Shirika la ujasusi la Kizayuni lafungua ofisi yake ya uwakilishi Abu Dhabi, UAE

jollyman91

Member
Sep 21, 2021
69
29
Duru za habari zimeripoti kuwa, shirika moja la kizayuni linalotengeneza vifaa vya intaneti vya ujasusi limefungua ofisi yake mjini Abu Dhabi, katika Umoja wa Falme za Kiarabu.

Kwa mujibu wa duru hizo za habari, shirika la kizayuni la AWZ Ventures linalojihusisha na teknolojia ya ujasusi, kuwatambua watu na kudukua taarifa zao kamili, limeanza shughuli zake katika mji wa Abu Dhabi nchini Imarati.

Ripoti za vyombo vya habari zimeeleza kwamba, shirika hilo limekabidhiwa pia kazi ya kuiuzia Saudi Arabia na nchi zingine za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi programu na teknolojia za kutengeza shirika la aina hiyo.

4bvc762d3f77eb1pn0c_800C450.jpg

Shirika la ujasusi la AWZ Ventures lina hisa katika mashirika mengine 18 ya Israel yanayojihusisha na masuala ya intaneti; na maajenti wa zamani wa shirika la ujasusi la Mossad na mashirika mengine ya intelijensia ya Israel na Marekani wanafanya kazi katika shirika hilo.

Tovuti ya SaudiLeaks imeeleza kuhusiana na suala hilo kwamba, wakati shirika hilo la ujasusi la Kizayuni linafuatilia kuuza bidhaa zake kwa Saudi Arabia, hivi karibuni gazeti la Kizayuni la Jerusalem Post liliripoti kuwa hatua mpya zimeanza kuchukuliwa kwa lengo la kustawishwa uhusiano kati ya Riyadh na Tel Aviv na kubainisha kwamba, serikali ya Saudia inaonyesha kuwa na hamu kubwa ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Mwezi Septemba 2020 na kwa upatanishi wa aliyekuwa rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump, Imarati na Bahrain zilisaini mkataba uliopewa jina la Makubaliano ya Abraham, wa kufanya mapatano na utawala ghasibu wa Israel na kuanzisha rasmi mahusiano ya kidiplomasia na Tel Aviv.../
 
Kwasasa hizi ndiyo tenda zenye kuingiza mtonyo mrefu sana,tengeneza software fulani ya kiulinzi na ujasusi iuzie nchi fulani umasikini hutokusogelea abadani.

Sijui TISS yetu inamiliki kampuni ngapi ndani na nje ya nchi ama wao kampuni yao ni Chama tawala tu?
 
Back
Top Bottom