Shirika linallotambua ndoa za mashoga latua tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shirika linallotambua ndoa za mashoga latua tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Netanyahu, Oct 23, 2008.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Oct 23, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Shirika linallotambua ndoa za mashoga latua TANZANIA

  Katika gazeti la Tanzania la Daily News tarehe 22 October 2008 Ukurasa wa 13 Kuna shirika linaitwa PADAIDS lenye website www.Padaids.org limetangaza nafasi za kazi kwa watanzania kujiunga nalo.

  Shirika hilo kufuatana na website yao linajulikana kama Elizabeth Glaser Pediatric AIDS Foundation.

  Moja ya mafao wanayotoa kwa waajiriwa wao chini ya heading -Benefits at the Foundation-Caring for Your Health wanasema ni

  “The Foundation offers medical, dental, and vision coverage for eligible same-sex domestic partners.”

  Ni shirika linalotambua ndoa za jinsia moja na liko tayari kuwapa maruprupu ya matibabu ya watu wa aina hiyo wao mashoga wa kiume au kike ili mradi wameoana kihalali.

  Na sasa hivi liko Tanzania

  Anwani waliyoweka gazetini kuonyesha walipo ofisi zao kwenye website yao ni:

  P.O. Box1628,
  Plot #576 Chole Road, Masaki
  Dar Es Salaam, Tanzania
  Phone: 255-22-260-1692/4
  Fax: 255-22-260-1696

  Lakini anwani ya Partners wao Tanzania waliowaonyesha gazetini Kuwa CV zipelekwe huko ni :

  The human resource Officer,EGPAF
  P.O. Box1628,
  OYSTERBAY,HAILE SELASIE ROAD PLOT 8 & 10
  Dar Es Salaam, Tanzania
  Phone: 255-22-260-1692/4
  Fax: 255-22-260-1696

  Ni vizuri au vibaya waajiri kuanza kuzitambua ndoa za mashoga wa kike na kiume Tanzania kuiga mfano wa shirika hilo na hao partners wao?

  Serikali inasemaje? Mapadri na mashekhe na wapagani mnasemaje? Na wana jamii forum mnasemaje? Any Comment?
   
  Last edited by a moderator: Oct 23, 2008
 2. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2008
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,758
  Trophy Points: 280
  Netanyahu nadhani hili shirika halina kosa lolote. Mimi nalijua ni shirika la kimarekani na linasaidia sana kwenye developing countries.

  Hili shirika ni non profit huko marekani KWA hiyo loko exempt kulipa kodi hivyo ni lazima liheshimu sheria za US. Na kama unavyojua ni kwamba ubaguzi kwa misingi ya ushoga ulishapigwa marufuku marekani na nchi nyingi za ulaya. Na litakuwa ni kosa kwa shirika kumnyima mtu haki zake simply because ni shoga.

  Sasa basi hapa mahesabu ni simple. Kama mtu ameajiriwa na hilo shirika na akataka apewe benefits za same sex marriage..si ni yeye kutoa ushahidi? (just like any other marriage?) na kama Tanzania hizo ndoa hatuzitambui, maana yake ni kwamba hutakuwa na ushahidi. KIFUPI, BENEFITS HUTAPATA. Simple. Labda hilo tangazo linawahusu wa-USA wenyewe au wengine wanaotoka mataifa ambako hizo ndoa zinatambulika. Ambalo siyo kosa kabisa.
   
Loading...