchi za magharibi na kudharau kabisa nchi zetu,mfano mzuri ni kwenye soka,yaani hivi sasa kila kona ya nchi za Afrika ili uonekane unakwenda na muda (wa kisasa) basi zungumzia ligi ya Uingereza na uwe mpenzi wa moja ya timu hizo na ukiweza kutaja majina ya wachezaji basi ndo utakuwa umefuzu ,kwanza utapata marafiki haraka lakini pia utaonekana wa kisasa zaidi,..Sasa swali langu ni kwamba huu si ukoloni mamboleo?Ni kwa nini tusishangilie na kuzisapoti timu zetu za nyumbani ili zifikie viwango vya juu?..Ninaomfano,nipo kwenye moja ya vyuo vikuu vya hapa Afrika,siku moja hapa karibuni wakati wa fainali za kombe la mataifa huru ya Afrika,siku ambayo Misri walicheza na Ghana ,siku hiyohiyo Manchester walikuwa wanacheza sikumbuki na timu gani huko ulaya,kilichonishangaza na kujiuliza uwezo wa Waafrika kufikiri kuhusu mustakabali wao wa maendeleo hasa ya soka ni pale nilipoenda common room kuangalia fainali ya Misri na Ghana,nikakuta wanafunzi wenzangu wanaangalia mpira wa Manchester,kusema ukweli sikuelewa,ilibidi niwaulize kulikoni,baada ya debate ya muda wakasema tutakuwa tunaangalia kila mechi dakika kumi kwa zamu,ukweli mpaka leo haijaniingia akilini,ni lini Afrika tutakuwa Proud kwa mambo yetu,...hivi Nyerere,Nkurumah,Mao,Karl Marx na wenzake wangekuwepo wangekuwa mashabiki wa timu zipi?..Hivi Pro.Shivji,Pandre Privatus Karugendo,Pro.Baregu,Mzee Mwanakijiji na wenzake wanashabikia timu gani za Ulaya...waungwana nisaidieni kama haya ninayoyasema ni mtizamo hasi wa mambo naomba mnirekebishe na kunielimisha.
Nawakilisha.
Nawakilisha.