Shirika la Posta Tanzania, mna taarifa na shindano hili la mtandaoni?

Alien pilot

Senior Member
Dec 29, 2017
194
224
Kuna ujumbe unatumwa chrome kuwa Shirika la Posta Tanzania (Posts Corporation) linatoa zawadi za sumsung S10 endapo utakuwa umechaguliwa nao kucheza mchezo wao wa kufungua link yenye vibahasha.

Unapewa chaguzi tatu yaani mara ya kwanza unakosa, mara ya pili unakosa lakini ukifika ya tatu unapata kisha inakuja message ya kulipia gharama ya mzigo Tsh. 5490.

Inaonekana ni matapeli wanaotumia jina la shirika letu vibaya. Tunaomba uongozi wa shirika kutolea ufafanuzi kwa sababu linaweza kuwa suala la uhujumu uchumi na kuchafua jina la nchi na mashirika yake.
 
Ni kama hivi watutolee ufafanuzi au ndo kudukuliwa maana wanataka address
IMG-20190812-WA0007.jpeg
IMG-20190812-WA0006.jpeg
IMG-20190812-WA0004.jpeg
IMG-20190812-WA0005.jpeg
 
Mi mwenyewe nimeshacheza zaidi ya mara mbili na nilishinda ila machale yakanicheza kwenye kutuma hela wananiambia eti niingize details za bank account yangu nilipie,michale ikanicheza,

Nikajua hapa kuna kukombwa hela zangu zote za kwenye account yangu,nikaenda kwenye tovuti ya posta ili nione kama kuna shindano la aina hiyo,nikaona chenga tu,nikaachana na huo mchezo wa kipuuzi.

Asante na wewe kwa kuliona hilo mkuu na kulileta huku kwa GT.

Hao ni matapeli
 
haha hawa jamaa wajinga sana ata mimi walinitumia kwenye kutuma pesa hapo ndio palipo nishtua nikajua utapeli tena wa wazi kabisa
 
Mkuu, dunia nzima kuna postal office.
Kuna sehemu yeyote umeona wameandika Tanzania?
 
Ndio link inakuja kwako kama Tanzania posts office na nembo yao ya Rangi ya kahawia so nilipo andika humu nembo wametoa fasta na site imekuwa can't be reached cjui wamelifanyia kazi wengi wametumiwa kama inatoka Tanzania posts office mkuu acha ubishi
Mkuu, dunia nzima kuna postal office.
Kuna sehemu yeyote umeona wameandika Tanzania?
 
angalia tu hiyo link utajua tu ni zile scam/spam site,hapo ukifungua na IPya tanzania itatokea Posta ya TZ,hivyohivyo ya kenya,etc
weka extension za ads blocker,hauta ziona tena,,,,,
 
Ndio link inakuja kwako kama Tanzania posts office na nembo yao ya Rangi ya kahawia so nilipo andika humu nembo wametoa fasta na site imekuwa can't be reached cjui wamelifanyia kazi wengi wametumiwa kama inatoka Tanzania posts office mkuu acha ubishi
Kuna sehemu nimebisha kwani?
 
Back
Top Bottom