Shirika la TSSF latangaza nafasi mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu

sir venance

Senior Member
Oct 26, 2017
151
222
Shirika la Tanzania social support foundation (tssf), linawatangazia wale wote waliokosa mikopo inayotolewa na hesbl kuwa, wanayo nafasi sasa ya kuomba mikopo kupitia shirika hili, walengwa ni wale wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale wa mwaka wa pili na kuendelea, hii ina makato ya 6 asilimia kwa mwaka, fomu zinapatikana ktk tovuti ya www.tssf.co.tz ,source tssf
 
ofisi zao zipo wapi....tuwaone physically kwanza...isije kuwa wanataka kutupiga 30k zetu za maombi tu
 
Hao wanashida na 50000 yako ya kujiunga ,na mkopo hutapata wakishapiga hiyo 50 watakuambia huna sifa
 
Huko Tssf retention fees ni 6% per year! Usiporudisha kwa mwaka riba ni 18%! Kopeni huku mkijua masharti msije kulia lia hapa baadaye! Kwa mfano: ukipewa mkopo wa milioni NNE, retention fees kwa mwaka wa kwanza ni 240,000/= kwa mwaka wa pili ni 480,000/= , kwa mwaka wa tatu ni 720,000/= kwa hiyo jumla ni 1,440,000/=. Jumla ya mkopo wako ni 12,000,000/= na ukiongeza hiyo retention fee zinakuwa 13,440,000/=.
Mwaka wa NNE ukiwa mitaani unasaka ajira inabidi uanze kulipa! Usipolipa kabisa kwa sababu yoyote ile retention fees yake ni 806,400/= kwa hiyo deni linakuwa 14,246,400/= wakiongeza na riba ya 18% kwa ajili ya kutokurejesha riba ni 2,564,352/= kwa hiyo jumla ya deni ni 16,810,752/=! Usipolipa na mwaka unaofuata retention fees ni 1,008,645/= na ukipiga na riba ya 18% unaingia kwenye zaidi ya milioni 20!
Lengo si kuwatisha Bali kuwatahadharisha! Ukope ukiwa unajuwa wajibu wako unaokusubiri! Ujanja siku zote ni kulipa mapema! Kwa mfano, mdhamini wako aanze kulipa hilo deni tangu ukiwa mwaka wa kwanza, kwa maana hiyo retention fees itakuwa ndogo sana na utakwepa riba ya 18%!
Lakini kama utasubiri mpaka uje kumaliza chuo, kisha upate ajira ndio uanze kulipa, hapo utakuwa mtumwa wa deni na kuja kulimaliza unaweza kujikuta unalipa zaidi ya milioni 30 kwa deni LA milioni 12!
Usifurahie mkopo bila kujipanga utaulipaje! Chonde chonde kibanda cha mdhamini kisije kupigwa mnada! Huwa wanasema mahakama siyo mama yako! Dalali wa mahakama huwa haangalii machozi ya MTU!
 
Mh huku kukopa bila kujua cha moto kitakachokutokea hakufai kabisa bora mtu ujipinde tu na mzazi wako ama mlezi ili ukimaliza chuo uangalie mambo mengine sio kufikiri unalipaje deni la pesa ambayo imeishia kuhonga tu na kununua mishikaki plus balimi
 
Mmmmhhh hapo naona akili kama inanikataza kuomba tssf
Usiogope, ila ujipange! Mkopo uliokuwezesha kusoma unalipa! Maana umekutoa shimoni! Tatizo watanzania walio wengi hudhani mkopo ni fadhila! Hapana, mkopo ni biashara! Lazima uulipe! Ukiulipa kwa wakati, hauumizi, lakini ukijifanya mjanja ularuka ruka, hilo deni litakutesa kwa miaka mingi sana.
Kumbuka pia wanasema marejesho ni asilimia 6 ya mshahara wako! Kwa ushauri wangu ni vizuri kulipa kama heslb wanavyofanya yaani 15%! Hii unaumia kwa muda mfupi na unaliza deni kwa kulipa retention fees kidogo! Lakini ukilipa 6% ya mshahara, deni litachukua muda mrefu kuisha na retention fees yake utalipa nyingi sana!
 
Ila kama wazazi wanaweza kujibana hata kwa shida shida ni afadhali usikope kabisa! Akope tu yule ambaye bila mkopo hana kabisa namna ya kuweza kusoma chuo!
 
tssf wa punguze makali mzgo wa kweli ni heslb pekeeee sht ukimaliza paka pate ajira
 
Wakuu tupeni vigezo vyake ili tuweze kuwaelekeza ndugu zetu huko,maana hii serikali inaona pesa za walipa kodi kama wanatoa wao mfukoni.inaboa sana!
 
Hakuna kitu kama hicho! Kiendacho kwa mganga hakijawahi kurudi!
Ha ha ha! Speaking of that, eti leo kuna mrembo ananipigia nimkopeshe hela atanirudishia kesho! Huo si utapeli huo? Yani ushawahi ona mwanamke analipa mkopo aliopewa na mwanaume kwa pesa tasilimu?
Nikamchomolea...
 
Back
Top Bottom