Shitaka la jinai linapochelewa kupelekwa mahakamani laweza kosa nguvu kisheria? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shitaka la jinai linapochelewa kupelekwa mahakamani laweza kosa nguvu kisheria?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Anold, Feb 22, 2011.

 1. A

  Anold JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Jirani yangu mwaka wa jana December aliripoti Polisi tukio la kutishiwa kuuwawa na mtu mmoja, pamoja na kuripoti mapema, Polisi walichukuwa muda kwenda kumkamata mtuhumiwa kitu kilichosababisha mtuhumiwa atoroke kukwepa kukamatwa na Polisi, kwakuwa mtuhumiwa ni mkazi wa eneo hilohilo kwa kuzaliwa ila makazi yake ni nje ya eneo hilo Polisi walitoa wito wa kuitwa shaurini mtuhumiwa kupitia kwa Baba yake mtuhumiwa. Pamoja na wito huo sasa ni karibu miezi miwili mtuhumiwa hajatokea na hakuna dalili kuwa atatokea. je ni hatua gani mlalamikaji anaweza kuchukua ili kesi hii iende mahakamani kwani mashahidi walioshuhudia tukiohilo sio wakazi wa hapo na wanaweza kuondoka wakati wowote je kesi hiyo inaweza kusikilizwa upande mmoja bila kuwepo mlalamikaji? wataalam naomba ushauri wenu ili tumsaidie huyu jirani.
   
 2. A

  Anold JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  jamani JF hakuna wanasheria wanaopitapita humu? au mpaka uende ofisini kwao?
   
Loading...