Shirika la nyumba, apartment milioni mia ni bei rahisi!!!!


J

Jahom

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2008
Messages
349
Points
195
J

Jahom

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2008
349 195
Ni kilio changu cha kimaskini kuwa Shirika la Nyumba linawaondoa wazawa kwenye nyumba za Shirika na kujenga nyumba nyingine na kuziuza kwa bei ya kuanzia milioni mia ambayo kwa mujibu wa shirika hilo, ni bei rahisi kwa Watanzania. kwa hakika watakaozipata nyumba hizo ni wachache wenye kipato kinachoweza kufikia kiasi hicho, na fursa kubwa zaidi itajitokeza kwa Watanzania wenye asili nyinginezo kwa kuwa wao hupiga hesabu za muda na foleni kuwa ni ghali sana ikilinganishwa na kuwa na makazi katikati ya Jiji unapofanyia kazi.

Maoni yangu ni kuwa, shirika lilikuwa linafanya biashara ya kupangisha ambayo lingeendelea na biashara hiyo kwa kuwapangisha watu wengi zaidi kwenye nyumba hizo mpya. Kipaumbele iwe kwa watumishi wa umma ili wawajibike kwenye ofisi zao kwa wakati badala ya sasa ambapo wengine wanakaa Mlandizi lakini wanafanya kazi maeneo nyeti ya ofisi za Serikali, kitu kinachohatarisha hata usalama wa nchi. Iwapo watumishi hao wangepangishwa na kulazimika kukaa kwenye nyumba hizo wakati wa utumishi wao ili kuwajibika kwenye kazi na kiusalama, ingepunguza pia asilimia 70 ya msongamano wa magari asubuhi na jioni kwenye Jiji la Dar kwa kuwa nyumba nyingi zipo karibu na mjini kati.

Kama somo limeeleweka, tujadili na najua wadau muhimu wataisoma na kufanyia kazi.
 
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Messages
23,652
Points
2,000
Shark

Shark

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2010
23,652 2,000
Hawawezi kukuelewa.
Nehemiah Mchechu ameshalewa madaraka, nae ameshakua fisadi a.k.a kibopa now, hawezi kukumbuka maskin kama wewe.

We angalia utaratibu mwengine wa kuweza kujisaidia mwenyewe.
 
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Messages
9,237
Points
2,000
Nyenyere

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined Sep 9, 2010
9,237 2,000
Hivyo mbona ni vijisenti tu.
 
C

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Messages
12,382
Points
2,000
Age
59
C

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2011
12,382 2,000
Hawawezi kukuelewa.
Nehemiah Mchechu ameshalewa madaraka, nae ameshakua fisadi a.k.a kibopa now, hawezi kukumbuka maskin kama wewe.

We angalia utaratibu mwengine wa kuweza kujisaidia mwenyewe.
Amesifiwa sana takataka tupu!!!!
 
snochet

snochet

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2011
Messages
1,272
Points
1,225
snochet

snochet

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2011
1,272 1,225
nijuavyo mimi,main aim ya shirika la nyumba ni kujenga makazi bora kwa wananchi wake,kuwakodishia kwa bei nafuu,na kuwauzia kwa bei nafuu,sasa milioni mia ni bei nafuu?pesa ambayo asilimia zaidi ya 80 ya watanzania,wanazisikiaga tu kwenye habari....hii nchi ni wizi wizi wizi wizi kila kukicha....Mungu atusaidie tu,tujitahidi kwa haki na sisi tuwe na mafanikio siku moja.
 
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2012
Messages
7,464
Points
1,250
Nivea

Nivea

JF-Expert Member
Joined May 21, 2012
7,464 1,250
nikiona kitu NHC huwa najisikia vibaya sana hawa jamaa walinipandishia kodi kwenye biashara yangu na kunizidishia squre mita kiasi kwamba hela yote niliyokuwa natengeneza iliishia kwenye kodi hatimae nikakata tamaa na tr 1may 2012 ile biashara yangu ikafa kumbe there waz mhindi behind me aliyekuea analiaka lile eneo .so hawa watu bwana hawako kwa maslahi ya taifa kabisa wala wananchi mbavu wale yaani nawachukia sana.
 
MTOTO WA KUKU

MTOTO WA KUKU

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2012
Messages
2,196
Points
2,000
MTOTO WA KUKU

MTOTO WA KUKU

JF-Expert Member
Joined May 3, 2012
2,196 2,000
NHC wana utani na watanzania...wanakwambia wanauza hizo nyumba kwa bei rahisi...MILIONI 100!!!milioni 100 Kweli unamwambia mtanzania wa kipato cha chini si unamtusi!...sasa hivi hilo shirika siyo kwa ajili ya wanyonge....lipo kwa ajili ya wenye nazo...malengo mazima yaliokusudiwa enzi za mwalimu hayapo....hii nchi hii imeoza kabisa

Sent from my HTC Sensation XL with Beats Audio X315e using Tapatalk 2
 
Brodre

Brodre

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2012
Messages
2,123
Points
1,500
Brodre

Brodre

JF-Expert Member
Joined Aug 23, 2012
2,123 1,500
nyingi wamekalia ma patel wenye uwezo... hawa watu wanahela za kujenga majumba lakini wanang'ang'ania nyumba za NHC viongozi hawawezi jiuliza ni kwanini iko hivyo? kwanini wasijaribu kuwapa wazawa ili kama kuna faida wapatayo.hawa ma patel wazawa ndo wafaidike nayo inauma men.... ipo cku i.can sense that watanzania hatutakuwa mbumbumbu daima
 
mtotowamjini

mtotowamjini

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2012
Messages
4,538
Points
0
mtotowamjini

mtotowamjini

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2012
4,538 0
nyumba million moja? ipo maeneo gani
 
dist111

dist111

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2012
Messages
3,162
Points
2,000
dist111

dist111

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2012
3,162 2,000
Kabla huduma hazijaanza! nilikuwa nafuatilia kwa makini nyumba zao, nikajua watatuuzia hata mil 30, na mwisho mil 50! Nilipokuja kusikia zile za 320mil! Nikasema NHC na serikali yao woote walaaaaaniwe!
 
J

JF Tanga one

Member
Joined
Nov 19, 2012
Messages
28
Points
0
J

JF Tanga one

Member
Joined Nov 19, 2012
28 0
nyumba million moja? ipo maeneo gani
We nawe huoni, vaa miwani. Milion moja kasema nani? c kila mtu angenunua, na kusingekuwa na Tangazo yaani ungeshtukia zimeisha tu. Soma vizuri ni MILLIONI MIA ndo kuanzia hapo.
Tutakaa uswazi hadi tufe aisee!
 
Monyiaichi

Monyiaichi

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2012
Messages
1,826
Points
1,250
Age
62
Monyiaichi

Monyiaichi

JF-Expert Member
Joined Jul 5, 2012
1,826 1,250
Hawawezi kukuelewa.
Nehemiah Mchechu ameshalewa madaraka, nae ameshakua fisadi a.k.a kibopa now, hawezi kukumbuka maskin kama wewe.

We angalia utaratibu mwengine wa kuweza kujisaidia mwenyewe.
nilimsikiliza jana, nikashangaa sana, kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa. amenikumbusha meti wangu mmoja ambae miaka fulani nyuma alipata shida, akaandika barua ya mkopo wa sh. 50,000. ilikuwa miaka ya tisini na... yule bosi kwa mshangao kabla ya ku-sign akauliza, hivi kuna staff hana mil.50 kwenye a/c?! kwamba elfu amsini anazipeleka wapi?
alipotushirikisha tukabaki tunashangaa jinsi watu walivyo na hela, tena za wizi (maana nyingi hivo haziwezi kuwa za halali), kisha wanashangaa watu wasiokuwa nazo.
huyu mchechu nae bila shaka kaishajikusanyia. milioni 100 anatufanya watz tuchanganyikiwe tu, anaziona ndogo tunamudu, sijui labda watauziana wao kwa wao wenye hio michango ya kodi zetu.mh
 
M

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2011
Messages
1,422
Points
1,225
M

Mjenda Chilo

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2011
1,422 1,225
Im completly against. Huwezi jenga nyumba city centre halafu ukauza. urban economics inasemaje? jenga nyumba pangisha, wapangaji majority ni watu wanaoanza maisha, graduates nk wape ten yrs baada ya hapo unawapiga ka fine kwenye kodi kwa kushindwa kumiliki makazi suburbs, wawekee mazingira ya kununua nje ya mji nje ya mji kwa mortgage nk. Kinachofanyika sasa NHC ni sawa na lile zoezi la magufuli la nyumba za serikali. Jiulize oportunity ya mtoto wako kununua nyumba. Mchechu na kundi lake la mabanker aliowajaza pale NHC wanataka short term achievments, wauze very potential properties halafu watuletee figures za ajabu. Hebu niambie how do u replace a property in masaki? ni short cut wanaitumia kupata capital at a very very big future costs. wataalam wanasema location is location is location, mchechu na mabanker wake hawalijui hili? zile nyumba walizojenga chalinze zimewasaidia nini? ubepari ni mfumo dhalimu sana.
 
Mzalendo wa ukweli

Mzalendo wa ukweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Messages
559
Points
0
Mzalendo wa ukweli

Mzalendo wa ukweli

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2012
559 0
Ni kilio changu cha kimaskini kuwa Shirika la Nyumba linawaondoa wazawa kwenye nyumba za Shirika na kujenga nyumba nyingine na kuziuza kwa bei ya kuanzia milioni mia ambayo kwa mujibu wa shirika hilo, ni bei rahisi kwa Watanzania. kwa hakika watakaozipata nyumba hizo ni wachache wenye kipato kinachoweza kufikia kiasi hicho, na fursa kubwa zaidi itajitokeza kwa Watanzania wenye asili nyinginezo kwa kuwa wao hupiga hesabu za muda na foleni kuwa ni ghali sana ikilinganishwa na kuwa na makazi katikati ya Jiji unapofanyia kazi.

Maoni yangu ni kuwa, shirika lilikuwa linafanya biashara ya kupangisha ambayo lingeendelea na biashara hiyo kwa kuwapangisha watu wengi zaidi kwenye nyumba hizo mpya. Kipaumbele iwe kwa watumishi wa umma ili wawajibike kwenye ofisi zao kwa wakati badala ya sasa ambapo wengine wanakaa Mlandizi lakini wanafanya kazi maeneo nyeti ya ofisi za Serikali, kitu kinachohatarisha hata usalama wa nchi. Iwapo watumishi hao wangepangishwa na kulazimika kukaa kwenye nyumba hizo wakati wa utumishi wao ili kuwajibika kwenye kazi na kiusalama, ingepunguza pia asilimia 70 ya msongamano wa magari asubuhi na jioni kwenye Jiji la Dar kwa kuwa nyumba nyingi zipo karibu na mjini kati.

Kama somo limeeleweka, tujadili na najua wadau muhimu wataisoma na kufanyia kazi.


Mmhhh,mi napita ntarudi baadaye kuja kuchangia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mrimi

Mrimi

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2011
Messages
1,702
Points
1,250
Mrimi

Mrimi

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2011
1,702 1,250
come on, ongeza sifuri mbili mbele, una makeng.. nn
Mweeh,jamani!
Huyu ndiye mtanzania anayejegewa hiyo nyumba unayomshauri aongeze hizo sifuri mbili! Sio makengenza,akina Mchechu wanatakiwa kusoma maoni yake,waone uwezo wa watanzania!
 
Root

Root

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
29,918
Points
2,000
Root

Root

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
29,918 2,000
Watanzania kwa kulalamika badala ufanye kazi upate hela ununue unakaa hapa na kulalamika.
Angalia kwanza sehemu nyumba imejengwa
Angalia pia ubora wa nyumba na vitu vilivyo ndani ya nyumba
Pia hujalazimishwa kununua nyumba city center kuna nyumba kibao huko bagamoyo


jamani ni maoni yangu tu
 
Nicole

Nicole

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2012
Messages
4,282
Points
0
Nicole

Nicole

JF-Expert Member
Joined Sep 7, 2012
4,282 0
Hiyo ndiyo tabia ya ma-estates manager wao, kula njama na wahindi kuwapandishia kodi wazawa then ukishindwa kulipa wanakutoa anawekwa mhindi, afu estate manager anapewa kidogo chake, wana hela hao maestate manager balaa, na wanazipata kwa dili hizo za kupandisha kodi na kuwauzia wenye nazo.................
nikiona kitu nhc huwa najisikia vibaya sana hawa jamaa walinipandishia kodi kwenye biashara yangu na kunizidishia squre mita kiasi kwamba hela yote niliyokuwa natengeneza iliishia kwenye kodi hatimae nikakata tamaa na tr 1may 2012 ile biashara yangu ikafa kumbe there waz mhindi behind me aliyekuea analiaka lile eneo .so hawa watu bwana hawako kwa maslahi ya taifa kabisa wala wananchi mbavu wale yaani nawachukia sana.
 

Forum statistics

Threads 1,285,183
Members 494,498
Posts 30,852,915
Top