Shivji asema kauli ya Kamati ya EPA inatia shaka

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,011
Posted Date::3/11/2008
'Serikali inawalinda mafisadi wa EPA'
*Shivji asema kauli ya Kamati ya EPA inatia shaka

* Asema kampuni haipo bila wamiliki

Na Jackson Odoyo
Mwananchi

MHADHIRI Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Issa Shivji amesema kitendo cha Kamati ya Rais Kuchunguza Watuhumiwa wa Ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ndani ya Benki Kuu Tanzania (BoT), kukiri kuwa kazi ya kuwakamata mafisadi ni ngumu, ni ishara ya kuwalinda mafisadi hao.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana kwa njia ya simu, Prof Shivji alisema kitendo cha serikali kushindwa kuwataja watuhumiwa hao wakati inayajua makampuni yaliyotumia kuchota fedha hizo ni ishara ya mchezo mchafu unaofanyika.

Alisema kufahamika kwa makampuni na fedha kurejeshwa ni ishara tosha ya kuwafahamu wahusika kwa sababu kampuni haiwezi kuwepo bila kuwepo watu nyuma yake.

Huu ni mchezo mchafu na ni ishara ya kuwalinda watuhumiwa hao. Serikali inadibi iwe wazi katika hili, haiwezi kusema kwamba watu hawafahamiki wakati pesa zinarudishwa, kwani kitendo cha fedha kurudishwa ama kampuni kufahamika ni sawa na kuwafahamu watuhumiwa, alisema.

Alisema ingawa kisheria kampuni inakuwa tofauti na mwenye hisa, lakini hawawezi kusema kuwa hawafahamiki kwa sababu kampuni hizo zina bodi ya wakurugenzi sasa iweje waseme kwamba wamebaini makampuni tu na si wamiliki.

Alisema hili ni sawa na serikali kukiri uozo wake mbele ya wananchi na kwamba ni kitendo cha aibu kwa taifa hili, kwani haya ni mazingira ya kuwafanya wananchi wakose imani na serikali yao.

Kama katika hili serikali imeanza kuonyesha ishara ya kuwalinda mafisadi ni dhahiri kwamba nchi hii inaelekea pabaya na tusipoangalia hatutaweza kufanikiwa katika vita dhidi ya ufisadi, aliongeza.

Hata hivyo, Profesa Shivji alisema pengine serikali inaogopa kuwataja mafisadi hao na kuwafungulia mashtaka kwa kuhofia uozo ulioingia wa kutafuna mfumo wa uendeshaji kesi mahakamani.

Kwa upande wa wake mkazi wa jijini Dar es Salaam, Teonesk Katanda alisema kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Serikali kusema kwamba wenye makampuni husika hawafahamiki, si kweli kwa sababu kabla ya kampuni kusajiliwa ni lazima iwe na bodi ya wakurugenzi.

Katanda alisema kisheria, kampuni haiwezi kukopeshwa pesa benki mpaka bodi ya wakurugenzi ikae na kuweka saini kwenye mkataba kabla ya kupewa fedha, sasa inakuwaje waseme hawafahamiki?

Haingii akilini kama serikali inawezaje kusema kwamba watu hao hawafahamiki wakati makampuni yao yanafahamika. Je, waliokwenda kuchukua fedha hizo benki ni akina nani?alihoji Katanda.

Alidai kuwa serikali inatafuta namna ya kuwalinda mafisadi hao kupitia kwa mwanasheria mkuu.

"Kwanza mwanasheria huyo huyo anatuhumiwa kutowajibika ipasavyo kwenye kashfa ya Richmond, leo yupo katika kamati hiyo inayotia mashaka," aliongeza Katanda.

Alisema kwamba hakuna kipengele kilichowaruhusu watu hao wakachukue pesa hizo, hivyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali anapaswa kurejea upya katika sheria ya makampuni ama serikali iwatumie wasomi waliosomea sheria za makampuni ili wafahamu ukweli juu ya suala hilo.

Juzi Mwanyika aliwaambia waandishi wa habari kuwa, hadi sasa uchunguzi wao umebaini kwamba yapo makampuni ambayo yamehusika kuchota fedha hizo, lakini watu waliohusika bado hawajafahamika.

Wajumbe wengine wa timu hiyo ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hosea na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema.

Hata hivyo, kauli hiyo mpya ya Mwanyika imeshindwa kujibu hoja ya msingi ya wanaharakati ambayo imezingatia kauli ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo ambaye alisema serikali imeshapokea marejesho ya fedha za EPA kiasi cha Sh50 bilioni, lakini akasita kutaja majina ya watuhumiwa.
 
Huyo aliyeunda kamati hiyo lazima na yeye ni fisadi,hivyo anataka kuficha uozo huo.Ktk kamati hiyo ni said Mwe'tu ndio angalau kashfa zake ni kidogo.Huyo Osea amechukuliwa kutokana na utaalamu wake wa kudanganya kama alivyofanya kwa Richmond,Mwanyika nae ndio yaleyale.Sitegemei kupata jipya toka kamati hii.Kwa sababu muda wa kamati hiyo bado upo,Mwakyembe akbidhiwe kua mwenyeketi na Shivji awe katibu wakisaidiana na Prof.Ibrahim Juma.Kwa vichwa hivi then watanzania wangekua na matumaini makubwa juu ya mafisadi hao.
 
Huyo aliyeunda kamati hiyo lazima na yeye ni fisadi,hivyo anataka kuficha uozo huo.Ktk kamati hiyo ni said Mwe'tu ndio angalau kashfa zake ni kidogo.Huyo Osea amechukuliwa kutokana na utaalamu wake wa kudanganya kama alivyofanya kwa Richmond,Mwanyika nae ndio yaleyale.Sitegemei kupata jipya toka kamati hii.Kwa sababu muda wa kamati hiyo bado upo,Mwakyembe akbidhiwe kua mwenyeketi na Shivji awe katibu wakisaidiana na Prof.Ibrahim Juma.Kwa vichwa hivi then watanzania wangekua na matumaini makubwa juu ya mafisadi hao.

Hapa ndipo ilipo mantiki ya Msimamo wa Ushirikiano wa Vyama Vya Upinzani kwamba iundwe Tume Huru ya Kuchunguza Ufisadi wote uliotajwa katika Orodha ya Mafisadi mpaka sasa, huu wa EPA ni sehemu ndogo tu ya ufisadi huo
 
Back
Top Bottom