Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP kununua mahindi ya Tanzania

Sep 5, 2017
24
20
"26Nov 2018
Na Mwandishi Wetu
Nipashe

WFP kununua shehena mahindi nchini

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), limetangaza neema nchini kwa kusema lipo tayari kununua tani za mahindi 150,000.



IMG_2223.jpg

Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa akijadiliana na mwakilishi wa WFP, Michael Dunford na Mkuu wa Usambazaji wa shirika hilo, Riaz Lodhi.​
Aidha, imeahidi kusaidiana na Tanzania kuboresha sekta ya kilimo.

Shirika hilo lilitoa ahadi hiyo wakati wa kikao kati ya Naibu Waziri wa Kilimo, Innocent Bashungwa na mwakilishi wake nchini, Michael Dunford na Mkuu wa Usambazaji wa shirika hilo, Riaz Lodhi, jijini Dar es Salaam, kujadili namna ya kuboresha ushirikiano baina ya serikali na shirika hilo.

Katika kikao hicho Dunford alielezea namna WFP imekuwa ikishirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya kilimo kupitia miradi mbalimbali ikiwamo ya kuboresha lishe, kuongeza thamani ya mazao, utafiti na ubunifu katika kilimo pia katika masoko.

Alimhakikishia Bashungwa kuwa WFP lina nia ya dhati ya kumkomboa mkulima wa Tanzania ikiwa ni sehemu ya Malengo Endelevu ya Dunia (SDG) ya kutokomeza njaa ulimwengu, na kuishukuru serikali kwa ushirikiano ambao imekuwa ikilipatia katika kutimiza majukumu yake.

Naye Bashungwa alimweleza mwakilishi huyo nia ya serikali ya kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri ya mazao ndani na nje ya nchi, ambapo WFP limekubali kununua tani 150,000 za mahindi kutoka ghala la taifa na kuahidi kununua nyingine.

Pia Bashungwa alimhakikishia kuwa serikali itaendelea kurekebisha na kuboresha baadhi ya sheria, ili kurahisisha biashara ya mazao nje ya nchi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), Vumilia Zikankuba na Elimpa Kiranga, Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Chakula."
 
Watanzania wanapenda kuzungumza sana walitakiwa waziachie mamlaka husika zifanye kazi mambo yatakaa vizuri baada ya muda. Japo tunahitaji suluhisho la kudumu kuhusu mazao yetu makubwa ili tusiendeshwe na wafanya biashara kama wanavyoongea wataalamu wengine kwenye sekta ya kilimo.
 
Mmeshanitia Hasara mie, niliuza kwa gunia 18,000 ili nilipenda ada ya watoto na silimi tena, sina uwezo wa kurejea shamba
 
Huchelewi kusikia sasa hv eti kuna wafanya biashara wamejitokeza kwa ajili ya kununua mahindi .... na walanguzi kutokea kwenda kununua kwa wananchi ili wawauzie serikali ndio maana Raisi ameweka jeshi kwenye korosho..!!
 
Aisee Mungu anazidi kushusha neema kwenye nchi yetu,huu utakuwa usiku mbaya sana kwa baadhi ya watu
 
Watanzania wanapenda kuzungumza sana walitakiwa waziachie mamlaka husika zifanye kazi mambo yatakaa vizuri baada ya muda. Japo tunahitaji suluhisho la kudumu kuhusu mazao yetu makubwa ili tusiendeshwe na wafanya biashara kama wanavyoongea wataalamu wengine kwenye sekta ya kilimo.
Sio kila jambo lazima uandike,fahamu haya
1.Wananchi ndio wanaoweka hizo mamlaka na ni haki yao kuhoji na kukosoa,kusifia ni hiyari tu
2.Hakuna biashara bila wafanyabiashara,na bei ya mazao huamuliwa na hali halisi ya soko,hakuna anayekuendesha.
 
Back
Top Bottom