Shirika la reli Tanzania (TRC) , boresheni huduma train ya deluxe kutoka Dar es salaam kwenda Arusha

Artificial intelligence

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
1,262
2,191
Kwenu shirika la reli Tanzania (TRC), chini ya mkurugenzi Masanja kungu kadogosa, train ya deluxe inayofanya safari zake kutoka Dar es salaam kwenda Arusha kupitia Tanga na Kilimanjaro huduma zake hazikizi viwango.

Ndani ya train mumeweka tv na feni vyote havifanyi kazi.

Sehemu ya VIP, hususani kulala ni kubovu, vitanda vidogo Sana, kumejaa vumbi yaani hakuvutii kabisa hata raha ya abiria kulipia pesa yote hiyo asafiri vizuri haipo.

Sehemu ya bar ni padogo muno kiasi kwamba watu wanajaa, inabidi kupanga foleni kama kupanda mwendokasi.

Viti vya kukalia vimechoka, kwa madaraja yote , seat covers zimejaa vumbi hazifuliwi.

Vyoo ni vichafu Sana haviridhishi, baadhi ya mizigo inachelewa kufika kwa wakati, mzigo kutoka korogwe kufika Arusha unaweza kutumia zaidi ya wiki tatu, hili ni tatizo.

Miundombinu mibovu, hususani kipande cha kuanzia Kilimanjaro kuelekea Arusha train inajaa vumbi yote ndani abiria ni mwendo wa kukohoa mwanzo mwisho.

Ulinzi ndani ya train bado ni tatizo, hivyo mna hatarisha usalama wa abiria na mali zao.

Tambueni ya kwamba train hii inabeba watalii wengi , baadhi yao wanajutia Sana kutumia usafiri huu, huku wakihapa kabisa kutotumia tena usafiri huu. Hali hii inaleta taswira mbaya kwenu shirika la reli na chi kwa ujumla.

Ushauri kwenu, boresheni huduma za train hii na ifanyieni ukarabati kwa sababu imechoka.
 
TRC na TTCL ni mtu na ndugu yake. Yaani jamaa hawa hawako creative kabisa. Usafiri wa kutumia masaa labda 9-10 unatumia siku 2 aisee. Ila poleni wakuu tuendelee kuwa wazalendo tupande hizo treni.
 
Hata usafi kwenye gari moshi unatushinda jamani. Ndio maana wazungu wanatuona kwamba kwenye ubongo wa mtu mweusi kuna tatizo.
 
TRC na TTCL ni mtu na ndugu yake. Yaani jamaa hawa hawako creative kabisa. Usafiri wa kutumia masaa labda 9-10 unatumia siku 2 aisee. Ila poleni wakuu tuendelee kuwa wazalendo tupande hizo treni.
Ni shida tupu, hii train inabeba watalii wengi, Ila ubovu wa huduma zake Una ikwamisha Sana kimapato. TRC iangalieni upya hii train.
 
Back
Top Bottom