Shirikisho vyuo vikuu CCM lamuunga mkono Rais Magufuli

Omary Kipingu

Member
Feb 22, 2016
40
48
f72f394a-9255-41e4-865d-b609a2233064.jpg

Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, Daniel Zenda akizungumza wakati wa kufungwa Kambi ya Vijana 219, waliokuwa katika kambi ya kukuza Uzalendo, iliyowekwa Hombolo mkoani Dodoma.

Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu nchini, limewahimiza Vijana kuzidisha uadilifu na uzalendo ili kufikia malengo yatakayoakisi CCM mpya na Tanzania mpya, kama anavyotaka Mwenyekiti wa Chama, Rais John Magufuli.

"Ili matakwa haya ya Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama, yaweze kufikika, ni lazima Watanzania hasa sisi vijana, tubadilike, kifikra na kimtazamo na kuacha kufanya kazi kwa mazoea", alisema Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo, Daniel Zenda, wakati wa kufungwa kambi maalum ya siku tatu ya Vijana kutoka vyuo mbalimbali, nchini, jana, Hombolo, mkoani Dodoma.

Zenda alisema, mabadiliko ya kifikra, mtazamo na kiutendaji, ndivyo vitakavyoonyesha udhati wa vijana na Watanzania kwa jumla katika kuendelea kumuunga mkono, Rais Dk. Magufuli, katika jitihada zake za kuiletea Tanzania mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutendaji kwa kushika misingi ya kuinua uchumi huku akipambana na uzembe na ubadhirifu.

Zenda, aliwapongeza vijana 219, walioshiriki katika kambi hiyo, akisema, mafunzo ya ukakamavu na yale ya kujenga utaifa, waiyopata kwa muda wa siku tatu hadi kufikia jana, yatawasaidia sana, katika kutambua nafasi yao katika kulitumikia taifa kwa uadilifu na uzalendo mkubwa.

Aliwataka Wanashirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu katika mikoa mbalimbali kuendelea kufanya shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwa ni kutekeleza maagizo yanayotaka kila mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuhakikisha anashiriki shughuli kama hizo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 40 ya kuzaliwa kwa CCM.

Zenda aliipongeza Viongozi wa Shirikisho katika baadhi ya mikoa ikiwemo Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Dodoma ambao tayari wamekuwa wakishirikiachama na wanachama na wananchi kwa jumla katika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi na kujitolea damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo ya miaka 40 ya CCM ambayo kilele chake ni Februari 5, 2017.

Kambi hiyo ya Hombolo ilifungwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Zainabu Abdalla Issa, ambaye akifunga kambi hiyo alisema, kwa kuwa CCM imekuwa ikionyesha kuwajali vijana kwa kuweka mipango mbalimbali ya kuwaendeleza sambamba na watanzania wengine, basi hawana budi nao kuhakikisha CCM inazidi kuimarika na kuwa CCM mpya.
 
Tamko zuri lakini liko limited, mfano akimaliza muda wake watakidhi lengo la nani tena.
Wanatakiwa kuwa waadilifu na wazalendo kwa taifa lao wakati wote vipindi vyote.
Uadilifu,Uzalendo iwe ni ndio misingi ya shilikisho lao wakati wote, Miaka iliyopita, huu uliopo na ijayo.

Taasisi ya wasomi inabidi iwe na maono ya kitaifa na endelevu
 
Mkuu,maono na akili zao ziko kwenye chama na sio taifa. Ndio maana speech yao inaongelea chama na sio taifa.
 
Tamko zuri lakini liko limited, mfano akimaliza muda wake watakidhi lengo la nani tena.
Wanatakiwa kuwa waadilifu na wazalendo kwa taifa lao wakati wote vipindi vyote.
Uadilifu,Uzalendo iwe ni ndio misingi ya shilikisho lao wakati wote, Miaka iliyopita, huu uliopo na ijayo.

Taasisi ya wasomi inabidi iwe na maono ya kitaifa na endelevu
Good
 
Hawa njaa zinawasumbua
Wanamuunga mkono kwa kujenga uwanja wa ndege mkubwa kwao Chato?
Wanamuunga mkono kwa kujenga ghorofa la TRA huko kijijini Chato?
Wanamuunga mkono kwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari pamoja na mitandao ya kijamii?
Wanamuunga mkono kwa kuhonga wabunge wa CCM kila mbunge milioni 10?
Wanamuunga mkono kwa kula pesa za rambi rambi huko Kagera?
Wanamuunga mkono kwa kusababisha hali ya maisha kuwa ngumu?
Wanamuunga mkono kwa kushusha hali ya uchumi?
 
Awamu hii hata ujipendekeze vipi mkulu hatoi bonus za vyeo nyie endeleeni na uzalendo wenu.
Zero hao watoto nikiwa na toto likifika Chuo kikuu lipende Uvccm ntakaa na mama yake aniambie vzr alikomtoa maana litakuwa sio langu
 
Back
Top Bottom