Shirika la Ndege nchini ATCL lakabiliwa na Uhaba wa Marubani!! Serious?.

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Shirika la Ndege nchini ATCL linalomiliki ndege mbili aina ya BOMBERDIER Mhandisi Ladislaus Matindi, amewaeleza Waandishi wa habari kuwa, shirika hilo linakabiliwa na changamoto zikiwepo;

==Ucheleweshwaji wa ndege
==Kutokuwa na ndege maeneo yaliyopaswa kuhudumiwa na ndege za shirika hilo.

Ameeleza tatizo ni kutokana na shirika hilo kuwa na IDADI NDOGO YA MARUBANI ambapo hadi sasa kuna marubani wanne tu huku wengine wapo mafunzoni.

Je huyu Mhandisi anatosha katika nafasi yake hiyo ya Ukurugenzi?
 
Zile ndege kwani ni za ATCL au ni za serikali ila zimekodishwa ATCL?
Mkuu hizi ndege zilinunuliwa na Serikali bila mkopo. ATCL ni kampuni ya Serikali na sio ya watu binafsi au makampuni mengine.

Kwa wale wagumu wakuelewa vitu "Zimenunuliwa haziku kodishwa".
 
Serikali imesomesha marubani wangapi...au INA mpango gani wa kusimesha marubani..??
 
Marupurupu yapo tuje?ata kama mshahara mdogo sio issue muhim nikipaa tu nataka changu,afu sitak nikatwe nssf.
 
Mkuu hizi ndege zilinunuliwa na Serikali bila mkopo. ATCL ni kampuni ya Serikali na sio ya watu binafsi au makampuni mengine.

Kwa wale wagumu wakuelewa vitu "Zimenunuliwa haziku kodishwa".

Ziko chini ya TGFA, then zimekodishwa/leased ATCL.. legally sio za ATCL, ni za TGFA

Why..? Bcoz ATCL wanadaiwa sana madeni makubwa ya kihuni tu, kutokana na mikataba feki walioingia miaka ya nyuma, so serikali ikafanya
hivyo kukwepa ATCL kushtakiwa na wadaiwa, so ATCL wana operate tu, but ni za TGFA

TGFA ni kitengo maalum cha Anga cha Mh. Rais, ni ndege za Rais ziliko, in other meaning, ATCL imeekwa chini ya usalama maalum na ulinzi, na makachero kibao thru TGFA, tit for tat..

TGFA is like Air Force One in other words, ila inatoa huduma za anga kwa Mh. Rais Bara, Rais Znz, Makamu wa Rais bara, Makamu wa Rais Znz na Waziri Mkuu.. wako makini sana sana, but makachero tupu nijuavyo..
 
Kwanini wasije huku Chuo cha Marubani Tabata Magengeni kuchukua deiwaka? Mbona Daladala zinapiga mzigo na deiwaka na faida inaingia tu.
 
Serikali imesomesha marubani wangapi...au INA mpango gani wa kusimesha marubani..??
Wapo marubani wanne nchini Canada sasa hivi wanapigwa msasa. Pia kuna kundi lingine litakwenda siku si nyingi zijazo baada ya hao wanne kuwa wameshahitimu.
 
Wapo marubani wanne nchini Canada sasa hivi wanapigwa msasa. Pia kuna kundi lingine litakwenda siku si nyingi zijazo baada ya hao wanne kuwa wameshahitimu.
Acheni blablaa nyingi...!?

Semeni mmekosa abiria na sio kusingizia Marubani.

Mbona wakati makamu amekodi ilipata rubani? Au kipindi cha mazishi ya Sitta RIP ilipata rubani?
 
Rubani anataka alipwe pesa ndefu nani ataenda hapo?

NI habari ya ajabu sana unanunua ndege ya mbii kwa USD 54,000,000 halafu miezi miwili baada ya delivery kwa mbwembwe unalalamika hazina marubani! Wakati mnapanga kununua mlifikiria zitaendeshwa na nani?
 
Acheni blablaa nyingi...!?

Semeni mmekosa abiria na sio kusingizia Marubani.

Mbona wakati makamu amekodi ilipata rubani? Au kipindi cha mazishi ya Sitta RIP ilipata rubani?
Mkuu najaribu kukuelezea facts wewe unaleta siasa za vijiweni. Hakuna shirika la ndege linalo take off na ghafla tu likaweza kununua airbus.

Awamu zilizopita zilikubaliana na mizengwe na upigaji lakini sio hii ya tano. Wape muda uone mambo makubwa watakayofanya. Ukiingiza siasa za makamu wa rais na mambo mengine utakuwa unapoteza muda na nguvu zako bure.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom