Uchaguzi 2020 Shiriki katika historia hii itakayoandikwa siku ya upigaji kura

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,810
Si wananchi, si Polisi, si Wanajeshi si Vyombo vya Usalama si wafanyakazi serikalini,wote wameshaichoka CCM kwa jinsi inavyowahangaisha, njooni huku twendeni kule watu hawana raha na maisha wapo mbioni tu wakitakiwa kuilinda CCM, ambayo bila ya kuwatisha watu kwa barua za kuhudhuria mikutano na kuweka waimbaji mastaa asingehudhuria mtu.

Watajwa hapo juu msiogope kitu kura ni siri na hakikisha unaondoa udhia huo unaowakumba kwa kuikataa CCM kwenye sanduku la kura, unaogopa nini, nani wakati CCM inachinjwa tarehe hio, wewe ukiwa mmoja wapo wa kuisitisha uhai wake.

Shiriki katika historia hii itakayoandikwa siku ya upigaji kura ambayo itabakia kuandikwa na kusomwakwa muda mrefu, chukua maamuzi magumu ya kuiweka na kuipumzisha CCM.

CCM wameshaanza kunyonyoka magoya na siku ya Uchaguzi wanakatwa mbawa, Wewe shiriki kuwachinja kwenye sanduku la kura na kuikataa milele.
 
Hujui jirani yako atampigia kura nani among 15 presidential aspirants, hivyo kauli zako za ccm au saccos kuchinjwa 28/10/20 ni propaganda za kisiasa.
 
Wanajeshi wanapigia kura kwenye kambi zao za jeshi, na mahesabu yanafanyika hapo hapo kambini, atakayepigia kura chama pinzani watamhesabu kama msaliti.
 
Huu ujumbe ulishatolewa tangia wakati wa Mrema akiwa NCCR uchaguzi wa 95, ukatolewa tena wakati wa Lipumba uchaguzi wa 2000 na mwisho ulitolewa 2015 Lowassa akiwa mgombea urais, lakini umepuuzwa marazote.

Kumbuka Mrema alikua waziri na alikuja upinzani akiwa na nguvu na ushawishi kwa watanzania,na Lowasa pia ni hivyo, lakini watanzania waliwapuuza.
 
2015 Lowasa hakushindwa, sema tume yenu iligoma kumtangaza! Siku ambayo tume ya uchaguzi itakuwa huru ndio siku ya kifo cha CCM! Tutaizika kama KANU kule Kenya!
 
Back
Top Bottom