Elections 2010 Shiriki kura ya maoni ya wafanyakazi wa Tanzania - Uchaguzi mkuu 2010

Liganga

Senior Member
Jul 4, 2007
165
125
Ndugu mfanyakazi,

Baada ya taasisi mbalimbali kutoa matokeo yake,

ni nafasi ya wafanyakazi na sisi kushiriki katika utafiti huu ambao ni jukwaa la wafanyakazi kutoa maoni yao

Tafadhali bonyeza link hapa chini ili uweze kushiriki:

Survey provided by FreeOnlineSurveys.com

Tunatanguliza shukrani zetu.

Timu ya watafiti

Tuma kwa wafanyakazi wote

HUITAJI KUREGISTER BAADA YA KUMALIZA SURVEY (Ignore that page)
 
tumeliwa kweupeee. msiifuate hiyo link


HAZITAKI KURA ZENU

Hazitaki amesema, kwa hakika hazitaki,
Mbona mna muandama, kwa kisa kile na hiki,
Kikwete mtu mzima, na wala msihamaki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Pendo kitu cha hiari, hakina lazima katu,
Ni vema kujihadhari, msizidi kuthubutu,
Si kwa kero nazo shari, mumwache mwana wa watu,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mapenzi kweli maua, huweza ota popote,
Bali huhitaji nia, kuyahudumia yote,
Bila maji kumwagia, Hunyauka kwa vyovyote,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Wafanyakazi hataki, mwataka nini zaidi?
Msitumie mikiki, hali mu watu weledi,
Binadamu ana haki, kupima na kukaidi,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mbona hamna simile, huria kumuachia,
Mmeng'ang'ana na lile, hamtaki kusikia,
M-bembeleze milele, hataki kawaambia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Mmejawa na hiana, kwa jibu alilotoa,
Kawaeleza bayana, wazi amewaambia,
Mwalitafuta laana, msilolitarajia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Kwa uvumba na ubani, kesha sema hazitaki,
Zaidi mwataka nini, awaeleze rafiki?
Tulia mkae chini, muwaze na kuhakiki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Hazitaki kakataa, kura zenu kasusia,
Japo mlete gitaa, na nyimbo kumuimbia,
Mumtembeze mitaa, kwa manoti mia mia,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.

Hazitaki si ajabu, kura zisizo na soko,
Msiitafute tabu, kujipendekeza mwiko,
Bure mwajipa aibu, kwa kumpa mialiko,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.


Kaditamati shairi, kura zenu hazitaki,
Kila kitu ni hiari, shuruti haina haki,
Kuchagua ni fahari, lazima haipendeki,
Wazi amewaambia, kura zenu hazitaki.
 
Watumishi wote wa umma walikwisha ji-organize na kukubaliana bila ajizi kwamba kura alizozikata kikwete pamoja na za ndugu zao na jamaa zao wanaowategemea watazipeleka kwa Mhe. Rais mtarajiwa Dr. (kwa kweli siyo wa heshima bandia) Slaa. Sasa maoni ya nini???? Au kuna kikundi cha mafisadi kinataka kubadili msimamo huu!!!!!
 
Back
Top Bottom