Shitambala ajibu agizo la Dr. Slaa

Shapecha

Member
Oct 21, 2010
45
1
WAKATI uongozi wa taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ukikataa ombi la kujiuzulu kwa mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mbeya, Sambwee Shitambala, kwa kutokidhi vigezo vya katiba ya chama, mwenyekiti huyo amesisitiza hatakuwa tayari kurudi katika nafasi hiyo kwa sasa hadi hapo chama hicho kitakapomaliza kabisa uchunguzi wake.

Shitambala ambaye ni wakili wa kujitegemea alisema ataendelea kukaa nje ya cheo hicho ili kupisha uchunguzi huru dhidi ya tuhuma za rushwa zinazoelekezwa kwake lakini pia kulinda hadhi ya kazi yake ya kutetea haki za raia kupitia kada ya sheria.


Msimamo huo aliutoa jana jijini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kujibu maagizo ya chama chake, ikiwa ni siku moja tu baada ya Katibu Mkuu wa chama hicho taifa, Dk. Willibrod Slaa, kulikataa ombi lake na kumsihi aendelee na uenyekiti.

Kwa mujibu wa barua ya Shitambala aliyokiandikia chama hicho na Tanzania Daima kupata nakala yake, sababu kuu nne ndizo zilizomfikisha kwenye uamuzi wa kujiuzulu wadhifa huo.


Miongoni mwa sababu hizo ni yeye kutupiwa lawama za kupokea rushwa kwenye uchaguzi wa ubunge Jimbo la Mbeya Vijijini pamoja na mkoa kukosa mgawo wa wabunge wa viti maalumu.


Alisema mbali na ukweli ulivyo juu ya mfumo uliotumika kupata nafasi za wabunge wa viti maalumu, wanachama na baadhi ya viongozi wa chama hicho mkoa wamekuwa wakitaka majibu, hali ambayo imekuwa ikimuweka katika wakati mgumu kwani hakuhusika katika mchakato huo.

Alisema katika hali ya kushangaza uongozi huo wa juu wa chama badala ya kufikiria kwa kina hoja hizo nzito na kuzitafutia majibu yanayoweza kuwatuliza wanachama wenye hasira wao wameendelea kutoa majibu mepesi.

"Hoja iliyopo mbele ni nzito, haiingii akilini Mkoa wa Mbeya kukosa nafasi ya viti maalumu wakati tumefanya kazi kubwa ya kukiinua chama tena kwa muda mfupi, walipaswa kutoa tiba kwanza kwa hili ndipo waamuru mimi nirudi kwenye nafasi yangu," alifafanua Shitambala.

Aliongeza kuwa baada ya kupata nafasi ya kuwa mwenyekiti maisha yake yalitengenezwa katika sura mbili hivyo kitendo chake cha kuamua kujiuzulu kutokana na tuhuma za rushwa zinazotokana na mambo ya siasa kina lengo la kuokoa hadhi ya maisha ya upande wa pili wa taaluma yake ya sheria.

"Si rahisi mimi kuona maisha ya siasa yanaharibu maisha yangu ya kawaida na wala maisha yangu ya kawaida yakiharibu maisha ya siasa, ni vizuri nikaeleweka hivyo. Mimi bado ni mwanachama mwaminifu na punde yote haya yakishughulikiwa na mimi kuonekana sikuhusika basi nitarudi kuwatumikia wananchi," alisisitiza Shitambala.



Source: Tanzania Daima
 
Chama hiki cha chadema hakina msingi mzuri, subiri kitasambaratika soon, kama kawaida yao!!
 
Shitambala anayo hoja ya msingi na namkubali sana kwa mawazo haya. Ingekuwa viongozi wetu wana msimamo kama wake tungeishafika mbali sana.
 
Kwanini anahoji mambo ya kupewa Viti Maalum Mkoani Mbeya?...haoni kuwa anakibomoa Chama?...Hivi Madai haya ya kupewa viti Maalum aliyaweka wakati anajiuzulu kupisha Uchunguzi? alau yangepata muda wa kujibiwa na Slaa...na nafikiri Slaa wala asingempa muda tena wa kumuomba aendelee kukaa ktk M/Kiti...

Lkn pia kwanini hataki Kutii Amri au Ombi la katibu wake Mkuu? ambae pia ndie aliekuwa Mgombea Urais...Hivi Slaa angekuwa President angekataa kutii au Ombi lolote?
 
Katika dunia yenye demokrasia ya ulimini kama hii tuliyomo mambo kama haya ni kawaida kutokea na makubwa zaidi ya haya tutayasikia. angepata ubunge si dhani kama SHITAMBALA angekumbuka kugawiwa viti maalum MBEYA. poleni mdhaniao kua mabadiliko ya kweli yako midomoni mwa wana siasa.
 
Angalau tunaanza kuona uadilifu baina ya ya viongozi wa cdm; pale wanapo tuhumiwa wako radhi kukaa pembeni na kupisha uchunguzi.
 
katika dunia yenye demokrasia ya ulimini kama hii tuliyomo mambo kama haya ni kawaida kutokea na makubwa zaidi ya haya tutayasikia. Angepata ubunge si dhani kama shitambala angekumbuka kugawiwa viti maalum mbeya. Poleni mdhaniao kua mabadiliko ya kweli yako midomoni mwa wana siasa.

yale yale
 
na viti viwili walivyogawiwa CHADEMA baada ya kushinda Mpanda Mjini vp? nathani hili suala zima la viti maalum ni kero wavifutilie mbali!
 
na viti viwili walivyogawiwa CHADEMA baada ya kushinda Mpanda Mjini vp? nathani hili suala zima la viti maalum ni kero wavifutilie mbali!

Visifutiwile mbali hadi hapo CDM itakapotatua tatizo linalojitokeza, TATIZO HALIKIMBIWI, LINAPASWA KUTATULIWA!
 
Sababu za Shitambala zina mashiko na ni nzuri.

Nimefurahi aliposema kuwa ataendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa CHADEMA hata akiwa nje ya uongozi. CHADEMA shughulikieni suala hili lisikipake matope chama na kupungua hadhi yake. Mbeya ni eneo nyeti sana kisiasa.
 
CDM kwa nini hawateuwi tume ikaenda kuchunguza na kutolea ripoti jamani hilo nalo ni tatizo ebu uongozi wa CDM lioneni hili
 
Uyu jamaa alikula mlungula enzi z uchaguzi mdogo so kama na huu wa 2010 kala siwezi shangaaaaaaaaaaaaaaa
 
wapuuzi hawa wameona kila mtu anawakimbia itakuwa so ngoja huyu tumnganganie bado wengi soon
udini ukabila ubinafsi utawamaliza chadema nilihisi CCM pekee
 
na viti viwili walivyogawiwa CHADEMA baada ya kushinda Mpanda Mjini vp? nathani hili suala zima la viti maalum ni kero wavifutilie mbali!
Mkuu

Thanks, ila kufuta viti maalum sidhani kama ndio solution... solution ni CDM kubadili mfumo wa kupata wawakilishi wa special seats uwe wa kidemokrasia zaidi. bado kuna tatizo kubwa
 
nadhani viti maalum viendane na uwiano wa ushindi wa majimbo, mkoa ulioshinda majimbo mengi upewe viti vingi uliokosa usipewe
 
wapuuzi hawa wameona kila mtu anawakimbia itakuwa so ngoja huyu tumnganganie bado wengi soon
udini ukabila ubinafsi utawamaliza chadema nilihisi CCM pekee

Viti maalum vya CHADEMA vinakwenda kwa watu maalum , Kanda maalum na familia maalum. Hivyo vilitengwa kwa watu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha tu, na kwa familia za Slaa, Mbowe na Ndesamburo
 
Viti maalum vya CHADEMA vinakwenda kwa watu maalum , Kanda maalum na familia maalum. Hivyo vilitengwa kwa watu wa mikoa ya Kilimanjaro na Arusha tu, na kwa familia za Slaa, Mbowe na Ndesamburo

Weka ushahidi basi kuthibitisha kauli yajo. At least orodha na mahali wanakotoka, la sivyo itakuwa UDAKU!
 
Kwanini anahoji mambo ya kupewa Viti Maalum Mkoani Mbeya?...haoni kuwa anakibomoa Chama?...Hivi Madai haya ya kupewa viti Maalum aliyaweka wakati anajiuzulu kupisha Uchunguzi? alau yangepata muda wa kujibiwa na Slaa...na nafikiri Slaa wala asingempa muda tena wa kumuomba aendelee kukaa ktk M/Kiti...

Lkn pia kwanini hataki Kutii Amri au Ombi la katibu wake Mkuu? ambae pia ndie aliekuwa Mgombea Urais...Hivi Slaa angekuwa President angekataa kutii au Ombi lolote?

Chuma, haya mambo ya kukubali maombi ya "wakubwa" ndiyo yameipeleka nchi hapa ilipo. Wasiwasi wangu ni kuwa tunaweka mno maisha yetu mikononi mwa watu wengine. Kuna umbaya gani kwake kuhoji na hata kupinga amri kama ulivyoiita wewe ya katibu wake mkuu kama yeye binafsi haoni ina mashiko? Taratibu tunajitengenezea miungu tusiyoweza kuihoji! It is hight time tuwahoji! Hata angekuwa rais! Kwani nani kamweka pale? Ni maoni tu!
 
Kila ambapo binadamu yupo, hapakosekani madhaifu pia.
dawa ni kutafuta ufumbuzi kwa faida ya wengi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom