Shiriki uzoefu wangu wa .. - usiku wa giza

salosalo

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
596
278
Wana JF, naomba niwashirikishe uzoefu wangu japo kidogo tu.
Nilipokuwa nasoma elimu ya juu nilikuwa nikipewa jumla ya sh. 420,000/- kwa semister moja yenye siku 120 kama pesa ya chakula na sponsor wngu, inamaana sh 3500/siku. Haikutosha, nilikuwa napewa sh. 300,000/ ya stationery kwa semister mbili. Jumla nilikuwa naweka kibindoni jumla ya sh 570,000/- kwa semister(siku 120). Yaani nilikuwa nachukia na kupata hasira huku nikiomba nimalize haraka chuo ili niende uraiani nikaajiriwe.

Niliamini chuo kilikuwa kinachelewesha maendeleo yangu mno. Nilijua nikimaliza ntalipwa zaidi ya sh 570,000/ kwa mwezi(siku 30) badala ya 570,000 kwa miezi minne. Dooooh! sasa nazikumbuka zile pesa za chuo japo zilikuwa za mkopo. tangu 2009 sijaona ajira pamoja na jitihada nyingi ninazofanya. NISAMEHE CHUO MAANA NILIKUSINGIZIA, ETI UNANICHELEWESHEA MAENDELEO NA UTAJIRI. Nakukumbuka rafiki yangu wa zamani (chuo), rafiki mpya niliyemtegemea(kazi) kwa kukuacha wewe ananikimbia hadi leo.

n
 
Kila nikiwafikiria watu waliopo mtaani bila ajira wakati wana elimu nzuri tu, namshukuru Mungu kwa hiki kibarua nilichonacho na motivation ya kufanya kazi inaongezeka mara mbili zaidi. Pole sana mkubwa na jipe moyo, kazi itakuja tu one day.
 
mkuu ID yako ina-match na maneno yako...big up
 
Kila nikiwafikiria watu waliopo mtaani bila ajira wakati wana elimu nzuri tu, namshukuru Mungu kwa hiki kibarua nilichonacho na motivation ya kufanya kazi inaongezeka mara mbili zaidi. Pole sana mkubwa na jipe moyo, kazi itakuja tu one day.

Alah! Yaani kumbe matatizo yetu ya ajira ndio motivation yako? kweli Kufa kufaana. Inamaana bila sisi kukosa kazi morale yako ya kazi ingeshuka au kuisha kabisa?

Hiyo nyekundu hapo juu iko poa sana. Hongera kwa uwezo wako mkubwa wa kubadilisha matatizo yetu kuwa mtaji kwako.
 
pole,ila ukiingia sehemu ya jf ujasiriamali utatoka tu, zipuuze ajira za kuajiriwa, jiajiri
 
Dah, yaani umeongea ukweli mtupu.Jipe moyo na wala usikate Tamaa maana watu kama wewe tupo wengi tu mtaani tunasubiri majaliwa yetu, kifupi mimi ni tangu 08, ila sijakata tamaa.
 
[/COLOR]

Alah! Yaani kumbe matatizo yetu ya ajira ndio motivation yako? kweli Kufa kufaana. Inamaana bila sisi kukosa kazi morale yako ya kazi ingeshuka au kuisha kabisa?

Hiyo nyekundu hapo juu iko poa sana. Hongera kwa uwezo wako mkubwa wa kubadilisha matatizo yetu kuwa mtaji kwako.

lol, kweli mkuu uko gizani kiasi kwamba umeshindwa kuilewa mistari ya tc. dah! haya pole bana
 
Dah, yaani umeongea ukweli mtupu.Jipe moyo na wala usikate Tamaa maana watu kama wewe tupo wengi tu mtaani tunasubiri majaliwa yetu, kifupi mimi ni tangu 08, ila sijakata tamaa.

Da! pole na wewe mkuu. Mimi nilidhani niko mwenyewe. Ila kama ulivyosema safari yetu ya kupigika iko ukingoni
 
Tuendelee kuombeana kila la kheri, ila sio mbaya kujishikiza hata kwa kishika chaki maana mtaani bila kukomaa kugumu sana.
 
Nikickia hayo nakata tamaa,maana ndo nimeingia mtaani mwezi june tu na naona nachelewa kupata kazi.
 
Back
Top Bottom