Shirika la Posta liboreshwe namna hii washushe na gharama tusinunue ndege nyingine

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,887
Anaandika mange kimambi
Ukielewa haya maneno ya Bilionea huyu utaelewa why kina Mange tulisema toka mwanzo Magu anachezea pesa za walipa kodi kwenye ATCL. Huyu ndo bilionea wa Virgin airways anakwambia kama unataka unatoka kutoka kwenye ubilionea kuingia kwenye umilionea kwa haraka anzisha basi shirika jipya la ndege.

Kuliko hii investment ya ATCL ni mara mia Magu angefanya investment ya huduma ya posta. Hakuna kitu kingewasaidia wafanyabishara wadogo kama huduma ya kutuma vitu. Kama hapa marekani wako tayari posta yao itengeneze hasara milele ila isife sababu kila kitu hapa kinategemea posta. Na huko Tz pia huduma ya posta ikipanuliwa na kuboreshwa uwiii biashara za online zitakuwa nyingi mnoo na bei ya vitu zitapungua.

Katika vitu vya kumlilia mama Samia mumlilie posta. Karne hii ya mfumo wa mitandao posta ndo kila kitu. Auze hayo madege ya ATCL hayo matrilioni aweke vituo vya posta kila sehemu, wawe na tracking system ya kutrack mizigo. Tuko karne ya mitandao inabidi serikali iwawezeshe watanzania kufanya biashara nchini na dunia nzima kupitia mitandao na hatua ya kwanza ni huduma ya posta. Bila posta hakuna biashara za mitandaoni zitafanikiwa. Na posta inabidi iangaliwe kama huduma na sio biashara kwa hiyo hata posta yenyewe ikitengeneza hasara it’s okay maana pesa itarudi serikalini kwa mfumo wa kodi kwa jinsi biashara zitakavyo ongezeka. Posta ya hapa marekani inatengenezaga hasara miaka yooote ila wenyewe wamarekani huwaelezi kitu juu ya posta yao. Wako tayari hata waongezewe kodi ila huduma yao ya posta ibaki kiwango cha juu.

Waziri wa biashara aangalie hili. Tanzania haitoweza kuingia kwenye ushindani wa biashara kupitia mitandao bila huduma ya posta kuboreshwa. Mambo yatabadilika sanaa tena sana kama serikali itajikita sana kwenye kusaidia wananchi kuanza biashara za mitandao kwa kuwaboreshea huduma ya posta.
 
Richard Branson Quote: “The quickest way to become a millionaire in the airline business is to start out as a billionaire.”
 
Back
Top Bottom