Mshikawezi Mwizi
JF-Expert Member
- Jul 24, 2013
- 751
- 374
Ninaandika haya kwa uchungu mkubwa nikiwa na ombi moja kuu kwa mamlaka zinazohusika kulichunguza kwa kina shirika hili, ili kubaini ukweli wa utapeli nitakaoufafanua hapa; kisha hatua husika ziweze kuchukuliwa kwa haraka.
Shirika hili limekuwa likijifafanua kuwa limekuja kutusaidia sisi wakulima wadogowadogo katika shughuli zetu za kilimo kwa kutuwezesha kupata pembejeo za kilimo kupitia mikopo isiyo na riba na kuirudisha mikopo hiyo mara tu baada ya kuvuna na kuuza mazao. Mimi nikiwa muathirika wa mradi huu, walikuja kwangu na kunihoji juu ya ufugaji wa kuku ninaoufanya, baada ya hapo waliahidi kuniwezesha kwa kunipatia vifaa na tiba zote za kuku ili kuboresha uzalishaji. Walinipatia vifaa na dawa mbalimbali za kuku, vyote vikiwa na thamani ya shilingi 180,000/= na kunitaka nianze kurudisha pesa hiyo baada ya miezi mitatu.
Vilevile walinihakikishia kuwa nitakapoanza kurudisha pesa hizi, nitarudisha kwa kila wiki kiasi cha shilingi 18,000/= kwa wiki zisizopungua 10, ila nitakuwa huru kurudisha hata kabla ya muda husika, au kurudisha pesa yote kwa mkupuo mmoja. Baada ya mwezi mmoja niliamua kwenda kuirudisha pesa yao yote kwa mkupuo mmoja, cha ajabu niliambiwa deni langu linakuwa kwa asilimia 35 kwa kila mwezi, hivyo ninadaiwa jumla ya kiasi cha shilingi 243,000/=, kama ningekaa na pesa yao kwa muda tajwa (miezi mitatu) deni langu lingefikia kiasi cha shilingi 369,000/=.
Hali hii ilinisikitisha sana, nilipohoji, nikaambiwa kwa nini ninalalamika wakati wamenisaidia kuongeza uzalishaji; nilipowaambia tatizo si kuongeza au kupunguza uzalishaji bali ni wao kwenda kinyume na maelezo yao, kiongozi wao mmoja mwenye jina lenye herufi za mwanzo L.L alinijibu kwa ufupi, “dawa ya deni ni kulipa”.
Nililipa pesa yao lakini nilihudhunika sana. Naziomba mamlaka husika zifanye kazi za kulichunguza shirika hili kujua ni jinsi gani linafanya kazi zake.