CONTROLA
JF-Expert Member
- Sep 15, 2019
- 6,939
- 22,963
Nawambiaga watu hamna biashara isiyo na faida chini ya JUA yani hakuna,ukiona umefungua biashara halafu wewe huoni faida tambua 1.umekosea location 2.unafungua kitu kile kile ambacho watu wanacho tayari.
tukiachana na yote hayo bado biashara inataka uvumilivu 81% unaweza ukakosea location ila ukiwa mvumilivu ukakaza hapo hapo (utatoboa) japo kwa mbinde,lakini pia unaweza kosea bidhaa ukaleta bidhaa sehemu isiyo sahihi ila ukiwa mvumilivu ukakaza hapo hapo (utatoboa) japo kwa mbinde pia.
Msingi wa biashara yyte chini ya jua ni 1.Mtaji 2.Uvumilivu ukiwa na hizi vitu viwili wewe biashara kwisha habari yesu atarudi atakukuta unafanya biashara maana wakukuweka SUB hatopatikana kwenye biashara.
Bana leo nataka niwasanue wananchi wenzangu ambao mpo ktk biashara na sasa hv umekaa ofisini kwako huoni wateja biashara kwako inazidi kuwa mbaya kadri siku zinavyoenda Afadhali ya Jana.
Sikia nikwambie ndugu yangu Hapo ulipo toka nnje ya ofisi yako angalia upande wakulia na kushoto angalia ofisi kama yako zipo ngapi? kama ni una tigo/M pesa angalia zipo ofisi ngapi za aina yako? kama unasuka kagua chochoro zote krbu na wewe kuna msusi mwingine wapi kama wewe? kama ni saloon ya kiume/kike inuka kagua kuna saloon ngapi kama yako mtaa huo?
ukitoka tu ukikutana na watu wanafanya biashara kama yako eneo lako,au mtaa wa pili fahamu upo kwenye Danger zone..Wanasemaga kwamba kwenye biashara "Ataewahi ndio Mshindi" biashara inataka hivyo wahi kufanya kitu ambacho bado watu hawajasanuka kinahela,Mfano mzuri ni mr.MAX wa max.malipo huyu mwamba ndio mtu wakwanza kula hela tamu za umeme hii nchi,enzi hyo umeme tunaenda nunua sheli foleni huku na kuleee..
Njo kwenye tigo/m pesa hii biashara n nzuri ila si nzuri kama unavyoiona sasa hv,nadhani upo hapo unaona hizo kamisheni zinakutosha kbsa (ni sawa) ila fahamu kwamba ingekulipa mara 4 ya unachokipata kama ungefanya tigo/m pesa miaka ya nyuma huko.
Kila biashara inalipa ila unapoona kila mtu anafanya biashara unayofanya,shtuka tambua anytime utaanza lia lia hali ngumu (usifurahi sanaaa) kuona mahali kuna biashara kama yako fahamu lazima mtagawana wateja,unafkiri wanaofungua biashara kama yako eneo ulilopo unadhani wanapata wapi wateja?
hamna cha kusema "kila mtu na wateja wake" huo ni uwongo,mtu anaefungua biashara kama yako eneo ulilopo kubali kataa Lazima mgawane wateja,akiongezeka mwingine nae mnagawana nae wateja,nk nk
Usisubiri maji yakufike shingoni,usisubiri sema biashara mbaya angalia tu majirani na mtaa uliopo wangapi wanafanya unachofanaya SIO tunasingizia vyuma vimekaza hali ngumu wakati sisi wenyewe akili zetu hazifunguki kuwaza zaidi.
sijasema uache unachokiifanya Point yangu ni wewe uone matokeo chanya ya biashara yako,ufungue asubuhi urudi jioni na pochi imejaa tembo sio urudi nyumbani na lawama na huzuni sasa basi ukishaona u yebo yebo umezidi HAMA.
HAMA hapo ulipo tafuta connection mahali pengine kafungue huko ofisi yako,kwani hiyo frem yako au umegundishwa kwani? kodi ikiisha tembea mbele kafungue mahali pengine biashara jitenge na hao iga iga yanini kugawana wateja wakati zipo sehemu unaweza kwenda ukafungua ukapata wateja peke ako au mkawa tu wawili kuliko kukaa sehemu ofisi mmepangana kama mahindi bana.
Kuhama sio dhambi,kuna wafanyabiashara wanaona aibu sana kuachia frem wakiamini ni dalili ya kufeli,nataka kuwambia kuwa kugandana kwenye hayo mafrem ambayo mnashnda siku nzima na bado mnarudi nyumbani hamna cha maana ndio kufeli kwenyewe.
imeisha hiyo/newspaper hilo.