Shitambala bado aiota CHADEMA

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,782
5,204
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Sambwee Shitambala, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Mkoa wa Mbeya, amekitaka Chadema kutambua kuwa siasa haiwezi kuendeshwa kwa namna ya maandamano,vurugu na uchochezi.

Amesema hayo jana wakati CCM kikizindua kampeni zake katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Majengo kwa ajili ya kumnadi mgombea wa nafasi hiyo, Samweli Mwamboma.

Shitambala alisema Chadema wamekuwa wakitumia maandamano yanayoambatana na vurugu wakidhani kuwa hiyo ndiyo njia mwafaka ya kukijenga chama chao bila kutambua kuwa Watanzani wanachotaka ni kuwa na chama ambacho kina mfumo mzuri utakaowawezesha kuwaletea maendeleo.

Alisema wananchi wa Mbeya wasikubali kuwapiga mawe viongozi na badala yake wapige kura kuwachagua viongozi waadilifu ambao wataweza kuwaletea maendeleo.

“CCM msipige mawe pigeni kura, CCM fanyeni maendeleo msifanye fujo, CCM jengeni hoja msifanye maandamano,” alisema Shitambala.

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya, Dk. Mary Mwanjelwa, alisema wanachama wa CCM watembee kifua mbele kwani serikali yao iliyopo madarakani inafanya mambo mengi ya kuwaletea maendeleo.

Naye mgombea udiwani kata ya Majengo, Samweli Mwamboma, alisema akichaguliwa atahakikisha anashirikiana na wananchi wa kata hiyo katika kuwaletea maendeleo.
 
Yuda Eskariote, alilamba mshiko akahujumu kampeni 2010. Jimbo alikuwa anashinda lile kama c kushikishwa
 
He kumbe bado yupo? Masikini Makamba alimdanganya atampa position, wht hapened makamba mwenyewe kawa gamba. Sasa bwana mdogo anahaha hana isue kumbe yupo mbeya. Safi sana ccm, alikuwa mwnyekt sasa kwenye magamba just member!
 
Zile suti naye alipewa moja..........

nzuri.JPG
 
He kumbe bado yupo? Masikini Makamba alimdanganya atampa position, wht hapened makamba mwenyewe kawa gamba. Sasa bwana mdogo anahaha hana isue kumbe yupo mbeya. Safi sana ccm, alikuwa mwnyekt sasa kwenye magamba just member!
Makamba ni sawa na nyoka aliye mdanganya Hawa, akala tunda kisha akafukuzwa kwenye Bustani ya Eden na kupewa adhabu kali ya kuzaa kwa uchungu
 
Wananchi wa Mbeya msikubali kudnganywa na huyu jamaa. Njaa yake ndiyo imempeleka CCM mbona hakujiunga na chama kingine
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom