Ni kilio changu cha kimaskini kuwa Shirika la Nyumba linawaondoa wazawa kwenye nyumba za Shirika na kujenga nyumba nyingine na kuziuza kwa bei ya kuanzia milioni mia ambayo kwa mujibu wa shirika hilo, ni bei rahisi kwa Watanzania. kwa hakika watakaozipata nyumba hizo ni wachache wenye kipato kinachoweza kufikia kiasi hicho, na fursa kubwa zaidi itajitokeza kwa Watanzania wenye asili nyinginezo kwa kuwa wao hupiga hesabu za muda na foleni kuwa ni ghali sana ikilinganishwa na kuwa na makazi katikati ya Jiji unapofanyia kazi.
Maoni yangu ni kuwa, shirika lilikuwa linafanya biashara ya kupangisha ambayo lingeendelea na biashara hiyo kwa kuwapangisha watu wengi zaidi kwenye nyumba hizo mpya. Kipaumbele iwe kwa watumishi wa umma ili wawajibike kwenye ofisi zao kwa wakati badala ya sasa ambapo wengine wanakaa Mlandizi lakini wanafanya kazi maeneo nyeti ya ofisi za Serikali, kitu kinachohatarisha hata usalama wa nchi. Iwapo watumishi hao wangepangishwa na kulazimika kukaa kwenye nyumba hizo wakati wa utumishi wao ili kuwajibika kwenye kazi na kiusalama, ingepunguza pia asilimia 70 ya msongamano wa magari asubuhi na jioni kwenye Jiji la Dar kwa kuwa nyumba nyingi zipo karibu na mjini kati.
Kama somo limeeleweka, tujadili na najua wadau muhimu wataisoma na kufanyia kazi.