Shivji,mzee mwanakijiji na padre karugendo wanashabikia timu gani za ulaya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shivji,mzee mwanakijiji na padre karugendo wanashabikia timu gani za ulaya?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donrich, Feb 17, 2010.

 1. D

  Donrich Senior Member

  #1
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nimekuwa najiuliza maswali mengi kuhusu hizi nchi zetu za Kiafrika nakosa majibu,hivi inakuwaje tunashabikia maendeleo ya nchi za magharibi na kudharau kabisa nchi zetu,mfano mzuri ni kwenye soka,yaani hivi sasa kila kona ya nchi za Afrika ili uonekane unakwenda na muda (wa kisasa) basi zungumzia ligi ya Uingereza na uwe mpenzi wa moja ya timu hizo na ukiweza kutaja majina ya wachezaji basi ndo utakuwa umefuzu ,kwanza utapata marafiki haraka lakini pia utaonekana wa kisasa zaidi,..Sasa swali langu ni kwamba huu si ukoloni mamboleo?Ni kwa nini tusishangilie na kuzisapoti timu zetu za nyumbani ili zifikie viwango vya juu?..Ninaomfano,nipo kwenye moja ya vyuo vikuu vya hapa Afrika,siku moja hapa karibuni wakati wa fainali za kombe la mataifa huru ya Afrika,siku ambayo Misri walicheza na Ghana ,siku hiyohiyo Manchester walikuwa wanacheza sikumbuki na timu gani huko ulaya,kilichonishangaza na kujiuliza uwezo wa Waafrika kufikiri kuhusu mustakabali wao wa maendeleo hasa ya soka ni pale nilipoenda common room kuangalia fainali ya Misri na Ghana,nikakuta wanafunzi wenzangu wanaangalia mpira wa Manchester,kusema ukweli sikuelewa,ilibidi niwaulize kulikoni,baada ya debate ya muda wakasema tutakuwa tunaangalia kila mechi dakika kumi kwa zamu,ukweli mpaka leo haijaniingia akilini,ni lini Afrika tutakuwa Proud kwa mambo yetu,...hivi Nyerere,Nkurumah,Mao,Karl Marx na wenzake wangekuwepo wangekuwa mashabiki wa timu zipi?..Hivi Pro.Shivji,Pandre Privatus Karugendo,Pro.Baregu,Mzee Mwanakijiji na wenzake wanashabikia timu gani za Ulaya...waungwana nisaidieni kama haya ninayoyasema ni mtizamo hasi wa mambo naomba mnirekebishe na kunielimisha.
  Nawakilisha.
   
 2. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #2
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,765
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  Entertainment na ushindani. Timu nyingi za ulaya ndiko cream ya wachezaji soka wanakocheza na kulipwa mamillioni, kutokana na matangazo kwenye TV etc etc. Afrika tuko proud sana na mambo yetu vile vile usisahau kwamba mataifa ya ulaya na marekani wanaiba sana mbinu kutoka Afrika tatizo letu ni viongozi walioko madarakani kama vile unavyowaona wale walioko kwenye Chama Cha Majambazi nk.

  Kuhusu ushabiki kwa nini usiwaulize wahusika wakwambie wanashabikia timu gani wao wenyewe? Bila kusahau Jakaya Kikwete alipowakimbia Watanzania na kwenda kuangalia kipenzi chake yaani Tottenham Hotspurs si unakumbuka.
   
 3. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Sio ushabiki ni upenzi kila mtu anapenda kile kizuri halafu kumbuka ligi ya wenzetu wanavyoitangaza duniani kote ni strategies tu. Nishabikie LIPULI?
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Feb 17, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 78,282
  Likes Received: 40,520
  Trophy Points: 280
  Watu sijui wamesomea shule gani tu. Mtu badala ya kuandika kwa aya unaandika kwa kurundika kila kitu kwenye aya moja hadi inaboa hata kusoma. Mijitu mingine kama haijaenda shule bana aaaagh
   
 5. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 6,820
  Likes Received: 1,672
  Trophy Points: 280
  My Gueses

  Professor Shivji huyu ni John Kisomo kawaida wasomi wa level hii wengi wanakua si washabiki wa mpira probably some county cricket team ili aonekane nae yupo up to date kwa wasomi wenzake.

  Padre Privatus Karugendo huyu atakuwa si mtu wa ku-impress na mzalendo kwa watu wake naamini hana timu ya nje bali Young African (Yanga)

  Professor Baregu huyu njaa na mpotoshaji Umma kwa faida yake hatakuwa Arsenal akija bongo just to fit in with the crowd hila deep own ana timu yoyote ana penda kusoma sana huyu entertainment kwake ni kusikiliza akina Mozzart and the likes au attending theatres.

  Mwanakijiji is a puzzle kwa kweli, he is a man with many talents juzi katuimbia mjomba hapa ana nakala zake the love huko kwenye jukwaa la love at the same time ndio mmoja ya watu mashuhuri hapa Jukwaa la siasa. Huyu nasema ana adapt easily kwa hivyo whatever is popular in detroit na yeye yumo. My guess will be the Pistons kwa kuwa anapenda ku-deal na what he can understnad rather than jump on a wagon.
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Feb 17, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,087
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Yani ulivyoandika mpaka macho yanauma, panga vizuri maandishi yako kama hujali ili ujumbe uufikie hadhira ipasavyo!..
   
 7. D

  Donrich Senior Member

  #7
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mkuu Julius hili swala la aya si shule naweza kusema ni negligence,ninaahidi kulirekebisha,naomba upunguze hasira..Ee bwana!
   
 8. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Bwana /Bibi Donrich walio wengi hapa watakupiga madongo kwani hii hoja inawagusa. Mimi nimekuwa najiuliza miaka mingi na kila siku sipati jawabu, nashangaa watanzania wengi tena wasomi hawajui hata bajeti yao kwa mwaka imekaaje, Juzi huko dodoma kulikuwa na miswada kibao mingine imegoma kupitishwa na waheshimiwa mingine imepita hakuna mtu ana muda wa kufuatilia hayo, ukizungumzia hali ya viwanda, kilimo, misitu, utalii nk watakuambia hayo ni siasa na wao si wapenzi wa siasa. Ukizungumzia Elimu, Afya, miundo mbinu watakuambia kamuulize JK.

  Kama watanzania tunge-invest nguvu zetu kwenye midahalo inayohusu mstakabali wa nchi yetu kama tunavyobishana kuhusiana na league ya uingereza na hispania naamini ingetuchukua muda mfupi sana kuona mabadiriko ya kweli katika njanja za kisiasa kiuchumi na hata kijamii. Lakini ndio hivyo tena huu ni wakati kama zilivyokuwa nyakati za pekosi na buga na raizon.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Feb 17, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Dunia kama kijiji! or is one big country!!

  mpira burudani bwana!

  wachezaji wanashinda kwa macheni kula nyama choma na siku mbili kabla ya game wanaenda bagamoyo kuroga! , tulivyokubali kuingia kwenye globalisation lazima tukubali na vyote, kama una uwezo na kuleta burudani utapendwa tu haijalishi uko wapi!

  I believe karibu vitu vingi unavyotumia vinatoka nje ya nchi! ila mpira unataka tushabikie wa ndani ili hali mavazi mpaka mpira wenyewe unatoka nje!

  I dont like white naangalia kipaji zaidi; angalia kifaa hiki cheusi ti mpaka watu wakambatiza soccer god! vipi, unasemaje anaenda kwa waganga

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=MyOHbCBApus&feature=related[/ame]
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,489
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Point zako zimeeleweka hata kama hukuzipanga vizuri. Kitu kimoja ambacho tumeganda nacho tangu enzi a ukoloni ni haya mamboya kushabikia kila kitu kilichotengenezwa/kutokea nchi za magharibi. We are a dedicated followers of fashion, kama alivyoimba mwimbaji mmoja Mwingereza. Mwafrika atajivunia kuwa na latest gadgets za modern technology, iwe ni blackbery, bluray, mercedes benz, audi A8, Cadillac Escalade au Range Rover. Ukiwa na hivyo unaonekana kwamba ndio umefika. Kwa hiyo usishangae sana kuyaona hayo. Ndio maana leo Dar-es-Salaam kumejaa apples kutoka Afrika kusini na mayai na ukionekana unanunua vitu Shoprite au pale Mlimani basi wewe ni wa kisasa.
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,480
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Heri mimi Kandambili...
   
 12. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,196
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkuu hata mi nakiri kuacha kuangalia Ghana vs Egypt na nikaangalia mechi ya uingereza. Mechi ya Egypt nlikua nabip tu kuangalia.

  REASON: I was fed up with th way Egypt ilivo bebwa hasa nusu fainal.
  Nawakubal Egypt wanacheza vizur lakini marefa wamekua wakichangia kuibeba.
  Kweli iliniboa sana nkaamua kuonesha hasira zangu na kugoma kutoa ushirikiano ktk kuiangalia mechi hii ya mwisho.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Sioni hoja hapa.

  Yaani wewe unataka kunilazimisha niangalie butuabutua badala ya soka la draft kisa UAFRIKA?? Uafrika ni dhana tu, hakuna kitu kinachoitwa UAFRIKA ktk physical dimension/
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...