Shirika la reli Tanzania laendelea na zoezi la ulipaji fidia Dodoma

Tanzania Railways Corp

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
251
595
Shirika la Reli Tanzania - TRC linaeendelea na zoezi la ulipaji fidia jijini Dodoma kwa wananchi wote waliopitiwa na njia ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa awamu ya pili Morogoro - Makutupora, ambapo Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Mhe. Patrobas Katambi alishuhudia zoezi hilo likiendelea wilayani kwake hivi karibuni April 2020 .

Zoezi hilo la ulipaji wa fidia linaendelea Dodoma mjini katika shule ya sekondari ya Mkonze mtaa wa Chidachi ambapo uliambatana utoaji elimu ya kujikinga dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona katika maeneo yote ambayo zoezi hilo litafanyika.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Patrobas Katambi ameipongeza Serikali ya awamu ya tano ikishirikiana na TRC kwa kutekeleza ibara ya ishirini na nne ya katiba ya nchi ambayo inaeleza kuwa kila mtu lazima apewe stahiki yake kwa wakati na bila shaka wananchi wote waliopitiwa na mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa wanalipwa kwa wakati.

“Kiukweli tunajivunia sana kwani tunaenda kupata mgao wa pili sasa kwa awamu ya pili ya mradi na katika Wilaya ya Dodoma wanaenda kunufaika watu 2394 “ alisema Mhe. Katambi.

Aidha Mhe. Katambi alisema kuwa Serikali inafuata Sheria na kanuni kwa kuwalipa kiasi kinachojitosheleza wananchi wote wanaotoa maeneo yao ya ardhi kwa kutekeleza majukumu ya serikali.

Aidha Mhe. Katambi ameipongeza sana TRC kwa kuweka mikakati ya kujikinga dhidi ya gonjwa la Corona wakati zoezi likiwa linaendelea kwa kuhakikisha kila mtu ananawa mikono na sabuni, na kupaka kitakasa mikono (Sanitizer) kabla ya kupewa hundi na pia kukaa umbali wa mita moja ili kujiepusha na maambukizi ya gonjwa hilo.

Naye Mhandisi Christopher Mang’wela alisema kuwa awamu hii ya zoezi hilo la malipo zitanufaika wilaya tatu ambazo ni Dodoma, Bahi na Manyoni ikiwa hapo awali walifanikiwa kulipa wilaya nne ambazo ni Mvomero na Kilosa Mkoani Morogoro pamoja na Mpwapwa na Chamwino mkoani Dodoma.

Mhandisi Mang’wela amesema kuwa takribani kaya 6224 wamepitiwa na mradi na pia zaidi ya Bilioni 35 zitatumika kulipa watu katika maeneo yote yaliyopitiwa na mradi ikijumuisha nyumba, mashamba , viwanja na pia taasisi mbalimbali zikiwemo za Serikali.

Vilevile Mwanaharakati Cyprian Musiba amemshukuru sana Rais wa awamu ya tano kwa kuwa mtetezi wa wanyonge na kuhakikisha wananchi wote wanalipwa haki zao kwa wakati bila lalamiko la aina yeyote.

“Mimi pia ni mmoja wa wahanga na niliambiwa taarifa za kuchukuliwa eneo hilo wiki tuu baada ya kuhamia“ alisema Bw. Musiba .
FB_IMG_1587557962020.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatua nzuri msisahau kuweka sanitizer na masks za kutosha kwa kila abiria .pia boreshen misosi jamani kwenye misosi mnafeli
 
Back
Top Bottom