Shirika laomba radhi treni kuondoka sekunde 20 kabla ya muda halisi

nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
7,335
8,116
_98777258_gettyimages-475245508.jpg


Shirika moja la reli Japan limeomba radhi baada ya moja ya treni zake kuondoka sekunde 20 mapema.

Wasimamizi wa shirika la treni za reli ya Tsukuba Express kutoka Tokyo hadi Tsukuba wanasema wameomba radhi sana kwa usumbufu ambao huenda waliwasababishia wasafiri.

Kupitia taarifa, shirika hilo limesema treni hiyo ilikuwa imepangiwa kuondoka saa 9.44.40 (Saa tatu na dakika arobaini na nne na sekunde arobaini na nne) lakini iliondoka saa 9.44.20.

Wengi wa watu mitandaoni, hasa kutoka mataifa mengine wameshangazwa sana na hatua ya shirika hilo
b-shinkansen-a-20141220.jpg


Shirika hilo limesema kosa hilo lilitokana na hatua ya wafanyakazi wake kutoangalia vyema ratiba ya treni kabla ya kuondoka.

Wameongeza kwamba hakuna mteja yeyote aliyelalamika kutokana na hatua ya treni hiyo kuondoka mapema kutoka kituo cha Minami Nagareyama kaskazini mwa Tokyo.

_98780520_japan-tokyo-tsubuka-976-1117.jpg


Tsukuba Express huwasafirisha abiria kutoka Akihabara mashariki mwa Tokyo hadi Tsukuba kwa dakika 45.

Ni nadra sana kwa treni Japan, nchi iliyo ya mfumo wa treni wa kuaminika sana duniani, kuondoka wakati ambao haipangiwi kuondoka.
tokaido-shinkansen-bullet-train-riding-through-downtown-tokyo-picture-id688537758


Reli ya Tokkaido, inayotoka Tokyo hadi Kobe, husafirisha watu karibu 150 milioni kila mwaka.

Shirika laomba radhi treni kuondoka sekunde 20 mapema
 
Hilo ni somo zuri / mujarab kabisa kwa Watoa huduma mbalimbali hasa hasa za Usafiri nchini Tanzania. Wenzetu wanaheshimu sana Wateja wao na wanajua mno kufanya customer care ya hali ya juu. Nina uhakika hali hiyo ingetokea hapa Tanzania wala Abiria wasingeombwa radhi na sana sana wangehoji wangeishia kupewa tu ' matusi ' ya Viungo mbalimbali vya Sayansi ya Uzazi kwa ama Mwanamke au Mwanaume na kusoteshwa mno tu.
 
Angalia wenzetu walivyo makini na mda, funzo kwa mswahili. Mafanikio yao ni halali kwani "time is money "
 
Huku tren ya Mbeya_Dar tuliambiwa inaondoka saa nane mchana_ikaondoka saa kumi usiku,NA WANANZENGO TUPO TU NDANI YA TREN TUNAMSUBIRI DEREVA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom