Shiriki shindano la #ChinaMade kujishindia simu ya Huawei au Xiaomi Arm Band

#ChinaMade

Stori yangu inahusu dawa ya kutibu malaria sugu ambayo imetengenezwa kutoka CHINA inaitwa DUOCOTEXCIN,inauzwa kuanzia shilingi 12,000

Mwaka jana(2014) niliugua malaria nikalazwa hospitali mjini BUNDA nakuongezewa maji ya quinin pamoja na vidonge vyake lakini sikupona na hali ilizidi kuwa mbaya karibu ya kufa, daktari alinibadilisha dozi na kunipatia DUOCOTEXCIN ambayoimetengenezwa kutoka CHINA.

Kwa kweli Papohapo nilipata nafuu na kuruhusiwa kuondoka hospitali, hivyo dawa hii naipenda sana kwa tiba ya malaria sugu kwani inanguvu ya uponyaji iliyokatika hali ya juu.
 
#ChinaMade

Stori yangu fupi:

Refurbished phones za China zimenipa pesa sana kuna jamaa zangu walikua wanantumia simu mi huku nauza na napata faida mara mbili ya ile bei walionunua kule.

Pia kitu ambacho sitokisahau ni kipindi zinaanza kutoka electronic e-ciggarates China walikuwa nazo kwa bei chee. China walikua wanauza 30rmb kama 10,000tsh na zikitumwa huku nilikuwa nauza 35,000tsh dah aisee nilipiga hela sana..wabarikiwe
 
#ChinaMade

Mimi ni mtanzania na najivunia sana kutumia bidhaa kutoka china hasa hasa hii simu yangu ya Huawei y530 ambayo inakaa na chaji muda mrefu sana ukilinganisha na smartphone zingine. Naandika hii post kwa kutumia hiyo simu yangu ya Huawei y530.

kabla ya hapo nlikua nkitimia simu ya itel ambayo ilkua sio smartphone. Hivyo nkaiuza ili niongezee pesa na kununua hii huawei y530. Nmedumu nayo kwa muda mrefu sana.

#ChinaMade ndo habari ya mjini. Asante
 
#Chinamade

Mnamo mwaka 2012 nilifurahishwa na msaada wa simu za kichina ambazo zimekua ni mkombozi wa sisi watu wa hali ya chini tarehe 31 August 2012 marehemu baba yangu kipenzi alizidiwa nikiwa nae peke yangu nyumbani baada ya week moja kupita tangu mama yangu aliyeparalize kupelekwa Mwanza kwa matibabu zaidi na kutuacha nyumbani na baba alipozidiwa sikuwa na msaada wowote zaidi ya simu yangu ya mchina niliyoweza kumiliki.

Kutokana na unafuu wake niliweza kutoa taarifa kwa ndugu zangu na wakanitumia pesa iliyonisaidia kumpeleka mzee wangu hospital na kupatiwa matibabu japo week 2 baadae aliaga dunia Mungu amrehemu.

Hivyo ni shukrani zangu za dhati kwa makampuni yote ya kichina kwa kuweza kuturahisishia huduma kama mawasiliano kwa bei nafuu bila wao nisingeweza kumiliki simu na mzee wangu angefia mikononi mwangu maana alikuwa kaishiwa damu.

Asanteni sana kwa bidhaa za kichina zinatupa fursa watu wa kipato cha chini kuzitumia..
 
#ChinaMade

Ilikuwa mwaka 2003 matumaini kuendelea na masomo baada ya kukaa nyumbani kwa muda wa miezi minne kufuatia kuharibika kwa mota ya mashine ya kusagia nafaka ambayo ilikuwa inatusomesha watoto wa tatu, baba mkulima na mama mkulima.

Baada ya kununua mota ya kichina aina ya #CT25MADEINCHINA mashine ilitengamaa na hatimaye tuliweza kurudi shule ya sekondari Mbangamao iliyoko mkoani Ruvuma wilaya ya mbinga na kuhitimu kidato cha nne mimi na mdogo wangu huku kaka yetu Gody akimaliza kidato cha sita na baadaye Diploma ya ualimu.

Leo nimepata kazi Mwanza, ile mota mpaka leo bado inapiga kazi ,na tumenunua pikipiki mbili kupitia mashine hiyo inayosukumwa kwa mota aina ya ct25 iliyofungwa mwaka 2003 hadi leo hii.

MWISHO.
 
#ChinaMade.

Unajua kinachokela katika bidha za china? ningumu kujua kipi ni feki na kipi ni orignal. inakua ningumu kujua ubora halisi wa bidhaa kutoka china. mfano unapofikiria kununua simu, kulingana na bajeti yako unajua ni simu ya hadhi gani waweza pata. namaanisha features zilizomo katika hio simu. chakushangaza ukifika sokoni na ukakutana na simu ya kichina yabei ndogo kabisa ina features zote ambazo simu ya bei kubwa huwanazo.

kwa muda huo ukiwa sokoni huwezi gundua kwa haraka ufanisi wa hizo features zilizopo.

Najua wachina sio bidhaa zote ni feki, Hapana. Tatizo ni kugundua kama bidhaa ni feki au laa. watu wengi wanatumia bidhaa za china original bila tatizo na kwa mda mrefu zaidi.

nadhani wakazanie kuwaelewesha watu jinsi ya kugundua bidhaa orijino na feki, watuwengi wakielewa zile bidhaa feki zitapotea sokoni zenyewe. pia wakielimisha vizuri jamii watapata imani ya bidhaa kutoka china kama ilivyo bidhaa kutoka marekani na nchi zengine zilizoendelea

Asanteni kwa kusoma kwa ufupi zaidi hili andiko.

Afadhali umekuwa mkweli
 
#ChinaMade

Bodaboda yangu ya kwanza kununua ilikuwa FEKON, nilimpa kijana akawa akiniletea shilingi 7000 kila siku, kiukweli ni imara sana na hata nikaudharau usemi wa kwamba bidhaa za China ni fake, ndani ya mwaka mmoja nikapata nyingine, sikutaka kubadili brand hivyo nikanunua tena FEKON, made in China.

Kiukweli sijawahi kujuta kutumia bidhaa za China wakati wowote nilipopata fursa. Mpaka sasa nina miradi kadhaa lakini najua mwanzo wa yote ulianzia katika bidhaa iliyotokea China, hivyo nawapongeza wajasiriamali wa China kwa kututengenezea bidhaa imara kwa bei affordable kwetu sisi wajasiriamali wadogo. Keep it up China!

#ChinaMade
 
#ChinaMade

Everyone has a story,and this is mine.

I was saved from death due to Severe Malaria by a Chinese medicine namely ARTEQUICK; Which apparently I got it in a way you can't imagine!Karibu usome story yangu fupi;

Mwaka 2014 nilikuwa naishi maisha ya mtaani.Nilikuwa naishi kwa shida sana maeneo ya Coco beach.Siku moja niliamka nikiwa naumwa sana.Nikaamua niende kupima pale Oysterbay dispensary. Kabla ya kupima,nilizimia mara tatu pale pale kiasi kwamba manesi wakawa wanasisitiza niwape namba ya ndugu yangu mmojawapo ili wampigie aje .

Kwa jinsi nilivyokuwa naishi,sikuwa na mawasiliano na ndugu yeyote.Kwa hiyo nikawaomba nipime halafu waniandikie tu dawa.Nilipopima ikaonekana nina Malaria kali,wakasisitiza ni muhimu nilazwe.Lakini kwa hali nikawaomba waniandikie tu dawa maana nikilazwa hakuna wa kunihudumia wala wa kulipia gharama.

Dawa ikaonekana zinagharimu Tsh 8,000/-.Mfukoni nilikuwa nina Tsh.500/- tu! Ikabidi nikawadanganya kuwa naenda kuchukua hela,wakaniruhusu niende.

Mungu si Athumani,nilikuwa na kawaida ya kupita katika 'jalala' moja lipo nje ya apartment ya foreigners mitaa ya Oysterbay. Lengo nipate japo mabaki ya mikate waliyotupa.Lakini wakati natazama kipi kitanifaa nikaona pakiti fulani ikanivutia kuitazama.

Ilikuwa sealed na ndani yake mlikuwa na vidonge viwili.*Kusoma kiingereza najua* so nikagundua ile ni dawa inaitwa "ARTEQUICK ".Niliposoma zaidi nikagundua ni dawa ya Kichina inatibu Malaria hata Malaria kali! Na si hivyo tu,bali pia dosage yake ni vidonge viwili tu kwa masaa 48... kidonge kimoja baada ya masaa 24.Oh you can't imagine my happiness!

Nikacheck expiry date,nikakuta bado miezi kadhaa kuisha muda wake.Nikacheki vizuri nikakuta bado ipo sealed!!So nikajiridhisha kuwa inafaa kutumika!

Aisee yaani nikajihisi kupona ghafla.Kwasabu nilikuwa nimepata dawa!! Kwa kufupisha story ni kuwa... baada ya kunywa kidonge kimoja,ilinimaliza nguvu kabisa!mpaka nikahisi nakufa maana nilikuwa nashindwa hata kugeuka. Nilikunywa kidonge cha kwanza mida ya saa kumi jioni hivi.

Namshukuru Mungu mida ya saa sita usiku nguvu zilianza kurejea taratibu na hatimaye siku ya pili nilipokunywa kidonge cha pili nikapona kabisa. Kwa hiyo nilipona severe Malaria kwa vidonge viwili tu.

Ukiniuliza dawa bora ya Malaria hata sasa ntakutajia bila kufikiria kuwa ni "ARTEQUICK".

Ni dawa ya kichina iliyookoa maisha yangu. Sitasahau!!

Mimi ninashukuru.
 
#ChinaMade
Natumia Startimes, FEKON,Tecno H6,Tecno R5,bidhaa hizi nimeridhika nazo na ni nzuri kwa kweli.Pikipiki nimeifanya Bodaboda kuniongezea kipato na familia yangu.Mimi na wife tunatumia simu za Tecno mwanzo mwisho.Viva China.
 
#Chinamade

Siji kusahau nilipokatwa mshahara wangu na mchina kampuni ya CCECC baada ya kupoteza sururu na chepe wakati wa ujenzi wa barabara mkoani Njombe wilaya ya Makete. Kumbe masikini vyote vilijifukia kwenye kifusi wakati wa kuchimba mitaro ya maji huku nikiwa na majonzi moyoni kwa kukatwa mshahara.

Mungu si Athumani nilivipata baada ya wiki 2 kupita wakati wa kufanya usafi na ninachomshukuru mungu nilivikuta katika hali nzuri, havijapatwa na kutu!

Ama kweli China inatengeneza vifaa vizuri vya ujenzi na kwa kuwa mtoto nililelewa katika mazingira ya kidini ilinipasa nimpelekee bosi wangu Mr. Lu na yeye bila hiyana pesa aliyonikata akanirudishia pale pale.

Ahsante simulizi yangu imeishia hapo.
 
#Chinamade. Maisha yamekuwa rahisi kwa maana ya upatikanaji wa bidhaa au huduma.Kwangu mimi nina mambo mawili ya kuzungumzia.

1.Uwepo wa pikipiki za China mfano SANLG n.k.umerahisisha mambo sana. Tukumbuke pikipiki enzi hizo ilikuwa kwa padre, afisa kilimo(w), afisa tarafa, basi. Leo madechina ni noma, kila kona si mnaona.ukiacha hilo bei zake zinawezekana, linganisha bei za 110 Honda, Yamaha n.k.

2.Taa na tochi za mchina. Adha ya kutumia kibatari wote mnajua, tena serikali ilipopandisha bei ya mafuta ya taa tabu ikakua ikawa shida, lakini wachina bwana, mara solata, mara vitochi vya betery, hatujakaa sawa mara sola za bei nafuu, yaaani we acha tu.

WACHINA WAKO JUU eee! Nisisahau na haka ka simu ka Tecno ninakotumia ka elfu 50, enzi hizo upate wapi? Hadi JF nipo!
 
#Chinamade

Mimi nimenufaika sana na simu nyingi ninazozitumia za China. Zina faida zifuatavyo;

>Bei nafuu
>Spead ya kasi mtandaoni
>Mwonekano mzuri

Na pia inanisaidia kuwasiliana na ndugu zangu muda wowote. Natumia bidhaa nyingi za kichina ziko vizur sana..
 
#Chinamade Mimi ni mkulima wa kilimo cha umwagiliji. Mwaka huu mwezi wa pili nilinunua waterpump aina ya boss. Nikawa nimelima bustani ya nyanya,sikuamini kwenye mavuno maana nilivuna mara tatu zaidi ya mavuno ya hapo mwanzo,hvo ndo nimenufaika
 
#Chinamade

Uwepo wa bidhaa za China hasa katika soko la Africa imekuwa faida kubwa kwangu. Katika upande wa mawasiliano #Chinamade imenisaidia kwa kweli kwa sasa natumia simu ya Tecno boom j7 ambayo imekuwa msaada kwangu..

Hii ni simu yangu ya 4 baada ya Tecno h6, Tecno t612, Tecno m3.
 
[URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] [/URL] [/URL]

Kwanza napenda kutoa pongezi kwawatu wa china kwa kutengeneza vitu ambavyo watu wa makundi yote waweza kumiliki.

Naomba nianze kwa kutoa manufaa nilio pata [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] [/URL] [/URL] Kwanza nimeweza kumiliki simu mpapaso ambayo apo nyuma ilikua ni gharama kubwa sana lakini kwa sasa namiliki HUAWEI Y300.

Pili [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] [/URL] [/URL] imeniwezesha kupata shahada yangu ya kwanza kwani kutumia pikipiki ambayo [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] [/URL] [/URL] niliweza kusoma Open university na kuhuzulia masomo kutoka kijijini.

Tatu [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] [/URL] [/URL] iliniwezesha kutafuta material kwajili ya masomo yangu kwani niliweza nunua laptop ambayo [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] [/URL] [/URL] na kuniwezesha kupata material tofauti.

Nne [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] [/URL] [/URL] imeniwezesha kubadili maisha yangu kwani apa chumbani kwangu kuna Kabati ya nguo na ya viombo,meza ya kioo,viti ..... vyote [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina][URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] [/URL] [/URL] ambavyo vyote kwa hali yangu nimeweza kununua na hali yangu ya chini.

Tano tochi ambayo #madechina iliniwezesha kusoma na kuandaa kazi mbali mbali nilizo kuwa napewa chuoni kwani nilikua nakaa kijijini ambapo ameme bado aujafika.

Mwisho [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] imebadili maisha ya watu wengi Africa na Duniani kwa ujumla kwani ni vitu vya gharama ya chini na vitu vya aina zote yani Mawasiliano,Usafilishaji,Mavazi,Vyakura,Mapambona vingine vingi tu na napenda kusema [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL] imebadili maisha yangu kama nilivyo elezea apo juu.
Aksante sana [URL=https://www.jamiiforums.com/usertag.php?do=list&action=hash&hash=madechina]#madechina [/URL]
 
#MadeChina

Nimeanza Kutumia Bidhaa Za China Zaidi Ya Miaka 15 Nyuma, Kwa Sasa Baadhi Ya Bidhaa Za China Ninazotumia Tv, Pasi, Feni, Radio Ndogo 3 Mojawapo Ya Redio Ndogo Hio Ina Scene Yenye Kuonyesha,subwoofer, Dvd, Na Sim Ya Mkononi.

Lakini Moja Kati Ya Bidhaa Za China Zinazonivutia Ni Filam Za China, Filam Hizo Pamoja Na Waandaji Na Washiriki Wake Walio Mahiri Hakika Kwangu Imekua Ni Bidhaa Za China Zenye Mvuto Sana Kwangu Na Hata Jamii Inayonizunguka.

Moja Kati Ya Filam IlioNivutia Ni Easterin Condars, Forteen Blades, Inter The Dragon, China White, China Strike Force Nk. Na Baadhi Ya Wacheza Filam Wanaonivutia Sana Pengine Kuliko Wote Ni Yuen Biao, ---- Yeung, Sammo Hung, Donnie Yen Bila Ya Kumsahau Marehemu Bruce Lee.

Viva China Endeleeni Kusonga Mbele.
 
#ChinaMade

Sikuwa nimewahi kufikiria kuwa nina bidhaa nyingi ninazotumia kwa ajili ya biashara zangu na nyumbani mpaka baada ya kuona shindano hili la Made In China na nimeliona kwa sababu nimekuwa nikifuatilia bidhaa mbalimbali kupitia mtandao mbalimbali ya china kama Aliexpress na Alibaba.

Nilianza kujua brand za kichina kwa undani zaidi mwaka 2009 nilipozawadiwa laptop aina ya Acer na tablet aina ya Ainol Novo II zote kutoka China. Miaka minne baada ya kutumia laptop hii niliamua kubadili betri ya laptop lakini cha ajabu bei yake dukani ilikuwa juu sana kati ya laki na nusu mpaka laki mbili ndipo nilipoamua kununua betri hii kupitia mtandao wa Aliexpress wa China kwa gharama ambayo haikuzidi 65,000/-

Tangia hapo nimekuwa nikitumia bidhaa nyingi za kichina kuendeshae biashara yangu ya masomo kupitia videos/DVD na vitabu. Nimetumia makopo ya DVD zaidi ya elfu tano na pia nimetumia wino kwa ajili ya kuprint kwenye DVD na vitabu ambapo wino kutoka nchi nyingie gharama ni 40,000/- kwa kila kidau cha wino na zipo sita tofauti kufanya jumla kuwa 240,000/- lakini kutoka nchini China ni 5,000/- kufanya jumla yake kuwa ni 30,000/-.

Baada ya kuamini bidhaa za kichina mwaka huu nilinunua bidhaa kwa ajili ya biasharaya laundry aina ya VON hotpoint washing machine na Mengchi . Pia nina solar panel na inverter kutoka china

UZOEFU WANGU WA BIDHAA ZA CHINA

  • China wanabidhaa nzuri na bora sababu wanatoa warranty kwa bidhaa zao Vonpoint washing machine nimepata waranti ya mwaka mmoja na Mengchi garmet steamer ni miaka miwili.
  • Bei zao ni nafuu, wakati wa kununua battery ya laptop nilipata battery kutoka nchi nyingine kwa gharama ya 150,000 mpaka 200,000/- , lakini niliweza kuagiza kupitia mtandao wa aliexpress kwa 65,000/-.
  • China wanao mitandao mikubwa ya kibiashara kama aliexpres na alibaba, kupitia mitandao hii nimenunu bidhaa nyingi sana

Asante.
 
#ChinaMade

Nimefanikiwa kujuana na supplier wengi kutoka China na kununua bidhaa zao kwa bei nafuuu kama GPS Tracker, pia wamefanikisha mimi kujiunga na Alliexpress na kupata bei za bidhaa mbalimbali hapo kwa hapo na nimeshanunua bidhaa nyingi kutoka China zenye thamani ya zaidi ya dola 6000 na zote nimezipata kwa wakati.

Huwa natumia DHL au China post mail kutegemea na uharaka wa mzigo ninaoutaka.jamaa ni wa kweli na wana uhakika na biashara zao.

KEEP IT UP Made in China am your member with ID joh2np@yahoo.com
 
#ChinaMade

Mara ya kwanza kusikia bidhaa ya kichina niliambiwa kuwa ni feki na hazina ubora madhubuti, kumbe nilidanganywa. Nilipofikia hatua ya kuweza kujinunulia kitu chochote mwenyewe Bila msaada wa wazazi nilinunua simu ya kichina Tecno M3 na hapo ndipo nilipojua ukweli wa mambo kwamba bidhaa za kichina ni imara na madhubuti.

Hapo tayari tangu utotoni nimeshatumia bidhaa nyingi sana za kichina kuanzia nguo za ndani, raba za michezo, masweta. Nikisikia Guanzhou najua yes brand ya kichina mbele yangu.

Hapa tu kuona huu uzi imebidi nijikumbushie Movie za Kichina mbili nizipendazo ya kwanza ni The Bodyguard ya Jet Li na ya pili ni Drunken Master Jackie Chan. Bila kusahau tamthilia kutoka kwa watu wa Jamhuri ya China Mao Dou Dou na Mama Wakweze pamoja na Matumaini ya Baba kupitia moja ya Television nchini zilinivutia sana na nikajua utamaduni wa watu wa China kwa undani.

HAPA PIA NAANDIKA KUPITIA DEVICE YA KICHINA.

Viva China.
 
#Chinamade

Mimi kilichonifurahisha na kuninufaisha ambacho ningependa kila mtu afahamu ni kifaa cha kutunzia umeme ambacho naweza kutumia kichajia simu pale simu yangu inapoishiwa chaji.

Kifaa hiki kinaitwa power bank (Universal Mobile Power Bank). Kifaa hiki kinanisaidia sana hasa pale ninapokuwa sehemu ambazo hazina umeme hasa vijijini.

Nanufaika nacho sababu kinaniwezesha kuwasiliana na ndugu na jamaa na kunirahishia shughuli zangu za kila siku. Sababu mazingira ya vijijini mengi hayana umeme.

Hivo basi, kama unakaa sehemu ambayo haina umeme, hakikisha unanunua kifaa hiki. kitakusaidia sana na hautakwama tena.

Hongera sana China kwa kuturahisishia maisha.
 
Back
Top Bottom